Boran Jakutay
Senior Member
- Apr 8, 2023
- 110
- 255
Habari zenu, kwanza nianze kwa kuwapa hongera wale wote walio kwenye mfungo wa KWARESMA na RAMADHANI, MUNGU WA MBINGUNI awaongoze salama hadi mwisho.
Leo nimekuja mbele yenu nataka ushauri, nifanye nini au tufanye nini sisi wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers inayomilikiwa na Mbunge wa Buchosa, ERIC SHIGONGO ili tupate haki yetu?
Stori nzima ipo hivi; Februari 12, 2024, Meneja Mkuu wa Global Publishers (Abdallah Mrisho) aliwapa taarifa wahariri wa magazeti ya michezo ya CHAMPIONI na SPOTI XTRA kwamba ofisi imesitisha kuchapisha magazeti kutokana na hasara inayopatikana.
Baada ya hapo, hakukuwa na kauli rasmi ya uongozi kwenda kwa wafanyakazi wote kwa maana ya waandishi waliokuwa wakiandikia magazeti hayo na hata wasanifu kurasa hawakupewa tamko rasmi nini kitafuatia baada ya hapo.
Cha kushangaza, baada ya siku mbili kutoka Februari 12 hadi 14, ikaundwa timu ya watu sita (6) yenye wahariri wawili (2), waandishi wawili (2) na wasanifu kurasa wawili (2) ili kuendelea na kazi ya kuyaandaa magazeti mawili yanayotoka mtandaoni kwa wiki (CHAMPIONI IJUMAA na CHAMPIONI JUMATATU).
Kumbuka wale wahariri waliopewa taarifa ya kusitishwa uchapishaji magazeti, walikuja kwa waandishi na wasanifu kurasa kufikisha taarifa hizo, sisi tulitarajia baada ya hapo uongozi utatoa tamko rasmi lakini imekuwa kimya mpaka leo hii.
Hata hivyo, taarifa zilieleza baada ya kusitishwa uchapishaji magazeti, zitatolewa barua kwa wafanyakazi ili kuonesha mikataba imesitishwa na kila mmoja afahamu stahiki zake na atazipataje, ukizingatia wapo waliokuwa kazini kwa zaidi ya miaka nane (8), lakini hakuna barua yoyote iliyotoka, hivyo ni kama tumeachishwa kazi KIHUNI.
Kila mara tunapoomba tukutane na Mkurugenzi Mkuu (Eric Shigongo) ambaye ni MBUNGE WA BUCHOSA ili tuzungumze naye, kumekuwa na ugumu kwani naye anawarushia mpira viongozi wa chini ndio wasikilize vilio vyetu.
Sisi tumekuwa tukitaka kuonana na SHIGONGO kwa sababu viongozi wa chini yake tumekaa nao vikao vingi, lakini majibu yao hayaridhishi, wakati mwingine hawana kabisa majibu ya maswali yetu, wanatoa ahadi ambazo hazitimizwi, hivyo basi tunapofanya juhudi ya kutaka kuonana na mmiliki wa kampuni, anatukwepa.
Tunajiuliza, Mbunge ambaye ana jukumu la kuongoza wananchi, anawakwepaje wananchi wake wa ofisini, je huko jimboni kwake matatizo yakitokea anayatatuaje au pia anayakimbia?
Ushauri wenu ni muhimu sana, tufanye nini ili tupate haki yetu kwa sababu siku zinazidi kwenda, hatujui hatma yetu na tupo nyumbani tangu tulivyositishiwa ajira zetu KIHUNI, tunaona tunakwenda kudhulumiwa.
Tunaidai ofisi hela nyingi sana ikiwemo mishahara ya takribani miezi 11, tumefanya kazi kuanzia Aprili 2023 hadi Februari 2024 bila ya kulipwa mshahara. Tunaishije na tuna familia zinatutegemea.