Tuliokuamini na kukutetea kwenye janga la Corona umetuangusha. Nimepoteza rafiki na ndugu kwa janga la Corona. Serikali chukueni hatua

Pole kwa msiba

Tulipiga kelele kwamba ugonjwa unafanyiwa mzaha sana. ''Tokeni mkachape kazi''
Tulisema wakati ukifika wa mtu binafsi mtatuelewa .

MsemajiUkweli na kundi lake vigelegele sifia sifia'' walikuwa busy kupotosha umma
Tukaitwa '' sisi tunaotoa tahadhari na ushauri si Wazalendo''

Hapa ndipo tulipo sasa, watu wanapukutika na masikitiko ni binafsi.

Huu ni mwanzo, subirini Mwezi May!
 
Sina haja na Rais kwenda Amana,nina haja na mikakati inayoonekana.Kwa sasa kila mahali mgonjwa akienda anakimbiwa,wahudumu hawana PPE...mahali pa Karantini watu wanakufa sababu hakuna huduma yoyote,unaumwa dalili za Corona na una kisukari,hupati huduma ya hata kimoja wapo mpaka unakufa...Kila mahali ukienda wanasema nenda kule nenda kule...sasa ni wapi watu wanatakiwa kwenda???

China walizuia misongamano kwa kauli ya kimamlaka,mikusanyiko ikaondolewa kwa muda...Huko Tz unaona nini kama sio kuwaza kodi?Pesa itawapeleka wapi ndugu yangu?Mlizaliwa nazooooo??

Hivi idadi ya wafu ingefikia kama huko China, Italia, Hispania, Marekani, nk ungetoa hoja gani? Au ungehamasisha kuingia mitaani!

Unadai mikakati inayoonekana ya kinga au tiba? Kumbuka nchi nilizozitaja, pamoja na uwezo wao, idara za afya zilishindwa kwa sababu zilizembea kuchukua hatua za kinga. China uliyoitaja imekuja kutafuta shuka kumekucha.

Ni kweli masoko na majumba ya starehe yako wazi. Je, nani anakwenda huko kama siyo sisi wenyewe? Wamiliki wa maeneo hayo wanachukua hatua gani kuwalinda wateja wao na maambukizi? Mimi kama mimi siendi sehemu ambayo hakuna usalama wa maisha yangu.

Mwisho wa siku, maamuzi ya kinga ni ya mtu binafsi.

JILINDE UMLINDE JIRANI. Tanzania bila COVID-19 inawezekana.
 
Pole kwa msiba

Tulipiga kelele kwamba ugonjwa unafanyiwa mzaha sana. ''Tokeni mkachape kazi''
Tulisema wakati ukifika wa mtu binafsi mtatuelewa .

MsemajiUkweli na kundi lake vigelegele sifia sifia'' walikuwa busy kupotosha umma
Tukaitwa '' sisi tunaotoa tahadhari na ushauri si Wazalendo''

Hapa ndipo tulipo sasa, watu wanapukutika na masikitiko ni binafsi.

Huu ni mwanzo, subirini Mwezi May!
Kama ni kweli umedhamiria janga hili lipite, basi "Kinga" ni tiba isiyo na mjadala.

Mbinu na mikakati ya "kinga" imetolewa na msisitizo wa kuzingatia unasimamiwa.
1) Iwapo wewe ni mwajiri, hakikisha usalama wa waajiriwa wako muda wote wanapokuwa kazini.
2) Mwajiriwa dai mwajiri wako mazingira salama ya mahali pako pa kazi
3) Wazazi nyumbani hakikisha familia inazingatia ushauri wa kujikinga dhidi ya maambukizi.

Serikali inatimiza wajibu wake wa kutoa ushauri na tiba kwa wale ambao masikio yao ni ya kufa kwa sababu hayasikii dawa

Kinga ni bora kuliko tiba ba gharama yake ni ndogo maana inaepusha kupoteza maisha ya wapendwa na nguvukazi.

