Tumefundishwa kupenda chama badala ya nchi

Mzalendo Mkuu

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
735
191
Ndugu, moja ya matatizo makubwa ya Watanzania ni pamoja na kukosa uzalendo na moyo wa kupigania nchi yetu Tanzania. Hili tatizo lipo kwa wananchi wa chini pia na viongozi wa juu katika serikali.

Jambo ninaloliona wazi hapa ni kuwa Watanzania tumefundishwa kupenda Chama badala ya kupenda nchi. Ndiyo maana mpaka leo wakubwa wanafanya kila njia kulinda vyama vyao lakini hawana juhudi kubwa sana kwenye kulinda nchi yao Tanzania.

Tubadirike, tubadirishe mwelekeo wetu.
 
Ni kweli ndugu yangu.

Miongo si mingi ilopita, TANU/CCM walikuwa wanafundisha watu kukipenda chama, kukufia chama nk. Ndio maana WaTz wengi hawajui Katiba ya Tz lakini baadhi (wengi) wanajua ya CCM. Ni udhaifu mkubwa wa CCM na siasa zake za kikomunist.

Leo tunayo kazi zaidi ya kuwa-indoctrinate masses kisha tu-instill utaifa.
 
Mkuu,
Huo ni urithi mmoja aliotuachia mwalimu. Si unakumbuka usemi wa chama kushika hatamu?
Ni katika mazingaombwe na kiini macho cha siasa za TZ.

Hata hivyo, 1992 baada ya kuingia katika mfumo wa vyama vingi tena, hali hii ilipasa kuondoka. hakuna juhudi maalum ambayo imechukuliwa kuwaelimisha wananchi kuwa sasa ni serikali ndio inayoshika hatamu, sio chama tena.

Kwa hiyo, wakati tunawacheka Wazenj, tunawabeza kwa hatua yao ya maridhiano, lakini wanaonekana sasa wanaacha siasa za kupenda vyama na badala yake wanapenda utaifa wao, nchi yao...sisi tunasema wamefunga ndoa. Wametuacha nyuma kwa hili.

Kwa hiyo, umetoa mada nzuri kutukumbusha kuwa nchi ni zaidi ya chama, utaifa ni zaidi ya chama na uzalendo ni kuwa na uchungu na nchi yako.
Hapa pia ndio kuna umuhimu wa katiba ya taifa na sio hii ya kulinda chama kimoja.

Hii haitofuta haki ya mtu kupenda chama akitakacho, lakini maslahi ya Taifa kwanza!
 
Back
Top Bottom