Tunahitaji mfumo mpya wa kijasusi?

kuna kitengo cha wachapakazi hasa kiko jeshini.., kitengo cha ujasusi ambacho hadi sasa kiko free from politics ni CMI (central military intelligence)..., lakini upande wa foreign assets ndo wazuri sana wako bize kukusanya taarifa hatarishi dhidi ya nchi yenu hiyo...,

Hawa wamegawanyika..., kuna wanaofanya kazi kufatilia mienendo na tabia za maofisa na askari ndani ya vikosi hata nje,

kuna wakusanya habari za ndani ya nchi zenye maslahi na jeshi, mfano kuna watu kazi yao ni kusoma magazeti daily, magazeti ya ndani na hata ya majirani au kuangalia tv, au kushinda kwenye mitandao kama humu, pia kuna ambao kazi yao ni kunasa mawasiliano ya jirani zenu...,

na kuna foreign assets.., wanaishi na kukaa nje...., kuna wanaotumwa for a specific mission na kuna wanaokaa tu huko kukusanya taarifa yoyote ambayo ina maslahi na usalama wa nchi.., na wapo ambao ni infiltrated kwny majeshi jirani na serikali za jirani

hawa ndo wamebaki kuwa pillar ya nchi from outside threats

Ila ile cream ilokua trained russia, israel, cuba ndo inastaafu..., wamebaki wale mnaowafundisha pale mikumi

...duu we jamaa nomaaa dah..!!??
 
Wakuu hebu tutafute kwanza mstakaabali wetu kwanza!; tujue uozo uko wapi na tuuondoe kwa any price! Vichwa vya uhakika vimo humu, hata hao isi, mosad, kgb, cia, m16...Walianza kama mchicha! Hatujachelewa....
 
Intelligence yetu haina plan zozote za kuzia watu wao wasiwe addicted na targets zao.Na ukizingati waafrica hswa watz wanavyopenda addiction.Utakuta usalama kawa addicted na CCM, dini yake,wanawake ,pombe,sifa za kijinga za kutumia hofu na access kutafutia sifa bar,na kutesa watu km vile kawa mlizi wa familia,marafiki na mahawara zake.
 
Huwezi kuimarisha ulinzi wakati watu wanaingia nchini kiholela ati kwa sababu tu ni member wa EAC. Subirini matokeo yanakuja very soon.

Hii nimeipenda. Tena wachukue mfano wa yule mwanajeshi aliekimbia jeshini wakati wa oparesheni flan
 
Miaka 50 ya Uhuru: Tunahitaji mfumo mpya wa kijasusi

Godfrey Dilunga

TAKRIBAN miaka 17 iliyopita, Januari mwaka 1994, aliyekuwa Rais wa Urusi, Boris Yeltsin, aliunda upya Shirika la Kijasusi nchini humo, maarufu kama KGB (Komitet Gosudarstvennoy Bezopasnosti).

KGB (Kiingereza; Commitee for State Security )ni kati ya mashirika makubwa ya kijasusi duniani yaliyopata kutambulika hivyo. Mwaka 1983 kwa mfano, Jarida la Time liliripoti kuwa shirika hilo ni bora zaidi katika kukusanya taarifa za kijasusi.

Wakati Yeltsin akiwa madarakani, KGB ilikuwa chini ya Wizara ya Usalama ya Urusi. Uamuzi huo wa kuvunja wizara na shirika hilo lenye rekodi ya ubora duniani linatusogeza katika swali la msingi; je, kwa nini Yeltsin alichukua uamuzi huo?

Kwa nini aliamua hivyo tena akipuuza rekodi kongwe na bora ya shirika hilo? Maelezo yaliyotolewa nyuma ya uamuzi huo ni kwamba; shirika hilo halikuweza kukabili changamoto za mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa kama alivyotaka Rais.

Kwa lugha nyingine, KGB ilikuwa kikwazo kwa Rais Yelstin kuongoza nchi kwa kasi aliyoitaka hususan mabadiliko ya msingi kiuchumi na kisiasa.

Ingawa katika kueleza sababu za uamuzi huo Yeltsin pia alikuwa na ‘hasira’ binafsi, lakini angalau pia ndani ya uamuzi wake aligusa mambo ya msingi kwa maslahi ya nchi yake.

Ndiyo, Yeltsin alikuwa na ‘hasira’ binafsi pia na hasa pale alipopata kueleza kuwa kati ya sababu za uamuzi wake huo dhidi ya KGB ni pamoja na shirika hilo kwa kushirikiana na Wizara ya Usalama, kutompa taarifa kamili za uchaguzi.