JILINDE UMLINDE JIRANI. Kwa pamoja Tanzania bila korona inawezekana.
 
Hakika bila hatua za dhati kukabiliana na corona, Dunia yote inaweza kutulia tukabaki tunaukimbiza mwenge ndani kwa ndani.

Toka ile wizara ipanguliwe na kisha kufuatiwa na hotuba nilishapoteza imani kabisa, tutapukutika sijui yeye labda ana uhakika atabaki ili ataifishe mali ambazo zitakuwa zimeachwa na familia zilizoteketea.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo na wewe umeona umechangia point ya maana sana siyo?, haya bhana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Barafu, kwanza pole sana kwa kufiwa na rafiki rubani wa Tanapa. Pia kwa incident ya kifo cha Mzee wa jirani aliyekosa huduma hadi kupoteza maisha na familia yake kuingizwa karantini.

Tangu kuingia kwa janga la Corona, elimu ya kinga imeenezwa sana, ila kwa upande wa msimamo na kauli za rais wetu, kuna watu hawajamwelewa ukiwemo wewe.

Watanzania tuko wa aina tatu
1. Kundi la kipato cha juu na watumishi wa umma, matajiri na wafanyabiashara wakubwa. Hili ndilo kundi pekee ambalo wanaweza kuishi kwenye lockdown. Hawa wako wachache nchi ikiamua kufanya lockdown, wataendelea kulipwa even by doing nothing, na wataninua mahitaji yao yote na kujifungia ndani. Hawa ni watu wenye magari yao na wanaweza kununua mahitaji yote supermarkets. Kwenye kundi hili, they've made money and now, they use money work for them.
Yaani wanapesa ambapo wanaweza kukaa na kuitumia pesa kuwafanyia kazi. Kati ya watu milioni 50 ya Watanzania, kundi hili lina watu 10% ambao ni watu milioni 5.

2. Kundi la pili ni watu wa kipato cha kati, the working class, hawa ni wafanyakazi waajiriwa, wazalishaji mali na wafabiashara wa kati. Hawa wanafanya kazi, wanatoka jasho ndipo wapate pesa. Ikitokea lockdown hawa uzalishaji utasimama, biashara zitasimama, uchumi utatikisika na the working class watapoteza kazi, hivyo hawawezi ku survive kwenye lockdown. Hawa they work for money to live, yaani wanafanya kazi na kuvuja jasho kutafuta pesa ili waitumie hiyo pesa kuishi na kuendesha maisha yao. Ikitokea lockdown hawawezi kufanya kazi na hawawezi kupata pesa hivyo hawawezi kuishi. Kundi hili lina 20% ya Watanzania ambao ni watu milioni 10.

3. Kundi la mwisho ni kundi la watu wenye kipato cha chini, hawa they live hand to mouth, kundi hili ni kundi la wakulima, wafugaji, wavuvi na wafabiashara wadogo ambao ili waishi lazima wawahudumie, makundi yale mawili, kukitokea lockdown, kundi hili ndio most hit, watakufa njaa inabidi wagawiwe chakula, kundi hili lina 70% ya watu milioni 50, ambao ni watu milioni 35. Hawa they don't make any money, they only struggle to survive.

Uamuzi wa rais Magufuli wa no lockdown una lengo la kuzuia kuporomoka kwa uchumi wetu sio ili to make money but kuzuia watu wetu wasife njaa, kama ni kufa kwa kakolona heri wachache wafe kwa Corona, kuliko kufanya lockdown na kuua wengi kwa njaa.

P
Kwa Upande wangu Lockdown naona Ni ngumu,lakini wahudumu wa Afya kukosa Vifaa vya kujikinga huu Ni uzembe mkubwa wa Serikali.Kwanini Hizo Bilion kadhaa zilizochangwa zisiende mahospitalini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si kweli bwana acha kutetea ujinga. Mtoa mada kaeleza kila kitu kinaga ubaga unakuja na ngonjera zile zile yaani. Hivi wewe mlamba viatu ngoja nikuulize,

1. Bado huamini kwenye kuzuia mikusanyiko? Bado huamini kwenye kuzuia shughuli ili kupisha hili janga? Pamoja na kutolewa mifano hai yote hiyo bado huamini kwenye kuzuia ATCL kuruka kipindi hiki? Hivi kwa akili yako kati ya Emirates na ATCL nani anajua biashara zaidi?

