Watanzania
JF-Expert Member
- Jul 7, 2009
- 727
- 42
Binadamu wenye ubinadamu tunasikitika sana na kumpa pole JK kwa kuanguka jukwaani akiwa kwenye kazi za chama. Tunamtakia afya njema rais. Hali hii imemtokea JK mara nyingi akiwa kwenye kazi za siasa. Tunaona uhusiano wa kazi anazofanya sasa za kisiasa na kuanguka kwake. Tunaona ni jambo la busara kwa JK kuacha siasa za jukwaani kabisa kwa vile afya na uzima ni muhimu zaidi kuliko madaraka au mali. Tunaomba JK aache siasa ili atunze afya yake. Akifanya hilo hana cha kupoteza bali ataitunza afya yake kwa manufaa yake, familia yake n.k. Hana cha kupoteza kwa vile atatunza heshima kwa kukubaliana na hali ya afya yake. Hana cha kupoteza kwa sababu atawaacha watanzania katika mikono salama ya urais wa Dr. Slaa. Na atakuwa ameacha historia ya pekee kwa kuacha demokrasia ichukue mkondo wake kwa kukubali chama mbadala cha Chadema kuongoza Tanzania.