Ni Rasmi Sasa!

Tundu Antipass Lissu mwana wa Afrika na mwanademokrasia wa kweli wa Tanzania amepitishwa rasmi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akiitangazia Dunia Mwenyekiti wa NEC Jaji Kaijage amesema Lissu ametimiza vigezo vyote na Masharti ya kuwa mgombea Urais kupitia Chadema.

Kulikuwa na hofu kubwa katika nchi kuanzia asubuhi baada ya Mgombea wa Chadema Kuwasili katika ofisi za Tume tangu asubuhi saa 5 Kama Ratiba ilivyoelekeza lakini Time haikumteua kwa wakati kwa kile walichodai bado fomu zake kuhakikiwa

Kwa kadiri muda ulivyokuwa unasogea ndivyo Watanzania walivyokuwa na hofu kwa kile walichodhani Kuna hujuma dhidi ya chaguo Lao .

Taarifa kutoka mikoa kadhaa inasema Mara baada ya kuteuliwa Shangwe za watu zimesikika kutoka sehemu kadhaa zikiwemo za starehe, masokoni na mashuleni huku kwa jiji la DSM watu kadhaa wamesikia wakipiga honi za magari barabarani Kama ishara ya kufurahia kuteuliwa Tundu Lissu ambaye anaonekana ndiye mwenye uwezekano mkubwa wa kushinda nafasi hiyo ya Urais kutokana na kuungwa mkono na Wananchi walio wengi.
[/QUOTe
hii ndo habari ilikuwa inangojewa na wengi, kazi imeanza
 
Bila presha wadau mbalimbali waliyoitoa Lissu asingetangazwa leo
Shukrani. Kwa Kigogo2014, real good luck haule, viongozi wa cdm na wanachama kwa ujumla
 
Sikuwa online, lakini nafikiri kwa sababu Lissu ni mwanasheria na muungwana sana lazima baada ya uteuzi kamshukiru sana jaji..ambaye kisheria ni senior kwake...

nakukuu

:Asante sana kaka yangu, nashukuru mno...." asante. Huku akitoa tabasam kwa kaka yake wa kisheria.

Lissu ni mtu mwema sana sana!!

Congratulations Lissu...first step done!!
 
Mahakama za Tanzania ni hovyo sana kitendo chao cha kuwarejesha wakurugenzi kuwa wasimamizi wa uchaguzi ilikuwa ni kosa kubwa sana.

Wakurugenzi ndio walio mstari wa mbele katika kuvuruga uchaguzi ili kuipendelea ccm. Kama hatutapata katiba mpya hizi chaguzi hazitakuwa na maana yoyote zitabaki kuwa ni chaguzi za kihuni tu.
 
Back
Top Bottom