2. Watu wanalaumu kwa sababu baada ya majanga kuongezeka tulitegemea Rais atoke mbele akemee na aeleze hali halisi sasa matokeo yake anatoka mbele anasema barakoa za nje zimewekewa virusi, anasema dawa ni kujifukiza! Kweli Bia unaamini haya? Katikati ya mapambano haya?

3. Kwanini data hazitolewi tena sasa? Kuna nini kinafichwa?

Kwanini hampendi kutumia akili mlizopewa bure na Mungu jamani. Hivi Dunia ikifanikiwa kutuliza hili janga Tanzania tutakuwa wageni wa nani sisi?
Lakini na sisi binadamu tunaangamia kwa kukosa maarifa ,hivi kufunga bar,kuacha kutosafiri ni lazima uambiwe na raisi,wa kujilaumu pia ni sisi wenyewe wananchi tumeshindwa kujilinda au kujikinga wenyewe ,tunasubiri matamko.huku mitaani tunaona watoto wamezagaa wakicheza cha ndimu,na wazazi tupo kwenye vijiwe vya kahawa.Je tumelazimishwa kwenda makanisani au misikitini,lakinii bado tunajaa huko makanisani na misikitini,kwanini uende huko wakati unajua mikusanyiko kwa wakti huu haifai,je napo tunamsubiri raisi aseme msiende huko?tumeambiwa tuvae barakoa tunapotoka majumbani au tukiwa kwenye mabasi lakini watu hatuvai,tumeambiwa tupunguze safari bado watu tunasafiri,kwanini tunasubiri viongozi,maisha yako hayaongozi na kiongozi wa serikali bali ni wewe mwenyewe.
 
Mkuu Barafu, kwanza pole sana kwa kufiwa na rafiki rubani wa Tanapa. Pia kwa incident ya kifo cha Mzee wa jirani aliyekosa huduma hadi kupoteza maisha na familia yake kuingizwa karantini.

Tangu kuingia kwa janga la Corona, elimu ya kinga imeenezwa sana, ila kwa upande wa msimamo na kauli za rais wetu, kuna watu hawajamwelewa ukiwemo wewe.

Watanzania tuko wa aina tatu
1. Kundi la kipato cha juu na watumishi wa umma, matajiri na wafanyabiashara wakubwa. Hili ndilo kundi pekee ambalo wanaweza kuishi kwenye lockdown. Hawa wako wachache nchi ikiamua kufanya lockdown, wataendelea kulipwa even by doing nothing, na wataninua mahitaji yao yote na kujifungia ndani. Hawa ni watu wenye magari yao na wanaweza kununua mahitaji yote supermarkets. Kwenye kundi hili, they've made money and now, they use money work for them.
Yaani wanapesa ambapo wanaweza kukaa na kuitumia pesa kuwafanyia kazi. Kati ya watu milioni 50 ya Watanzania, kundi hili lina watu 10% ambao ni watu milioni 5.

2. Kundi la pili ni watu wa kipato cha kati, the working class, hawa ni wafanyakazi waajiriwa, wazalishaji mali na wafabiashara wa kati. Hawa wanafanya kazi, wanatoka jasho ndipo wapate pesa. Ikitokea lockdown hawa uzalishaji utasimama, biashara zitasimama, uchumi utatikisika na the working class watapoteza kazi, hivyo hawawezi ku survive kwenye lockdown. Hawa they work for money to live, yaani wanafanya kazi na kuvuja jasho kutafuta pesa ili waitumie hiyo pesa kuishi na kuendesha maisha yao. Ikitokea lockdown hawawezi kufanya kazi na hawawezi kupata pesa hivyo hawawezi kuishi. Kundi hili lina 20% ya Watanzania ambao ni watu milioni 10.

