DOKEZO Mkandarasi wa SGR ametoa majina wanaopunguzwa kazi, Serikali isaidie tupate haki zetu tunaopunguzwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Leo tarehe 21 mwezi wa 11 kumefanyika Kikao cha Wafanyakazi wanaojenga Mradi wa SGR na Maafisa Rasilimali Watu wa Kampuni ya Yapi Merkezi ambaye ni Mkandarasi Mkuu wa Mradi huo, hakuna muafaka ambao tumeufikiwa kati yetu.

Kikubwa ambacho tumezungumza ni kuwa Wao wametoa orodha ya majina ya Wafanyakazi ambao wanapunguzwa kazi lakini kwa masharti yapi hapo ndipo muafaka haujapatikana.

Wao wanadai Mkandarari Mkuu ameishiwa na ana hali ngumu kiuchumi.

Serikali iingilie kuangalia haki za Wafanyakazi ambao wanapunguzwa ili haki zao zipatikane.
2d5083eb-5cfa-419d-b640-9a4c8d48e8c3.jpeg

a9a1fe8e-9529-4350-b2c4-1766730cfa7d.jpeg

d5c6c99a-7fca-4d33-b9d5-890dca331923.jpeg

3935ac26-7c4d-410f-97a2-22bbb0077b57.jpeg
 
Lakini kiuhalisia muajiri akisema anapunguza Staff wake, hasa kazi za mikataba kama hizo za ujenzi, unaweza kweli kupingana naye? Labda issue iwe ni kulipa watu mafao/stahiki zao.
 
YEPI ana hali ngumu sanaa....maana TRC hawajawalipa muda mrefu sanaa.....na wanashindwa kusema ukweli ...Saa 100 ana hali ngumu sanaa.....miradi inadodaa
Huu ni uthibitisho Kwamba huu mradi unakwama halafu kuna mbuzi fulani inaitwa Lucas Mwashambwa kila dakika humu jf eti Sa100 ....!!!!
 
Okey,kupunguza lasirimali watu sio Jambo baya katika projects nyingi.
Maana inatokana na mwelekeo WA kazi umefikia asilimia ngapi kuisha.
Ila stahiki za wahusika zikilipwa hakuna tatizo.
Kitu ambacho hujatuweka wazi,ni Haki zipi ambazo unahisi Kona Kona plus janja janja inaweza kupitia hapo mkuu.
Inauma Sana swala hili,ila hakuna namna,japo watu ni wengi mno.
Au labda mradi unaelekea kuisha.
Kikubwa ainisha stahiki hizo ambazo unahisi vibopa hao wanaweza kuwapiga chenga ya mwili.

Uendelee kutupa Update ya swala Hilo mkuu.Tukiwashindwa tutawaroga tu usijali🤔🤔🤔🤔🤔🤔.
 
Hatari sana, ninapata shida ninaposikia eti YARPI ana hali ngumu kiuchumi..

Huyu Yarpi alikuwepo Ethiopia na kamaliz kazi bila kelele, huku Yarpi ni giant kule Turkey na hizi projects heavy ndio issue zake za kila siku.

Nafikiri Tatizo hapa ni kifo cha JPM, angekuwa JPM yuko hai leo hii bila shaka train ingekuwa inatembea.
 
tunapoendelea kuchekacheka na hawa wafanyabiashara tutambue pia wengi wao sio Watanzania na hata Tanzania ikiwa masikini na watu wake kwao wao sio issue.
 
Hatari sana, ninapata shida ninaposikia eti YARPI ana hali ngumu kiuchumi..

Huyu Yarpi alikuwepo Ethiopia na kamaliz kazi bila kelele, huku Yarpi ni giant kule Turkey na hizi projects heavy ndio issue zake za kila siku.

Nafikiri Tatizo hapa ni kifo cha JPM, angekuwa JPM yuko hai leo hii bila shaka train ingekuwa inatembea.

Au wanataka aondoke walete wakwao. Maana aliyemleta hayupo tena duniani. Yapi Merkez ana madeni mengi na suppliers mbalimbali hapa nchini
 
Back
Top Bottom