Mbunge Abdulhafar: CCM ni wazoefu wa kupokea matokeo ya kushinda na kushindwa, upinzani wafundishwe

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
Mbunge Abdulhafar Juma akichangia kwenye miswada ya sheria uchaguzi ametoa pendekezo la kuongeza kipengele cha kutoa elimu namna ya kupokea matokeo.

Akisema, "Kushindwa kwa baadhi ya viongozi katika uchaguzi ndio kunaleta kitahalani katika taifa. Kumbe labda tu kwasababu hawana elimu.

"Nadhani kiwekwe kabisa kipengele katika mswada huu, moja ya majukumu ya tume ni kuwafunza wanasiasa kupokea matokeo. Wakishindwa wajue huyu ameshindwa.

"Mimi Chama changu Cha Mapinduzi ni wazoefu wakubwa wa kupokea matokeo ya kushinda na kushindwa. Nadhani sisi ndani ya chama chetu tumefundishwa sana, pale tunaposhindwa tunahimili, tunasubiri miaka mitano tunaendelea.

"Nina wasiwasi na vyama vingine vya upinzani kama kwao wanapeana elimu ya kupokea matokeo ya uchaguzi, Sasa nataka nione tume ya uchaguzi ina wajibu wa kisheria wa kuwafundisha kuwa ukishindwa kubali, tulia, unga mkono tujenge taifa letu."

 
nadhani hajui tatzo , tatzo ni serekali iliomadarakani kutumia dola kama chombo chao ili kukimbia na masanduku ya kura.

pia PAWEPO NA NENO TUME HURU YA UCHAGUZI,

KIONGOZI WAKE MKUU ASITEULIWE MAMLAKA (serekali)

wajumbe wawepo toka VYAMA VYA SIASA kwa mujibu wa usajiri wa vyama
 

VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WAPEWE ELIMU YA KUPOKEA MATOKEO HATA BAADA YA KUSHINDWA CHAGUZI ILI TUENDELEE KUJENGA NCHI

"Mswada wa Tume ya Uchaguzi unaonesha dhamira njema ya kuendelea kujenga uwazi na kuimarisha Demokrasia ambayo imekuwa ni desturi ya Chama Cha Mapinduzi kilicho madarakani kutoa elimu kwa nchi nyingine Barani Afrika juu ya namna bora ya kutekeleza Demokrasia" - Mhe. Abdulhafar Idrissa Juma, Mbunge wa Jimbo la Mtoni

"Mapendekezo ya Maboresho ya Mswada wa Tume ya Uchaguzi yemeendelea kulinda hadhi ya Muungano. Mswada umesema wazi kuwa tutakuwa na Mwenyekiti wa Tume kutoka upande mmoja wa Muungano na Makamu Mwenyekiti atatokea upande mwingine wa Muungano pamoja na wajumbe wengine" - Mhe. Abdulhafar Idrissa Juma, Mbunge wa Jimbo la Mtoni

"Naomba tuboreshe katika Ibara (18), Sekretarieti ya Tume ya Uchaguzi. Muundo wa Mwenyekiti wa Tume na Wajumbe wake umekaa katika taswira ya Kimuungano. Serikali iweze kuona namna tunavyotengeneza Naibu Mkurugenzi Mkuu atakayeshughulikia masuala ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi wa Muungano kwa upande wa Zanzibar" - Mhe. Abdulhafar Idrissa Juma, Mbunge wa Jimbo la Mtoni

"Katika Maboresho ya Mswada wa sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi iwepo nafasi ya Naibu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambaye atafanya shughuli zake Zanzibar atakayesimamia masuala ya kimuungano katika uchaguzi na kuyawasilisha kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi" - Mhe. Abdulhafar Idrissa Juma, Mbunge wa Jimbo la Mtoni

"Ibara (11) imeeleza majukumu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Natamani liongezwe moja, Kutoa elimu ya kupokea matokeo kwa viongozi wa vyama vya Siasa. Viongozi wa vyama vya siasa hawana elimu ya kupokea matokeo. Tume ina wajibu wa kutoa elimu kwa wapiga kura" - Mhe. Abdulhafar Idrissa Juma, Mbunge wa Jimbo la Mtoni

"Katika Mswada wa sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi uwepo utaratibu wa siku Maalum (Healing Day) kama ilivyo Zimbabwe 🇿🇼. Kampeni zinakwisha leo, kesho hapana kabisa Kampeni, wananchi keshokutwa wanakwenda kupiga kura. Hii itasaidia kushusha joto la Siasa na kuwapa nafasi wananchi namna bora ya kufanya maamuzi baada ya kusikia kauli za wanasiasa" - Mhe. Abdulhafar Idrissa Juma, Mbunge wa Jimbo la Mtoni

"Mwaka 1992 CCM iliyokuwa madarakani ndiyo iliruhusu uwepo wa Vyama vingi vya Siasa. CCM ndiyo ilisababisha uwepo wa wabunge wa upinzani Bungeni. CCM hii hii ndiyo imeielekeza Serikali kuleta Mswada wa mabadiliko ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi" - Mhe. Abdulhafar Idrissa Juma, Mbunge wa Jimbo la Mtoni

"Ni lazima masuala ya kijinsia yawe katika makosa ya kiuchaguzi. Kila dharirisho la kijinsia wakati wa Uchaguzi dhamira yake ni kumuondolea kura mgombea. Wanawake wanadharirishwa sana wakati wa Uchaguzi. Rushwa, hongo na udharirishaji wa kijinsia yawe ni makosa ya kiuchaguzi" - Mhe. Abdulhafar Idrissa Juma, Mbunge wa Jimbo la Mtoni
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2024-01-31 at 17.51.35.mp4
    18.3 MB
  • ccm-picqawser.jpg
    ccm-picqawser.jpg
    103 KB · Views: 1
  • maxresdefaultqwserd.jpg
    maxresdefaultqwserd.jpg
    98.4 KB · Views: 1
Back
Top Bottom