3. Kundi la mwisho ni kundi la watu wenye kipato cha chini, hawa they live hand to mouth, kundi hili ni kundi la wakulima, wafugaji, wavuvi na wafabiashara wadogo ambao ili waishi lazima wawahudumie, makundi yale mawili, kukitokea lockdown, kundi hili ndio most hit, watakufa njaa inabidi wagawiwe chakula, kundi hili lina 70% ya watu milioni 50, ambao ni watu milioni 35. Hawa they don't make any money, they only struggle to survive.

Uamuzi wa rais Magufuli wa no lockdown una lengo la kuzuia kuporomoka kwa uchumi wetu sio ili to make money but kuzuia watu wetu wasife njaa, kama ni kufa kwa kakolona heri wachache wafe kwa Corona, kuliko kufanya lockdown na kuua wengi kwa njaa.

P
Bwana Paskali watu wanamuelewa mkuu ndio maana hawakubaliani nae, kwanza kuelimisha wananchi siukweli elimu nyingi iliyotolewa haina msingi unawaambia wavae barakoa wakati uwafundishi hata jinsi ya kuivaa na kuivua barakoa sawasawa, na izo barakoa nyingi ni chini ya kiwango so maambukizi yako pale pale.
Ukija kwa mkuu anakosea kuukashifu ugonjwa kama hauna madhara wakati yeye kajificha katutosa sisi.
Kama ulivyosema watanzania wengi ndio wako mbele iyo asilimia kubwa ya kundi la tatu ukitoa wakulima na wavuvi wao hawakaribiani sana na watu. Lakini hao wafanyabiashara wadogo ndio kundi kubwa na ndio wenye uwezo mkubwa wakufanya maambukizi makubwa, nilifikiri mkuu atatoa maelekezo jinsi gani ya hawa kufanya biashara zao bila kuambikizana mfano masokoni au maduka wasiingie watu wengi kwa mkupuo mmoja, umbali wa muuzaji na mnunuaji wasisogeleane, mnunuzi asiwe anashikashika bidhaa wakati wa kuchagua unayoshika ndio unayo chukua.
Vitu vingi serikali na mkuu walitakiwa wajenavyo kuzuia mlipuko kuliko kuwaambia watu wajifukize huo ni utani haijathibitishwa sehemu yeyote kisayansi kama unaweza kuzuia Corona kwa iyo njia.
Tusipoangalia Tanzania ndio itauwa watu wengi kwenye ili janga zaidi ya nchi zote duniani.
 
Wewe Bwana yako tu huwezi kumtimizia haha zake za kimsingi ije iwe masuala ya kitaifa, huyawezi wewe,utabaki kutumwatumwa tu kama pochi. Hapa anatetewa mtu au maamuzi yanayofanyika..hivi weww kwa akili zako mbuzi unategemea Nini kingefanyika...mmebaki kulalamika na kutoa matusi Wala hamjui Nini kifanyike..mawazo mmefikisika na bahati mmeanza kupasuana wenyewe kwenye lichama lenu kumtafuta mgombea urais..eti mnamtaka Lissu..shwainnnnn..Nani amewaambia Lisssu atarudi nchini..ni ndoto hizo..mmebaki mmevurugwa Kama maharage ..Mbowe hamuntaji lakini hamna jinsi huyohuyo...dikteta wenu mpaka mnyoroke. Shenzzzz
Rubbish
 
Ni dhahiri kuwa kwa sasa Rais John Pombe Magufuli anajionyesha kuwa katika uongozi wake,suala la majanga na uhai wa wananchi wake hayana vipaumbele.Kwake ni pesa na kuona uchumi unakuwa.Rais wetu tofauti na matarajio yetu,amelinganisha uhai na thamani ya pumzi ya watu wake na uchumi wa nchi,kwake Uchumi kwanza uhai baadae.

