Tumelamba Garasha

Rev Masa,

Karibu tena home. Sie wenzio tumeshazoea mwendo wa yebo yebo. Tumemwachia Nkwere afanye atakavyo ati!!

Tunisia na Misri ni mbali sana na Tz. Pia nguvu za Shekh mashuhuri A & C Africa (Y.H) zinafanyakazi ipasavyo!

No one is worried na kelele za mlangoni...mwenye nyumba anauchapa usingizi kama kawa!
 
Rev

Haujatutendea haki sisi wakazi wa Kyela kwa kutokumbushia ahadi yetu kwa "Maulana"JK;mbali na kutuhaidi meli kubwa ya kisasa ktk ziwa nyasa mwaka jana lkn mwaka 2005 alituhaidi kutujengea barabara ya kiwango cha lami toka Njia panda Kyela-Ipinda hadi Matema Beach!

Miaka inazidi kukimbia lkn hatuoni sio tu karandika kuja kuanza kusafisha bali hatujawahi kuwaona bado hata hao waandisi wanaotakiwa kuja kuanza kufanya uhakiki wa kitaalam!

Tafadhali nikumbushieni JK ahadi yake hii kongwe aliyoitoa Kyela kwenye uwanja wa mpira wa Mwakangale yenye miaka 6 sasa bila kuona hata dalili za kutimilizwa;atekeleze hii kwanza ya mwaka 2005 ndipo aanze hii mpya ya kutununulia meli aliyoitoa mwaka jana tu!
 
Rev, kwanza karibu back.
The list is impresive lakini nadhani tunapoteza muda kujadili hili. hao wenyewe kwanza inaonekana hawajui waliahidi nini maana juzijuzi hapa walisema kwua ndo wameunda timu ya kufuatilia na kuorodhesha ahadi zote zilizotolewa na JK wakati wa kampeni. naona umewasaidia kupunguza kazi yao.
Kama wangekuwa makini, nadhani wangekuwa wanajua ahadi zote mara tu baada ya kampeni kwisha na wala wasingehitaji kulipana posho kuanza kuzunguka kuorodhesha ahadi.
Si ajabu kuwa hiyo kazi ya kuorodhesha ahadi ikachukua miaka miwili, kuzichambua mwaka mmoja na kuandaa mkakati wa utekelezaji mwaka mwingine na hivyo kubakiwa na mwaka mmoja tu wa kuzitekeleza.
We are being atken for a ride

Kwani mkwere alikua hana campaign manager .... au ndo kila kitu kwake hadithi kwa wajukuu.

Unajua tukisubiri ya Tunisia na Misri yanaweza yasitokee any time soon and it will be too little, too late. Wenzetu majority wana arabic nature ya kujitoa muhanga for the good cause.

I think we should unfold more cards on the table...............
 
Tatizo hatukuuliza atazigharimiaje...

Kulikuwa na vibwagizo vingi sana kusindikiza hizo ahadi kama hivi;
-Ujenzi wa barabara ya Musoma-Arusha kupitia serengeti, upembuzi yakinifu umekamilika sasa tunatafuta mkandarasi wa kutekeleza ujenzi wa barabara,
-Mradi wa maji toka ziwa victoria kwenda tabora, fedha zimeshapatikana toka benki ya dunia,
-Ununuzi wa meli yenye uwezo wa kubeba tani 4000 ziwa victoria, tumepata mkopo wa riba nafuu toka benki ya maendeleo ya africa mashariki,
-Ununuzi wa bajaji 400 kwa ajili ya kubebea akina mama wajawazito, serikali imetenga katika bajeti yake kiasi cha shilingi bilioni mbili kwa ajili ya kazi hiyo,
-Ujenzi wa njia mpya ya umeme toka makambako hadi songea na kuunganisha makao makuu yote ya wilaya, tanesco imepata mkopo wa muda mrefu na riba nafuu toka serikali ya japan,
-Na bla bla nyingine nyingi za namna hiyo, unadhani watanzania hawa tulionao wangeweza kuhoji hiyo mifeza iliyokuwa inatajwa na wakati huo huo kila idara na shirika la serikali katika sekta husika walikuwa wanawazuga wananchi kwamba kila mradi uliotajwa na mkulu ni wa kweli na maandalizi ya utekelezaji ndo yamepamba moto. Tanesco mbona hawakuthubutu kukata umeme kabla ya uchaguzi, sasa kiko wapi? gizo totoro na hatujui tutatoka lini humo gizani!
 
Hi dharau kubwa sana! Tunajua cha kufanya Ben Ali nguvu ya Umma ilimwangukia na sasa upepo unaelekea kwa Hussein Mubarak! Natamani na sisi tumtoe mkwere na dharau zake hizi. Sidhani akama anajua kuwa tunajua anatudharau

Karibu sana mpwa.

