Tunahitaji mfumo mpya wa kijasusi?

Hapo kwanza tujue kuwa mtanzania yeyote yule mwenye akili timamo ni usalama wataifa.Nasema hv kwa sabbu vko vtendo vingi vinafanyika vya kuihujumu nchi na vinasabbsha nchi iingie kwenye hasara kubwa sana. Vitendo hv kama wananchi wangejua haki yao ya kutoa taarfa nchi yetu ingekua mbali sana.
 
Hahahahah,
hakupitia INFORMATION LITERACY HUYU,DUNIA YA LEO UTAKWEPAJE SOS ZA NET?
wapi? ulikosomea masters Rukwa? walikueleza reference za net hazifai?? inaonekana bado haukumuelewa mwalimu wako mkuu........muulize tena!!! wengine tunafundisha vyuo vikuu humu!
 
Rukwa? Nina MBA kaangalie chuo cha 4 africa kwa ubora kwa MBA na cha kwanza Tanzania ndiko nilikosomea mimi....

kama umesoma cha 1 tanzania,u mean UDSM,utakuwa unawasingizia,KUNA WALIMU NA WAHTIMU WA UDSM HUMU,USIZUE MAMBO
 
Naomba nitoe angalizo.
Naona watu wanatolea mifano kwa kuitaja sana CIA. Kwa taharifa yenu Intelligence agency ambayo ni high efficiency na kiwango zaidi Duniani ni ile ya Pakistan, ISI.
Mkuu umesahau mosad!na shirika laupelelezi la Iran (IIA)
 
Una uhakika?? ISI wangejua long before CIA osama alipokua.., na what about suicide bombers in karachi..,

ISI wangejua operation ya kumuua osama kabla hata ya tukio lenyewe through intel comm interceptions...,

Be careful na sources za data zako..,


Moshi darini;
Kwa mawazo yangu huyo jamaa anayesema ISI wako juu duniani mimi nakubaliana naye kwa issue moja. Naona kama waliamua kumlinda Osama na hivyo no leakage ya information iliyotokea kwa mda mrefu ndiyo maana akawa hakamatiki. Otherwise wangekuiwa legelege, angekamatwa siku nyingi kabla ya siku hiyo. Mimi nakubaliana na huyu hoja yake. Unataka kuniambia ISI wao walikuwa hawajui kama Osama alikuwa ndani ya Pakistani? Walikuwa wanajua na wao ndiyo waliomlinda siku zote hizo nadhani. Jama kweli watakuwa wako juu!
 
cha kujiuliza ni kwamba mkurugenzi wa usalama wa taifa anachaguliwa na nani? kama ni Rais basi ujue huyo atakua kibaraka wa rais vyovyote vile maana yule ndio boss wake. Rais akitaka brief yoyote kuhusu hali ya usalama anapewa na huyo director so kama rais or vibaraka wake wakifanya kosa la jinai ni rahisi likazimwa na hao kwenye hiyo idara maana wamewekwa na hiyo hiyo serikali. Hata america or europe ukifuatilia katika history kumeshatokea situations ambazo wanafichiana madhambi yao hiyo ipo kila mahali
 
Nafikiri wewe mwenyewe una jibu mh, kwamba siasa zetu uchwara zimeingia mpaka sehemu nyeti, badala ya kulinda nchi na raia wao wanalinda kikundi cha watu na chama fulani. Hao hata wauze nchi hutasikia taarifa za kiintelijensia lkn wewe iba kuku utawasikia wamepata taarifa za kiintelijensia! Hapa Tz hakuna chombo cha usalama kisichotumiwa vibaya kwa maslahi ya mwanasiasa fulani. Si unakumbuka kina gen Shimbo? Akina Hosea, DCIA Manumba? tunahitaji kuwa na utawala wa sheria.

sisi ni vibaraka wakuu wa mataifa ya kiarabu na hatuwezi kujiimalisha ki uslama wa taifa kama ilivyo Ulaya na marekani na Israel. Kila mataifa ya kiarabu yakifanyizwa na USA, Israel au Ulaya magharibi, Utaona watanznaia wanasiasa wa kitanzania wanajibu matusi kwa niaba ya waarabu. Kwa nini malecelela aliyaota majeshi ya marekani eti ni ya uvamizi yalipoingia Iraq na hajawahi kuyaita majeshi ya Uganda ni ya kivamizi yalipoingia Congo? Kw anini watoa makala hawakukumtaka museveni akashitakiwe the hague kwa kuingiza majeshi yake Congo ila walitaka Bush ashitakiwe the hague kw akuingiza majeshi yake Afghaniustani? unaona jinsi tunavyotumiwa na waarabu kujichafulia jina letu ktk ulimwengu wa kidiplomasia?
 
