Tuliowahi kufukuzwa shule au kusimamishwa shule tukuje hapa

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Mar 10, 2022
17,812
32,178
African

Mimi nilisimamishwa shule nikiwa form two kwa muda wa wiki mbili kule Iringa, shule ipo karibu na Lugalo ile ya Serikali jirani yake kuna shule ya private.

Nilisimamishwa kwa kosa la kumtukana mtu mbele ya darasa, mwalimu mmoja maarufu kwajina la Uhuchu alisikia kelele Class baada ya kuja akawa anatafutwa alieanza class wote wakasema mimi wakamtetea yule mpumbavu Zamwamwa, nilichukia sana.

Alianza nitukania mama yangu na mimi nikamjibu so nilichezea sana stiki nikaandikishwa barua kila ofisi nilikopelekwa walimu walikuwa hawaamini kama ndio mimi nimeanza tukana akaitwa mzazi wangu, akaja pale alipofika kapewa short story akaanza kulia, alikuwa ni mama kalia pale huku nachapwa.

Uhuchu huku akikazania kuwa huyu lazima afukuzwe shule, dah nilichukia sana.

Wewe mwezangu ulifanya kosa gani?
 
Tuliuza vitoto vya nguruwe,kipindi nipo seminary πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
Unanikumbusha mbali sana unajua kipindi cha pasaka sasa alikuwa anakuja father kutoka Tundurunkutufundisha mafundisho ya moyo sasa utakiwi kuongea kwa sauti asinakishindwa jizuia nikajikuta nabwatuka uko duh father alinipa afhabu ya kulishia nguruwe mwezi mzima wakat nilikuwa nasafisha nyumba yao na kuandaa chakula πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ nilikuwa sili dona
 
kuna mshikaji alipotea shule miezi miwili, siku aliyokuja akapelekwa kwa mwalimu mkuu,,,,,kuulizwa ulikuwa wapi muda huo wote akajibu nilifanywa msukule..hahaaaaaa
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ na akarudije sasa kutoka msukule
 
Mob/Crowd psychology….hii kitu ilinifundisha kwa vitendo.

Ilikuwa High school, msala wa class zima, wachache tukatolewa kafara, suspension kwa muda usiojulikana, baada ya mwezi nakuja kuitwa nikajua soo limeisha nikaambiwa utakaa nyumbani mpaka Necta ya Six itapoanza hapo kuna kama miezi miwili mbele plus na ule mmoja, nyundo tatu zikanihusu.

Kilichobaki ni mimi na familia yangu πŸ˜…
 
Mob/Crowd psychology….hii kitu ilinifundisha kwa vitendo.

Ilikuwa High school, msala wa class zima , wachache tukatolewa kafara, suspension kwa muda usiojulikana, baada ya mwezi nakuja kuitwa nikajua soo limeisha nikaambiwa utakaa nyumbani mpaka Necta ya Six itapoanza hapo kuna kama miezi miwili mbele plus na ule mmoja, nyundo tatu zikanihusu.

Kilichobaki ni mimi na familia yangu πŸ˜…
Ww jamaa inaelekea ulipigika vibaya πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Ilikuwa huzuni lakini sikujali aisee lakini nahisi nilikia nina gundu tangu nikiwa vidudu maana niliwai kufukuzwa vidudu kisa nilikua na kiu na kumuita mwanafunz mwemzangu mshkaji nipe maji nikafukuzwa shule daah

Nilipofika darasa la tano nikaiitiwa mzazi na kutishiwa kufukuzwa shule kisa nilimpiga kichwa mwanafunzi mwenzangu akavimba nundu kubwa sana, walimu waliogopa sana.

Nilipofika form four nikasimamishwa shule kwa kosa la kupita panya road mwalimu akaniwekea sigara condom na bang na kusema siingi darasani nashinda vichakani navuta bang

Nilipofika form six kuna dada alikuwa ananipenda kumbe headmaster anamtaka daaah head master akanipa kazi ya kubeba magunia ya mkaa dakika tano kabla ya mtihani nikasita sita bwanaaa wee kumbe ndio najaaa akanitumbua.
 
Back
Top Bottom