Alidai KGB na Wizara ya Usalama kwa pamoja walishindwa kumpa taarifa kamili juu ya uwekezano wa chama cha Liberal Democratic (LDP), kupata ushindi katika uchaguzi mdogo uliofanyika Desemba 12, mwaka 1993.

Pengine kwanza tuelezane baadhi ya kazi za msingi za KGB ambazo ziko bayana katika machapisho mbalimbali ya masuala ya ulinzi na usalama na labda, kwa kuzingatia kazi hizo, Yeltsin aliona kuna tatizo na hivyo mabadiliko yalihitajika.

Mbali na jukumu la kupambana na mitandao mizito ya uhalifu, KGB ilikuwa na majukumu mengine ambayo ni kukabili mbinu za majasusi wa nchi nyingine ambao huingia Urusi kwa malengo maalumu.

Malengo hayo maalumu ni pamoja na kutaka kujua siri za nchi hiyo ambazo zinaweza kutumika na nchi nyingine hasimu kusababisha maafa au kuyumbisha Urusi (wakati huo Umoja wa Kisovieti).

Ili tuelewane vizuri zaidi kuhusu eneo hilo mahususi kimajukumu (nchi moja kufanya ujasusi dhidi ya nchi nyingine), nirejee mfano wa tukio la Aprili, mwaka 1999, wakati Marekani ilipofanyiwa ujasusi na China ambayo kupitia kwa ‘jasusi’ wake waliiba teknolojia kutoka maabara ya Marekani.

Ilikuwa hivi; Aprili, 1999; Marekani (kupitia shirika lake la ujasusi CIA- Central Intelligence Agency) ilikuwa ikiendelea na uchunguzi dhidi ya wizi wa taarifa za siri kuhusu masuala ya nuklia, kwenda China.

Aliyekuwa Waziri wa Nishati wa Marekani, Bill Richardson, Aprili 28, mwaka huo alithibitisha kuwa, Wen Ho Lee, mwana-sayansi wa kichina (jasusi?) aliyekuwa akifanya kazi katika Maabara ya Taifa la Marekani ya Los Alamos, amefukuzwa kazi tangu mwezi uliopita (Machi).

Alifukuzwa kwa tuhuma za kuiba siri hizo na kuzituma kwao China. Katika ‘wizi’ wake, Wen Ho Lee, alifanikiwa kusafirisha kiwango kikubwa cha takwimu (data) kutoka kompyuta za Marekani zenye kiwango cha juu cha ulinzi.

Tukio hili lilikuwa zito katika masuala ya usalama Marekani na Aprili 21, mwaka 1999, maofisa ujasusi wa Marekani walifanya tathmini na kutoa taarifa kwa Rais na Bunge (Congress).

Katika taarifa hiyo walikiri kwamba China imefanikiwa kunasa data kuhusu silaha za nyuklia na kwa hivyo, China ipo rasmi katika ujasusi dhidi ya Marekani.

Kama nilivyoeleza awali, huu ni mfano tu kwa hiki ninachoeleza kuhusu uamuzi wa Yeltsin kuvunja KGB na moja ya majukumu ya KGB kuwa ni kudhibiti majasusi wa nchi nyingine wanaoingia katika nchi yao.

Majukumu mengine ukiondoa hilo na mfano niliotumia, ni pamoja na kuhakikisha ulinzi wa nchi, kuendesha oparesheni maalumu za kijasusi, kudhibiti huduma za mawasiliano baina ya Rais na Serikali na masuala mengine nyeti.

Baada ya uamuzi huo wa Yeltsin kuvunja KGB, itakumbukwa kuwa msemaji wake (Rais) kwa wakati huo, Viacheslav Kostikov, alitoa ufafanuzi kuhusu hatima ya majasusi ambao ‘kibarua’ kimefikia mwisho.

Kostikov alieleza tu kwamba wafanyakazi waliokuwa wa Wizara ya Usalama watahamishiwa katika idara nyingine za Serikali na baadhi ya majasusi watahamishiwa katika shirika jipya litakaloundwa kwa vigezo maalumu.

Pengine kama ilivyokuwa kwa Rais Yeltsin, hata hapa Tanzania kwa sasa kuna viashiria dhahiri hatuna mfumo imara wa kijasusi na kimsingi, tunahitaji marekebisho makubwa ambayo kimsingi ni sawa na kuweka mfumo mpya.