CCM wanatulazimisha tufanye kinacho tokea Misri na Tunisia wanashindwa kusoma alama za nyakati.
 
Rev

Haujatutendea haki sisi wakazi wa Kyela kwa kutokumbushia ahadi yetu kwa "Maulana"JK;mbali na kutuhaidi meli kubwa ya kisasa ktk ziwa nyasa mwaka jana lkn mwaka 2005 alituhaidi kutujengea barabara ya kiwango cha lami toka Njia panda Kyela-Ipinda hadi Matema Beach!

Miaka inazidi kukimbia lkn hatuoni sio tu karandika kuja kuanza kusafisha bali hatujawahi kuwaona bado hata hao waandisi wanaotakiwa kuja kuanza kufanya uhakiki wa kitaalam!

Tafadhali nikumbushieni JK ahadi yake hii kongwe aliyoitoa Kyela kwenye uwanja wa mpira wa Mwakangale yenye miaka 6 sasa bila kuona hata dalili za kutimilizwa;atekeleze hii kwanza ya mwaka 2005 ndipo aanze hii mpya ya kutununulia meli aliyoitoa mwaka jana tu!

Mkuu umenikumbusha kitu muhimu sana! Ningeweza pata kumbu kumbu za ahadi za 2005 ningeweka na hizi za 2010 tuone tunamagarasha mangapi! Kweli huyu jamaa sura halisi tunaanza kuifahamu. Nakumbuka mama Mongella aliwahi kusema Kikwete ni mtu wa mizaha na hafai kuwa raisi sababu yeye kila kitu ni utani tu. Dr William Shija yeye alisema kama Kikwete atakuwa raisi wa Tanzania basi tusehesabu maumivu makali. Dr Shija hakugombea hata ubunge kule Sengerema ingawa alikuwa bado anakubalika.
 
kwa hakika kwa namna ulivyozidokumenti, wewe lazima ni mmoja wa mliokuwa kwenye msafara wake. Huwa hamumshauri au hashauriki?
 
kwa hakika kwa namna ulivyozidokumenti, wewe lazima ni mmoja wa mliokuwa kwenye msafara wake. Huwa hamumshauri au hashauriki?

Hahahahaah nadhani hashauriki! Siku hizi wanakuja na kamsemo kuna ahadi za CCM na ahadi za Mgombea...naona wanataka muachia zigo Mkwere wa watu.
 
Well, CCM imeamua kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CHADEMA. Tumekuwa wazi - Tumeanza na elimu ya bure kuanzia 2012 ( Je, Ilikuwepo kwenye ilani yetu?), Tumefuatia na Katiba Mpya..... Sasa hizi ahadi zako Rev. Masalia nenda kamuulize Dr. Slaa ndo azitekeleze. Sisi tulichaguliwa na wananchi baada ya kusaidiwa sana na Dr. Slaa kunadi sera tunazozitekeleza sasa hivyo hizo ahadi siyo zetu. Usiponielewa muulize Jaji Makame atakueleza ukweli wa ilani inayopaswa kutekelezwa!!!

Kidumu chama cha Majambazi!!!! Zidumu fikra sahihi za Mh. Dk.Dk. Dk. Mkuu sanaaaa, Mh. Dkt Kikwete!!
 
Tatizo hatukuuliza atazigharimiaje...

Mkuu unadhani option ya kuuliza maswali ilikuwepo? tuliokwenda tumejiandaa kuuliza maswali tulikuta kampeni ni kama fiesta live concert, tukaimbiwa bongo fleva masaa matatu, jamaa alipokuja alipanda jukwaani akahutubia dk 5-7 na kuahidi ahadi kibao zisizotekelezeka, by the time una digest utekelezaji wa ahadi hizo ukiwa umepigwa butwaa, unaona bongo flava zinaanza tena jamaa kesha timua.

it was too fast kama uporaji wa simu vile. shukuru Mungu you did not see.
 
Mkuu unadhani option ya kuuliza maswali ilikuwepo? tuliokwenda tumejiandaa kuuliza maswali tulikuta kampeni ni kama fiesta live concert, tukaimbiwa bongo fleva masaa matatu, jamaa alipokuja alipanda jukwaani akahutubia dk 5-7 na kuahidi ahadi kibao zisizotekelezeka, by the time una digest utekelezaji wa ahadi hizo ukiwa umepigwa butwaa, unaona bongo flava zinaanza tena jamaa kesha timua.

it was too fast kama uporaji wa simu vile. shukuru Mungu you did not see.