Huyu sio Rais ambaye kwa sasa unaweza kutoka mbele ya wafiwa na wahanga wa corona na kuwaeleza kuwa ni Rais wa wanyonge, hata mara maja, abadani haitawezekana kwa sasa. Ni kama mkubwa wetu huyu kayaweka maisha ya watu wake rehani na kuutazama kwanza uchumi na pesa.

Kuna malalamiko mengi juu ya ubovu wa huduma za afya katika sehemu walizotengewa wagonjwa wa COVID-19,anatumia mpaka magazeti ya serikali kueneza propaganda kuwa vifaa tiba vimejaa kila mahali, ukweli ni kuwa, huko Mnazi Mmoja, Amana na Mwananyamala wahudumu wa afya ni kweli wanawakimbia wagonjwa sababu na wao wanaokoa maisha yao kwa kukosa PPE.

Watu wanakufa,watu wanaambukizana na kwa kweli wengine wanaangamia kwa sababu ya kauli za Rais na matendo yake.Hali ni mbaya ndugu zangu,tusisikilize propaganda.

Sasa bila shaka kila mtaa umeanza kukumbwa na vifo vya Corona,juma la jana,familia ya rafiki yangu waliuguliwa na mzee wao kwa ugonjwa wa Corona,wakatoka nyumbani kwenda hospitali ya jirani ya Palestina,huko wakawaambia waende Amana,kufika hapo wakaambiwa wanatakiwa kwenda Buguruni kwa Mnyamani ndio kuna kituo kinashughilikia,kufika Buguruni wakaambiwa waende Mloganzila maana ndio watapata haduma.

Safari yote hiyo mgonjwa hana huduma yoyote,walipofika Mloganzila wakaambiwa hawana huduma yoyote,katikati ya bumbuwazi mgonjwa akafariki bila matibabu,na baadae serikali kuuchukua mwili na kuuzika kwa madai kuwa wamechukua sampuli za maiti na kuona maambukizi,familia nzima sasa ipo karantini.

Ummy Mwalimu na Serikali,iseme sasa,na iseme tena,kwanini kila mahali wagonjwa wanakataliwa??Wagonjwa wetu tupeleke wapi?

Habari mbaya kwangu,na ngumu sana,ni kumpoteza rafiki yangu wa muda mrefu,mwanafunzi wangu na comrade wangu mcheshi,huyu alikuwa rubani wa ndege za TANAPA ambaye amepoteza maisha kwa janga la corona na hayupo hata katika kundi la watu waliotangazwa kuwa wamekufa na ugonjwa huu.Huyu ameondoka na watu kadhaa nyuma yake ambao walimbukizana.Na hao watu wameambukiza wengine...Hali ni mbaya na bado serikali inashindwa kutoa sauti ya kimamlaka kuonyesha kuwa hali ni mbaya.

Marehemu huyu(nahifadhi jina lake) siku kadhaa nyuma tuliwasiliana akienda kuhuisha mambo yake ya leseni za urubani na vibali kadhaa pale mamlaka ya Usafiri wa Anga,na baadae kuwa na training nje ya jiji la Dsm wakiwa na mwenzake na watumishi kadhaa wa mamlaka,maanake alikutana na watumishi hapo mahali,hao watumishi wana familia zao,na hao sehemu ya familia wana jamaa zao wengine makazini na mitaani.

Naambiwa sehemu ya ofisi za Mamlaka hizo watumishi wapo karantini sababu waligusana au kuchangamana na marehemu rafiki mpendwa na mwenzake.

Kwa hali hii,bado serikali imejaa vitisho,haizuii misongamano,haiuzuiii mjii wa Dsm kusongamana katika bars,kumbi za starehe na mikusanyiko mingi.Mji upo wazi kusambaza magonjwa mikoani kwa jina la "Kukuza Uchumi".Huu ni unyama gani?Tunawaza pesa juu ya uhai?