Hatuwezi kuangalia chochote na zaidi tunaweza kufanya INTELIJENSIA ya maandamano ya wananchi na kuzuia uharibifu wa mali zao japo wanasema mali za umma.

Pia kuna uwezekano mkubwa kuwa tunachunguzana wenyewe ili kuzuia kujulikana kama unamiliki mali kihalali au la

Na lazima wanaojulikana kuwa wanajua wizi unavyofanywa na viongozi wauwawe maana wanahatarisha usalama wa viongozi kwa kivuli cha usalama wa nchi.

Hatuwezi kufanya uchunguzi wa nchi nyingine kama hapa kumchunguza mtu ili ateuliwe tu hatuwezi je ya nje tutaweza mfano Vijisenti baada muda mfupi wa kuteuliwa kwake.

Mafisadi wameshika uskani wa usalama na pia usalama wamebinywa na TAKUKURU inyojua yote maana CAG hajui zaidi uhasibu zaidi ya TAKUKURU na wao wanasema kama pesa imepotea au la!

Umeona wapi na katika nchi ipi duniani Usalama kuwa hauna makali kama hapa kwetu,nadhani usalama umeng'oka kama alivyong'oka mwalimu.

Ni lini siri isivuje? Ni lini siri za baraza zisivuje? Wapo mamluki katika usalama maana kazi sasa ni watoto wa vigogo, ndugu wa vigogo, waliokaribu na vigogo na waliokaribu na wanasiasa wafanyabiashara.

Ndo maana maamuzi magumu hatuwezi maana watakaojadili maamuzi magumu utayakuta nje kabla ya msemaji mkuu

Wapo wenye moyo katika kazi lakini ushauri wao hauzingatiwi je ya nje watasikilzwa kama ya ndani hawasikilizwi? Acha tuone yanayoendelea katika teuzi mbalimbali za wakubwa ni fulani mtoto wafulani,rafiki wa mtoto wake, shemeji yake, mkwe wake, nk

"TUIMARISHE USALAMA WA TAIFA, TUTENGANISHE KAZI ZIPI ZA TAKUKURU NA ZIPI TAKUKURU HAWARUHUSIWI KUZIFANYA SIO KILA KAZI TAKUKURU HATA IWE YA KIDAKTARI NA UHESHIMIWE UTARATIBU HUO NA USALAMA WA TAIFA UWE NDO KAULI YA MWISHO KWENYE USHAURI WA KITAIFA NA SIO INTELIJENSIA YA POLISI JUU YA MAANDAMANO NA NDOTO ZA ALINACHA ZA KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA WAKATI LISTI YA WATUHUMIWA ANAYO RAIS
 
kuna kitengo cha wachapakazi hasa kiko jeshini.., kitengo cha ujasusi ambacho hadi sasa kiko free from politics ni CMI (central military intelligence)..., lakini upande wa foreign assets ndo wazuri sana wako bize kukusanya taarifa hatarishi dhidi ya nchi yenu hiyo...,

Hawa wamegawanyika..., kuna wanaofanya kazi kufatilia mienendo na tabia za maofisa na askari ndani ya vikosi hata nje,

kuna wakusanya habari za ndani ya nchi zenye maslahi na jeshi, mfano kuna watu kazi yao ni kusoma magazeti daily, magazeti ya ndani na hata ya majirani au kuangalia tv, au kushinda kwenye mitandao kama humu, pia kuna ambao kazi yao ni kunasa mawasiliano ya jirani zenu...,

na kuna foreign assets.., wanaishi na kukaa nje...., kuna wanaotumwa for a specific mission na kuna wanaokaa tu huko kukusanya taarifa yoyote ambayo ina maslahi na usalama wa nchi.., na wapo ambao ni infiltrated kwny majeshi jirani na serikali za jirani

hawa ndo wamebaki kuwa pillar ya nchi from outside threats

Ila ile cream ilokua trained russia, israel, cuba ndo inastaafu..., wamebaki wale mnaowafundisha pale mikumi

Nimeipenda hii.
Heshima kwao makamanda.
To be honest, kama inawezekana niko tayari kufanya kazi na hawa watu.
 
