WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 956
Napata taabu kusema kama tumeridhika au tumekata tamaa kwa sababu sina hakika kama tunajitambua na tunajua tunalolitaka.
Shida yangu ni kuwa wale ambao angalau tuko tunapiga mswaki hatujaribu kamwe kuwastua wenzetu. Tunawaongezea blanketi na shuka waendelee kuuchapa usingizi. Kama tungewanyang'anya wakaguswa na baridi kidogo hiyo picha wa wakazi wa Bonde la Mpunga ingekuwa tofauti!
DC, Hebu fafanua zaidi.
Kwa hili suala la usafi/uchafu - kujali/kutokujali nadhani tuna matatizo .Nakumbuka kuna kipindi nilijaribu kuanzisha kampeni ( kama mtu binafsi) ya kusafisha mazingira ya eneo ninaloishi mimi -hivyo vikwazo unavyokumbana navyo usiombe!Lakini tulipelekeshana tu vizuri.
Katika maeneo mengi ya makazi kuna mchanganyiko wa watu wenye fikra tofauti - wapo wenye kujali na kufanya mazingira yao yawe safi - halafu wapo wale wasiojali kabisa na hawa ni wagumu sana kushughulika nao maana wanachojali wao ni mradi kumekucha.Na usipoangalia utaishia kutukanwa mpaka ushangae.Je usafi ni class issue?
Narudi tena kwa wenzetu wapanga miji. Miji/jiji letu lilivyopangwa inashangaza kidogo- kuna mchanganyiko maalum. Utakuta mixture of high,low.medium density plots.jE, NINI mantiki ya huu mchanganyiko? haieleweki kama eneo ni slam au ni affluent surbarb na ujengaji wa nyumba nao unashangaza pia.Tazama maeneo kama Mikocheni,Msasani na hata Mbezi Beach utaona hiyo hali.Inakuwa vigumu sana kuweka madhari nzuri kwa maana huo mchanganyiko wenyewe ni kero.Sijui tufanye nini.