Mzalendo Uchwara
JF-Expert Member
- Jan 26, 2020
- 3,721
- 11,717
Sio dhambi wala jinai kuwa na ambitions za kuusaka uongozi wa juu wa nchi, lakini wengi wanakuwa consumed na ndoto hizo, wako distracted, wanafanya siasa zaidi kuliko kazi waliyopewa, wanahangaika kukusanya fedha na kusuka mitandao yao. Watu hao sio wazuri kwako.
Moja ya mambo yaliyomfanya Hayati Magufuli kuwa waziri bora kipindi kile ni kwamba hakuwa anapoteza muda kufukuzia ndoto ya Urais. Alikuwa bize kutekeleza majukumu yake, umpende au umchukie ukweli ni kwamba he was reliable. Rais alikuwa anapumzika na kupumua akiwa na uhakika kuwa kwenye wizara yupo mtu ambaye focus yake 100% ni kuifanya kazi aliyopewa.
Pamoja na mabadiliko iliyoyafanya, lakini bado umeendelea kuwakumbatia hao watu ukiamini wanaushawishi mkubwa na watakusaidia kisiasa 2025. Lakini ukweli ni kwamba utendaji kazi wa hao watu ni wa hovyo kwakua akili yao haipo kwenye kazi waliyopewa.
Na lingine la muhimu zaidi ni kwamba hao watu watafanya juu chini kukwamisha mchakato wa katiba mpya, nani hataki ufalme, nguvu na utukufu wa kiti cha urais wa JMT kama zilivyo sasa??
Kama kweli unayo nia ya kusonga mbele na kutuachia katiba mpya, basi jitahidi uwe na watu kama akina Doto, Mbarawa na wengine wa aina hiyo. Wanaweza kuwa na mapungufu madogo madogo lakini akili zao zipo kazini.
Mzee Mwinyi, Ben Mkapa, JPM na hata wewe mwenyewe hamkuwahi kuusaka urais kama hao watu wanavyofanya. Mwalimu wao na kiongozi wa genge lao unamjua. Watakuharibia.