Sijui kwa kina kuhusu masuala yetu ya kiusalama (kijasusi) lakini ni dhahiri kuna udhaifu wa mfumo wetu huo. Udhaifu huu unadhihirika katika baadhi ya michakato ya kitaifa, hasa masuala ya uchumi.

Mfumo wetu wa utafutaji taarifa nyeti hauna tija na kimsingi una mianya inayoruhusu nchi kudanganywa au kutapeliwa kirahisi mno hata na kampuni kubwa za kimataifa.

Baadhi wanaamini mfumo wetu bado ni imara isipokuwa taarifa hizo nyeti, mara kwa mara hazitumiki ipasavyo au hupuuzwa kabisa. Hoja hii ni nyepesi mno na binafsi siamini hivyo.

Mfumo wa kiusalama ambao una mianya inayotoa fursa kwa taarifa zake nyeti zilizokusanywa kwa njia hatari na gharama kubwa kutotumika hata kama zinabeba maslahi ya nchi, huo ni mfumo dhaifu.

Mfumo wa namna hiyo unapaswa kuvunjwa au kufanyiwa marekebisho makubwa. Mfumo wa kiusalama lazima si tu uwe na uwezo mkubwa wa kusaka taarifa nyeti kwa njia yoyote (halali au kinyume chake), lakini pia unapaswa kujijengea mazingira ya kuhakikisha matumizi bora ya taarifa hizo kwa maslahi ya nchi.

Kwa mfano, kama kweli tunao mfumo imara wa kukusanya hizo taarifa kwa nini yameibuka madudu mwengi kwenye mchakato wa ubinafsishaji?

Hata ukiangalia michakato mingine muhimu kwa taifa ‘mikono’ ya kitapeli umeshindwa kudhibitiwa, kwa nini? Ni dhahiri mfumo wetu ni dhaifu isipokuwa swali la kujiuliza; je, udhaifu huo uko kwenye eneo gani mahsusi?

Je, ni eneo la ukusanyaji taarifa au ni matumizi ya taarifa husika? Au vyote viwili? Ndani ya maswali haya, ufumbuzi muhimu unaojitokeza ni kwamba; tunahitaji mfumo imara zaidi wa kiusalama nchini na hasa kwenye eneo la uchumi na siasa kama ilivyo kwa Urusi ya Yeltsin kwa wakati ule.

Mfumo ambao si tu utakusanya taarifa kwa mujibu wa mahitaji lakini pia taarifa hizo zitajengewa mazingira ya lazima ili kutumika kwa manufaa ya nchi. Hakuna sababu ya kuendelea kuwa na mfumo ambao utekelezaji wa taarifa zake unategemea upeo wa kiongozi mkuu pekee, ingawa pia natambua Rais ni taasisi.

Tujenge mfumo ambao ingawa utahitaji wanasiasa, wachumi, wahandisi, wanasheria na wanataaluma wengine lakini kamwe usiwe na maslahi ya moja kwa moja na makundi hayo wakati wote. Kwa sasa, inawezekana mfumo wetu umefungamana zaidi na utashi wa baadhi ya wanasiasa kuliko utaifa.

Tunahitaji kujenga mfumo mpya imara wa kiusalama ambao utakuwa karibu na taaluma zote nyeti lakini hautafungamana na maslahi ya taaluma hizo wala wanataaluma husika.

Hii itasaidia kujenga mwelekeo wa taifa katika mazingira halisi ya mwelekeo wa dunia na si mazingira ya utashi wa wanataaluma au wanasiasa husika.

Kwa bahati mbaya, mfumo wetu wa sasa umejenga hisia kwa umma kwamba umetekwa na wanasiasa na zaidi, ni mfumo uliowekeza zaidi katika siasa kuliko eneo la uchumi. Chombo chetu hiki lazima ‘kicheze’ vilivyo na kwa ustadi ‘disco’ la dunia kuhusu uchumi na siasa.

Hisia kwamba mfumo wetu wa kiusalama ni dhaifu zina ushahidi. Pale tulipopaswa kudhibiti au kuchukua hatua kabla, tumeshindwa kufanya hivyo na hatimaye kufikwa na madhara yasiyo ya lazima.

Matapeli ‘wasiojaa hata mkononi’ wanaingia popote na kufanya wizi wa mali za umma. Wengine wanafanya hivyo wakijiita wawekezaji wa kimataifa ambao baadhi ya makuwadi wao ni wanasiasa au wataalamu wetu ‘mashuhuri’ nchini.

