G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Nijikite moja kwa moja kwenye msamaha wa Babu Seya na Nguza
Hapa naona kama rais Magufuli amefanya siasa kutokana na ukweli kuwa amepingana na hukumu waliyopewa hawa watu na ushahidi uliothibitisha makosa yao.Kama sivyo basi ipo vita ambayo ameamua kuianzisha kwa kusudi fulani ikiwa ni pamoja na kunusa kuwa huenda hukumu aliyopewa Babu Seya na mwanae haikuwa sahihi?
Ikiwa rais anapaswa kutoa msamaha kwa wafungwa. Huwa hasemi ninawasamehe fulani na fulani kama alivyofanya kwa babu Seya na mwanae tofauti na pale alipoanza mfano kusamehe wale wenye miaka 85 ns kuendelea kwa maana kuwa lile kundi lote limenufaika na msamaha tofauti na alivyofanya kwa Babu Seya na mwanae maana hawa pekee ndiyo walionufaika na msamaha na siyo kundi fulani.
Hapa rais alitakiwa ama atoe msaha kwa wafungwa wote waliowahi kuhukumiwa kutokana na kupatikana na hatia ya kulawiti ili kuleta maana.Hapa rais kwa mara nyingine ameteleza na ategemee kuzuka kwa mjadala mkubwa juu ya hili. Aidha tayari rufaa zote zilishakatwa hivyo hukumu ilikuwa imefikia tamati! Kwanini uwe ni msamaha wa kubagua? Vipi kwa hawa "walawiti" wengine?