Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,997
Mkazi wa Msasani Bonde la Mpunga akipita katika matofali kukwepa maji machafu yatiririka kutoka katika makazi ya watu.(Picha kwa hisani ya Mroki)
My Take:
Picha hii ukiangalia kwa haraka ni kama picha ya kawaida tu ya hali halisi ya maisha ya watu wetu. Lakini ukianza kuiangalia kwa vipande na kuweka focus ya kitu au theme moja moja utaona kuwa inabeba ujumbe mzito kweli.
a. Nyumba
b. Maji machafu
c. Mtu
d. Makazi
e. Umeme
f. Takataka
Kitu kimoja hata hivyo nilicho na mang'amuzi nayo ni kuwa usione mazingira hayo kwa nje, hizo nyumba kwa ndani zina umeme, TV n.k na wakazi wake wanatembea na viselula huku wakitinga pamba za nguvu kila siku wakienda kujobu au kuchakarika. Wakazi wake usishangae kuwaona kwenye matamasha mbalimbali wakiwa wanaburudika na moja moto moja baridi.
Hii picha ina ujumbe mzito sana.