Kama tunafeli kudhibiti masuala yaliyoko ndani ya uwezo wetu tutawezaje kupanga na kutekeleza mipango ya kupata taarifa nyeti kutoka kwa mataifa mengine ili tujenga taifa bora zaidi katika ushindani wa kidunia?

Kwa nini hata wale wanaojifunza au kuchipukia kwenye utapeli wa kimataifa (wawekezaji), Tanzania iwe sehemu yao ya mazoezi?
Katika mwaka huu wa 50 tujiulize na kutafakari je, tunasababu ya kuendelea kuwa dhaifu ndani ya nchi yetu na hata nje ya nchi? Kama jibu ni hapana, basi sehemu ya kuanza kufuta udhaifu huo ni kuimarisha au kujenga upya mfumo wetu wa kiusalama. Happy birthday Tanganyika.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika

Ni kweli mkuu mfumo wetu ni dhaifu na unaendelea kuprove failure
 
Mbona wamerakani walienda kumchukua Osama Bin Laden na kumuua bila ya wao kujua??? Je CIA taarifa walizipata wapi? Hebu jifunze kuunganisha dots bana!

September 11th unaiongeleaje, cia nsa fbi mbn hawakuizuia, na kwavipi unaamini kuwa isi hawakuiuzia taarifa cia, na kwa kuogopa machafuko ya al qaida nchini mwao wakaamua kukana kujua taarifa hizo, ama hujui kama huwa kuna vitu kama hivyo, simply fikiria, umetoka na hela zako benki, watu wanakufata wanazichukua kwa mtutu, how did they know you have enough money
 
Mkuu hakuna mpepelezi anayeongoza kama akina Jack Baur na kina Wily Gamba, Joram Kiango n.k.
Ila kunakuwa na Unit flan ndani ya agencyambayo ndio inakuwa inategemewa sana lakini sio mtu individual.

Mkuu hujawai ona umemtongoza demu akakutolea nje af mpingauonevu akafanikiwa, mtu akatumwa taarifa zako zikamchukua mwaka mzima na mwingine akazipata baada ya mwezi, hujaona tofauti ya watu hapo
 
September 11th unaiongeleaje, cia nsa fbi mbn hawakuizuia, na kwavipi unaamini kuwa isi hawakuiuzia taarifa cia, na kwa kuogopa machafuko ya al qaida nchini mwao wakaamua kukana kujua taarifa hizo, ama hujui kama huwa kuna vitu kama hivyo, simply fikiria, umetoka na hela zako benki, watu wanakufata wanazichukua kwa mtutu, how did they know you have enough money

Is all about creating fear
 
Naomba nitoe angalizo.
Naona watu wanatolea mifano kwa kuitaja sana CIA. Kwa taharifa yenu Intelligence agency ambayo ni high efficiency na kiwango zaidi Duniani ni ile ya Pakistan, ISI.
Wewe nawe umeshadidia tu Pakistani, changia vitu vinavyoeleweka, Pakistani wala ngada kila siku wanalipuliwa na taliban ya mullar omar, wa tz kibao wanaingia na kutoka wakiwa wamebebelea magunia ya madawa ya kulevya, sasa hiyo nchi unawezaje kuwalinganisha na CIA,
 
Wewe nawe umeshadidia tu Pakistani, changia vitu vinavyoeleweka, Pakistani wala ngada kila siku wanalipuliwa na taliban ya mullar omar, wa tz kibao wanaingia na kutoka wakiwa wamebebelea magunia ya madawa ya kulevya, sasa hiyo nchi unawezaje kuwalinganisha na CIA,
Bro mimi nimebezi kwenye research zilizofanywa na wenye taaluma zao. sijabezi kwenye movies.
 
Hiyo namba 6 na namba 7 aaah namba hizo zinachezewa sana wanatuyumbisha nina wasiswasi na uzalendo wa namba 6 na 7
 
Hiyo namba 6 na namba 7 aaah namba hizo zinachezewa sana wanatuyumbisha nina wasiswasi na uzalendo wa namba 6 na 7
 
Hizo namba 6 na namba 7 aaah namba hizo zinachezewa sana wanatuyumbisha sana nina wasiswasi na uzalendo wa namba 6 na 7
 
Hizo namba 6 na namba 7 aaah namba hizo zinachezewa sana wanatuyumbisha sana nina wasiswasi na uzalendo wa namba 6 na 7
 
Back
Top Bottom