Tuliowahi kufukuzwa shule au kusimamishwa shule tukuje hapa

Ilikuwa huzuni lakini sikujali aisee lakini nahisi nilikia nina gundu tangu nikiwa vidudu maana niliwai kufukuzwa vidudu kisa nilikua na kiu na kumuita mwanafunz mwemzangu mshkaji nipe maji nikafukuzwa shule daah

Nilipofika darasa la tano nikaiitiwa mzazi na kutishiwa kufukuzwa shule kisa nilimpiga kichwa mwanafunzi mwenzangu akavimba nundu kubwa sana, walimu waliogopa sana.

Nilipofika form four nikasimamishwa shule kwa kosa la kupita panya road mwalimu akaniwekea sigara condom na bang na kusema siingi darasani nashinda vichakani navuta bang

Nilipofika form six kuna dada alikuwa ananipenda kumbe headmaster anamtaka daaah head master akanipa kazi ya kubeba magunia ya mkaa dakika tano kabla ya mtihani nikasita sita bwanaaa wee kumbe ndio najaaa akanitumbua.
Umenikumbusha form 3 kuna second master alikua mnoko sana, tulikua tunatoroka saa 4 ijumaa sasa tukawa tunapita njia ya vichakani yeye akiwa barabarani kwenye boda boda akatuona akamkariri mmoja.

J3 tupo class akaingia akasema kama ulitoroka ijumaa pita mbele, tukabunda wote! Akamfata yule aliyemkariri ktk kundi letu akamuinua na kofi moja zito sana jamaa alibanwa akatutaja wote,tukaambiwa sisi ni vibaka tunampango haramu wa kuchoma shule.
 
Back
Top Bottom