Jamaa msanii sana huyu! Alijua kabisa hana kipya na hawezi jenga hoja akakimbia midahalo
 
Tuna matatizo yanayofanana kama watanzania. Ugumu wa maisha ni kwa kila mtu regardless ya itikadi zake kichama hata kidini. Ni miaka 50 hadi leo tunakosa maji safi ya kunywa wakati fisadis wanakunywa maji sipesheli na matibabu majuu. Misri huyu Husni Mubarak alishinda kwa 95% leo watu wako mtaani hawataki ujinga. Zaidi ya watu Mil 1 wameandamana polisi wameungana nao maana huwezi uwa watu wote hao

_51047570_011166519-1.jpg


Mchungaji habari za siku nyingi? Ukweli ni kwamba tumelamba gharasha mara mbili, mwaka 2005 na mwaka jana!! Hayo ya Tunisia na Misri nadhani siku moja wakifanya mchezo yatakuja tokea kwetu na jamaa watakosa kwa kukimbilia kwani Msoga hapatatosha!!
 
Mchungaji habari za siku nyingi? Ukweli ni kwamba tumelamba gharasha mara mbili, mwaka 2005 na mwaka jana!! Hayo ya Tunisia na Misri nadhani siku moja wakifanya mchezo yatakuja tokea kwetu na jamaa watakosa kwa kukimbilia kwani Msoga hapatatosha!!
Lakini tusijilaumu sana. Nadhani wananchi wa Tanzania walipeleka ujumbe wazi kuwa Mkwere ni garasha, lakini mfumo mbovu tulio nao pamoja na tume isiyo huru ya uchaguzi vikamrudisha Mkwere magogoni. Tusahihishe ubovu uliomo kwenye mfumo ili tusimpate tena mtu wa kaliba ya Mkwere kutudanganya.
 
Lakini tusijilaumu sana. Nadhani wananchi wa Tanzania walipeleka ujumbe wazi kuwa Mkwere ni garasha, lakini mfumo mbovu tulio nao pamoja na tume isiyo huru ya uchaguzi vikamrudisha Mkwere magogoni. Tusahihishe ubovu uliomo kwenye mfumo ili tusimpate tena mtu wa kaliba ya Mkwere kutudanganya.

Nikifikiria ni miaka mingine minne ya huyu bwana nachoka kabisa!
 
Hahahahaah nadhani hashauriki! Siku hizi wanakuja na kamsemo kuna ahadi za CCM na ahadi za Mgombea...naona wanataka muachia zigo Mkwere wa watu.

Wanataka kumuacha zigo lote mkwere kwasababu wakina Makamba walikasilika kwa fedha zote za kampeni kuthibitiwa na familia badala ya chama!! Kikwete kumuacha January kwenye baraza la mawaziri pia kumemkwaza sana father X-Mas.[ Makamba]
 
tuumpe muda atazitekeleza tu :)
Kwa wale wacheza karata wanajua maana ya kulamba dume kunavyoweza kuathiri mchezo mzima na kupelekea ushindi. Ila Ukilamba magarasha lazima upate maumivu ya kupoteza mchezo mzima wa karata hata kama utakuwa na jockeri moja na magarasha matupu. Nimeanzia mbali nikijaribu kuangalia ahadi na utekelezaji wa kile alichokuwa akikisimamamia Mh Mwenyekiti wa CCM wakati wa uchaguzi uliopita. Ninapata wasi wasi na IQ yake kwa kile alichokuwa akikisema, Nimeongezea ahadi ya 70 ambayo iko wazi lazima ataitekeleza tena kwa mbwe mbwe.

1.Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
2.Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
3.Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
4.Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
5.Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
6.Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
7.Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
8.Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
9.Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
10.Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
11.Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
12.Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
13.Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
14.Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
15.Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
16.Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
17.Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
18.Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
19.Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum
20.chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
21.Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
22.Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
23.Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
24.Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
25.Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
26.Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
27.Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
28.Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
29.Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
30.Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na
31.kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
32.Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
33.Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
34.Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
35.Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
36.Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
37.Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa -Musoma
38.Kulinda haki za walemavu - Makete
39.Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
40.Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
41.Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
42.Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
43.Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
44.Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
45.Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
46.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
47.Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
48.Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
49.Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
50.Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
51.Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
52.Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
53.Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
54.Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
55.Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
56.Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
57.Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi - Ifunda
58.Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
59.Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
60.Kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii – Kibandamaiti Mjini Zanzibar
61.Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa – Kibandamaiti mjini Zanzibar
62.Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
63.Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
64.Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
65.Kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
66.Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
67.Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
68.Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
69.Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
70. Kufuata utawala wa kisheria wa kutii mamlaka za kimataifa hata kama mchakato wa DOWANS umejaa utapeli, lazima tuwalipe ili Rostam asifanye nchi isitawalike.


Sisiti kukuona wewe Mkwere ni kama garasha kwa hizi ahadi zako.
 
Back
Top Bottom