Tumelamba Garasha

Jamaa anapenda sana kuimba bongo flava hata kwenye mambo yanayohitaji umakini! Umeme ni shida baada ya miaka 50.....hawa jamaa ni yak yak!

Rev, kwanza karibu back.
The list is impresive lakini nadhani tunapoteza muda kujadili hili. hao wenyewe kwanza inaonekana hawajui waliahidi nini maana juzijuzi hapa walisema kwua ndo wameunda timu ya kufuatilia na kuorodhesha ahadi zote zilizotolewa na JK wakati wa kampeni. naona umewasaidia kupunguza kazi yao.
Kama wangekuwa makini, nadhani wangekuwa wanajua ahadi zote mara tu baada ya kampeni kwisha na wala wasingehitaji kulipana posho kuanza kuzunguka kuorodhesha ahadi.
Si ajabu kuwa hiyo kazi ya kuorodhesha ahadi ikachukua miaka miwili, kuzichambua mwaka mmoja na kuandaa mkakati wa utekelezaji mwaka mwingine na hivyo kubakiwa na mwaka mmoja tu wa kuzitekeleza.
We are being atken for a ride
 
Masa... Karibu Arusha mkuu

Tumelamba garasha na bahati mbaya washabiki wanaona lile garasha nzuri simply kwasababu lina rangi ya kuvutia
 
Jamaa anapenda sana kuimba bongo flava hata kwenye mambo yanayohitaji umakini! Umeme ni shida baada ya miaka 50.....hawa jamaa ni yak yak!

Hapa tusipogeuka Tunisia/Misri tutaendelea kulia na kusubiri hizo ahadi hewa mpaka ile kwetu mazima.
 
Hivi kwanini jamaa anashindwa kuwajibisha watu hata kama ni kwa utani tu?
 
Masa... Karibu Arusha mkuu

Tumelamba garasha na bahati mbaya washabiki wanaona lile garasha nzuri simply kwasababu lina rangi ya kuvutia

Mazee nashukuru Arusha ni mji wa mapinduzi! Natamani Mtwara na Lindi wawe kama Arusha wasikalie Korosho tu. Mwaka jana nilikuwa Naliendele jamaa hata vyoo hawana ila wana kadi za CCM na mobile (simu za mikononi) wenyewe anaita simu za voda
 
watanzania tunatakiwa tufanye kitu kionekane
tukiongea tutekeleze kwa vitendo!
tukigoma tugome kweli mpaka impact ionekane !
tukiandamana tuandamane kweli!
tukisusia jambo tuungane mkono!
One Day we will see the end of this odd regimes
 
Mazee nashukuru Arusha ni mji wa mapinduzi! Natamani Mtwara na Lindi wawe kama Arusha wasikalie Korosho tu. Mwaka jana nilikuwa Naliendele jamaa hata vyoo hawana ila wana kadi za CCM na mobile (simu za mikononi) wenyewe anaita simu za voda

Rev Masa,

Huko Lindi na Mtwara sio kutamaani tu, inabidi jitihada endelevu zitumike kuwahamasisha ndugu zetu vinginevyo kutaendelea kuwa hivyo hivyo hata baada ya miaka hamsini ijayo.
 
Mazee nashukuru Arusha ni mji wa mapinduzi! Natamani Mtwara na Lindi wawe kama Arusha wasikalie Korosho tu. Mwaka jana nilikuwa Naliendele jamaa hata vyoo hawana ila wana kadi za CCM na mobile (simu za mikononi) wenyewe anaita simu za voda

kule nadhani ni kautaratibu kao,pale Mikindani(mji mdogo wa zamani wa asilia Mtwara) wao wanapakualia mzigo baharini tu
 
Wakuu kama nyinyi ni hazina kwenye hii JF. Senksi kwa kutukumbusha hizi ahadi hewa za bosi Jakaya. Da! Sijui hii miyeyusho itaisha lini. Kesho naanza Novena.
 
siku moja nilkuwa naagalia kipindi cha tanesco kwenye TV, kiongozi wa Tanesco akasema "mipango ya tanesco ni kuwapatia umeme watanzania 100,000 kila mwaka.
Nilipofikiria population increase ya 3% kwa mwaka nikaona haitatokea hata siku moja ailimia 10 ya waTZ wapate umeme. The two graphs, populatiopn increase and electric supply will never meet.
Hali hiyo ni sawa na ahadi za JK na utekelezaji wake.
Mkuu kuna ahadi nyingine umesahau: Masista wa parokia fulani huko Karagwe aliwaahidi trekta mpya ndani ya mwezi mmoja, sasa ni miezi zaidi ya minne hakuna dalili ya trekta!
 