Naomba nitoe angalizo.
Naona watu wanatolea mifano kwa kuitaja sana CIA. Kwa taharifa yenu Intelligence agency ambayo ni high efficiency na kiwango zaidi Duniani ni ile ya Pakistan, ISI.

Hizo ni data za wakoloni kupaka watu mafuta kwa mgongo wa chupa...osama/al qaeda wasingeichagua pakistan kama chaka salama...sema wanamafungamano/wafadhili na vikundi vya kigaidi...CIA ni zaidi..hata huu urongo takwimu unapikwa nao kwa kusudi lao tena maalumu...ndo hawa kila uchao wanatoa takwimu za uchumi wetu unapaa nk..wanacheza na akili zetu kila uchao..
 
Hakika hakumwelewa. Hata mimi ukiniletea references za google.com au wikipedia.com,nitakutimulia mbali.

bado hamjui wote...wikipedia lazima uweke reference!!! google?? inajisimamia yenyewe? jamani ebu jueni mambo yalivyo
 
Up-to-date (2012) docs have revealed that the Pakistan's ISI is currently the best intelligence agency in the world followed by CIA.
 
Lakini hawa jamaa mara nyingi huwa hawapendi kujadiliwa. Nakumbuka mh. MNyika alikuwa anahoji baadhi ya matumizi ya fedha yanayohusu kitengo hichi bungeni. Kaka moja alilalamika sana sana kusemwa hadharani idara yake hapo hapo bungeni. nadhani lilikuwa Bunge la sita.

Tukirudi kwenye mada, Usalama wetu wa taifa unatia shaka kidogo kutokana na mwendendo wa matukio yanayotokea hapa nchini. Kuna baadhi ya wachangiaji wamesema jukumu la usalama ni letu sote. Ni kweli ni letu sote lakini nadhani waliopewa jukumu la kuhamasisha hili watakuwa wamepwaya. Nakumbuka enzi hizo tunaajiriwa mara tu baada ya kumaliza shule tulikuwa tunapewa maelekezo maalumu ya namna ya kulinda usalama katika eneo la kazi na taifa kwa ujumla. Na yalikuwa mafunzo muhimu sana. Siku hizi sidhani kama kautaratibu haka kama bado kapo, na kama kapo bado kako' efficient' kulingana na mabadiliko ya kisayansi na tekinolojia?
 
kuna mchangiaji mmoja amelisifia shirika la upelelezi la Iran (IIA) Naomba kuuliza kwasasa nalo lipo nafasi gani duniani kiupelelezi
 
kama umesoma cha 1 tanzania,u mean UDSM,utakuwa unawasingizia,KUNA WALIMU NA WAHTIMU WA UDSM HUMU,USIZUE MAMBO

Mkuu Bajabiri,
Cha kwanza kwa Tanzania ni Eastern & Southern African Management Institute (ESAMI)
(The Most Popular Business Schools 2012 in Africa). UDSM ni cha pili kwa Tanzania na
cha 17 katika Afrika...
 
hapo kwanza tujue kuwa mtanzania yeyote yule mwenye akili timamo ni usalama wataifa.nasema hv kwa sabbu vko vtendo vingi vinafanyika vya kuihujumu nchi na vinasabbsha nchi iingie kwenye hasara kubwa sana. Vitendo hv kama wananchi wangejua haki yao ya kutoa taarfa nchi yetu ingekua mbali sana.

tatizo lilopo vyombo vyetu vya usalama vinashirikiana na hao wahalifu kwa 100%inakuwa ni vigumu kutoa taarifa
 
Jamani Usalama ni wetu waTZ huko Pakistani walimuua Osama naye aliibomoa Twin Tower
Mm nisiesoma. Hata huko Mikumi nikumbusheni hakuna Mfungwa (Uncle Tom)alitoroka Keko? Tena askari Magereza akalipwa yy na familia yake mbona yule mtoro yupo na kesi hakuna. Nani hamjui Balali? Usalama ni ww
 
Back
Top Bottom