Mgonjwa mmoja wapo kule Rukwa,alitokea Dsm kwa njia ya ndege ya ATCL,akapanda ndege mpaka Mpanda na akasogea mpaka Sumbawanga,hapo kaacha ugonjwa kuanzia kwenye ndege,Mpanda hadi Sumbawanga,maanake alichangamana na abiria wengine,alioambukiza ndio wenye dalili na walio hoi,maanake tamaa za uchumi na pesa,zinafanya tunarusha ndege toka Dsm kwenda Mpanda ili ipeleke ugonjwa ukasambae vijijini kwa masikini na wanyonge.Hao Emirates na wengine walifunga safari sio kwamba hawajui pesa,wanajali uhai wa watu wao.

Hizi ni dalili mbaya za kiuongozi,huu ni uuwaji usiokuwa wa moja kwa moja au ni tuseme wa moja kwa moja.Ni ukosefu wa utu na upendo kwa watu ulioapa kuwalinda ukiwa na katiba kuume na kitabu cha dini kushoto.Wewe baba badilika,okoa watu wako...hiyo ndio kazi tuliokupa kwa njia ya kura.

Sasa ni kama hata data zinapikwa,watu wengi wanakufa,tumeanza kupoteza hata wahudumu wa afya ambao ni askari wetu wa mstari wa mbele...Watumishi wa afya wameanza kufa kwa maambukizi ya kukosa PPE!

Serikali ipo,inaaminisha tutapona kwa mvuke,ni labda kweli,lakini kwanza ilipaswa tuwaambie watu wetu kuwa hali ni mbaya,kukiri kuzidiwa na ugonjwa huu sio udhaifu wa kiuongozi bali ni uimara wa kiuongozi,hii ni kwasababu unawapa watu wako taarifa iliyo kamili na bora.

Sasa barakoa zilizothibitishwa na mamlaka za viwango zinakosa wateja,sababu Rais kaongea hadharani kuwa haziaminiki sababu zinaweza kuwa na virusi.Kazi hii sasa imeachiwa kwa machinga na mafundi cherehani,ambao sasa wanachonga barakoa zisizo thibitishwa ubora wake na mamlaka yoyote.

Si mbaya kuwa na barakoa ya kitambaa,lkn ni hakika kuwa wataalamu wanaeleza kuwa haizuii virusi kwa kiwango hicho zaidi ya kuzuia vumbi tu,lkn haya yote ni sababu ya kauli ya Rais ambayo ina mamlaka ndani yake.

Katika masoko,makanisani na misikitini bado watu wanajazana...Hali ni mbaya,na kwa sababu kwa siku kadhaa serikali imeanza kutaja tu wanaopona kwa idadi kubwa,hatutaji tena vifo,tukidhani kifo ni aubu,kumbe kwa mantiki ya ugonjwa huu wanaopona hata wakiwa 1000,lazima tulie na aliyekufa mmoja,sababu uhai na utu wa mtu una thamani isiyofananishika.Kila mahali sasa watu wamelegeza kufuata kanuni za afya na kujikinga wakiona kuwa wataugua na kupona.

Kuusema ukweli juu ya ugonjwa huu si kuleta hofu,ni kuelezea ukweli na uhalisia wa madhara ya gonjwa hili.Kuficha data sio sifa za uongozi bora,bali ni sifa za uongozi mbovu unaouwa watu wake kwa kufanya "Massaging of data"

Toka mafichoni Rais,wewe ni Amiri Jeshi mkuu,kaa mstari wa mbele...Umekuwa ukivaa magwanda kuonyesha u mwanajeshi,sasa onyesha kwa vitendo...Njoo mbele baba njoo,wasisitize watu wako kuwa hali ni mbaya.

Mikoa iliyoathirika kama Dsm,si lazima uifunge,ruhusu magari ya mizigo na chakula kuingiza na kutoa bidhaa kupeleka mikoani.Hii itasaidia kupunguza maambukizi.

Huwezi kuelewa bandiko hili,mpaka sehemu ya ndugu au jamaa yako afe kwa ugonjwa huu katika mazingira ambayo kuna uzembe mkubwa kutoka kwa watu tuliowapa dhamana...Hii ni ujinga,ni ajabu sana kwanini watu wanashindwa thamini maisha ya watu na wanaona pesa ni bora zaidi.