Tuna matatizo yanayofanana kama watanzania. Ugumu wa maisha ni kwa kila mtu regardless ya itikadi zake kichama hata kidini. Ni miaka 50 hadi leo tunakosa maji safi ya kunywa wakati fisadis wanakunywa maji sipesheli na matibabu majuu. Misri huyu Husni Mubarak alishinda kwa 95% leo watu wako mtaani hawataki ujinga. Zaidi ya watu Mil 1 wameandamana polisi wameungana nao maana huwezi uwa watu wote hao

_51047570_011166519-1.jpg

welcoooooooooome back, welcome back, welcome back, welcooome back lol.
Nimeipenda style yako ya kurudi Masa.
 
Tuna matatizo yanayofanana kama watanzania. Ugumu wa maisha ni kwa kila mtu regardless ya itikadi zake kichama hata kidini. Ni miaka 50 hadi leo tunakosa maji safi ya kunywa wakati fisadis wanakunywa maji sipesheli na matibabu majuu. Misri huyu Husni Mubarak alishinda kwa 95% leo watu wako mtaani hawataki ujinga. Zaidi ya watu Mil 1 wameandamana polisi wameungana nao maana huwezi uwa watu wote hao

_51047570_011166519-1.jpg

Mkuu tatizo kubwa hapa kwetu ni kuweka mbele ujinga kuliko maslahi ya watanzania wote hususan tabaka la chini.
Ukiitisha mgomo au maandamano kwa ajili ya kudai vitu vya msingi kwa maslahi yetu, kwa mfano sasahivi bei ya bidhaa madukani inapaa(sio kupanda). Usitaje unga wa sembe, mchele, sukari, mafuta ya kula, petroli, dizeli, mafuta ya taa, n.k watu wataanza kukuangalia usoni kwanza na kuulizana wewe chama gani badala ya kuzungumzia suala unalopendekeza lifanyike.
Kuna watu wamenyweshwa rangi za bendera za vyama vyao, pamoja na kwamba wengine ni wasomi waliobobea lakini akili zao zimeharibiwa na itikadi za vyama vya siasa.
Wacha tuendelee kupigika tu, ikifika wakati muafaka wala watu hawataambiwa ku Ben Ali, wenyewe watajikuta wamejazana mnazi mmoja na magogoni.
 
Ujinga ni hazina kubwa ya CCM! Kuwa mjinga hakuhusiani umekaa darasani miaka mingapi! Hata ukiwa na PhD za heshima 100 utaendelea kuwa mjinga tu
 
Tuna matatizo yanayofanana kama watanzania. Ugumu wa maisha ni kwa kila mtu regardless ya itikadi zake kichama hata kidini. Ni miaka 50 hadi leo tunakosa maji safi ya kunywa wakati fisadis wanakunywa maji sipesheli na matibabu majuu. Misri huyu Husni Mubarak alishinda kwa 95% leo watu wako mtaani hawataki ujinga. Zaidi ya watu Mil 1 wameandamana polisi wameungana nao maana huwezi uwa watu wote hao
[/CENTER]

Ungelitambua haya wakati ule ulipokuwa unabwabwaja matusi na kebehi kwa hao uliotofautiana na kidini na kiitikadi ni wazi leo hii tungekuwa tunasema mengine. Waswahili tunasema, usidharau mkunga, uzazi ungalipo....Jifungue mwenyewe sasa...
 
Unaweza elezea kwa mapana kidogo! Sijakufahamu kabisa na usitake nipeleka nisiko kujua.
 
yani mkwere hizo ahadi hatekelezi hata moja labda hiyo ya bajaji kwa mama wajawazito...
 
Tuna matatizo yanayofanana kama watanzania. Ugumu wa maisha ni kwa kila mtu regardless ya itikadi zake kichama hata kidini. Ni miaka 50 hadi leo tunakosa maji safi ya kunywa wakati fisadis wanakunywa maji sipesheli na matibabu majuu. Misri huyu Husni Mubarak alishinda kwa 95% leo watu wako mtaani hawataki ujinga. Zaidi ya watu Mil 1 wameandamana polisi wameungana nao maana huwezi uwa watu wote hao

_51047570_011166519-1.jpg

Karibu mkuu Masa..huyu dikteta Hosni alikuwa anajitangazia ushindi wa zaidi ya 99%
 
sasa ilikuwaje akasema ahadi ya Mh. Slaa kusomesha bure wanafunzi haiwezekani?
 
Back
Top Bottom