Zile tambo zote na mikakati mliyotutambia kuwa hii ni serikali mpya,mbana zimefifia??Okoa maisha ya watu wako,pesa makaratasi.
Corona inapukutisha watu Dar. Kuna wanaolalamika ndugu zao kuzikwa kinguvu na Mamlaka Dar huko Bahari Beach, Buza na Mbweni - JamiiForums
 
Mkuu Barafu, kwanza pole sana kwa kufiwa na rafiki rubani wa Tanapa. Pia kwa incident ya kifo cha Mzee wa jirani aliyekosa huduma hadi kupoteza maisha na familia yake kuingizwa karantini.

Tangu kuingia kwa janga la Corona, elimu ya kinga imeenezwa sana, ila kwa upande wa msimamo na kauli za rais wetu, kuna watu hawajamwelewa ukiwemo wewe.

Watanzania tuko wa aina tatu
1. Kundi la kipato cha juu na watumishi wa umma, matajiri na wafanyabiashara wakubwa. Hili ndilo kundi pekee ambalo wanaweza kuishi kwenye lockdown. Hawa wako wachache nchi ikiamua kufanya lockdown, wataendelea kulipwa even by doing nothing, na wataninua mahitaji yao yote na kujifungia ndani. Hawa ni watu wenye magari yao na wanaweza kununua mahitaji yote supermarkets. Kwenye kundi hili, they've made money and now, they use money work for them.
Yaani wanapesa ambapo wanaweza kukaa na kuitumia pesa kuwafanyia kazi. Kati ya watu milioni 50 ya Watanzania, kundi hili lina watu 10% ambao ni watu milioni 5.

2. Kundi la pili ni watu wa kipato cha kati, the working class, hawa ni wafanyakazi waajiriwa, wazalishaji mali na wafabiashara wa kati. Hawa wanafanya kazi, wanatoka jasho ndipo wapate pesa. Ikitokea lockdown hawa uzalishaji utasimama, biashara zitasimama, uchumi utatikisika na the working class watapoteza kazi, hivyo hawawezi ku survive kwenye lockdown. Hawa they work for money to live, yaani wanafanya kazi na kuvuja jasho kutafuta pesa ili waitumie hiyo pesa kuishi na kuendesha maisha yao. Ikitokea lockdown hawawezi kufanya kazi na hawawezi kupata pesa hivyo hawawezi kuishi. Kundi hili lina 20% ya Watanzania ambao ni watu milioni 10.

3. Kundi la mwisho ni kundi la watu wenye kipato cha chini, hawa they live hand to mouth, kundi hili ni kundi la wakulima, wafugaji, wavuvi na wafabiashara wadogo ambao ili waishi lazima wawahudumie, makundi yale mawili, kukitokea lockdown, kundi hili ndio most hit, watakufa njaa inabidi wagawiwe chakula, kundi hili lina 70% ya watu milioni 50, ambao ni watu milioni 35. Hawa they don't make any money, they only struggle to survive.

Uamuzi wa rais Magufuli wa no lockdown una lengo la kuzuia kuporomoka kwa uchumi wetu sio ili to make money but kuzuia watu wetu wasife njaa, kama ni kufa kwa kakolona heri wachache wafe kwa Corona, kuliko kufanya lockdown na kuua wengi kwa njaa.

P
Corona inapukutisha watu Dar. Kuna wanaolalamika ndugu zao kuzikwa kinguvu na Mamlaka Dar huko Bahari Beach, Buza na Mbweni - JamiiForums
 
Mkuu Barafu, kwanza pole sana kwa kufiwa na rafiki rubani wa Tanapa. Pia kwa incident ya kifo cha Mzee wa jirani aliyekosa huduma hadi kupoteza maisha na familia yake kuingizwa karantini.

Tangu kuingia kwa janga la Corona, elimu ya kinga imeenezwa sana, ila kwa upande wa msimamo na kauli za rais wetu, kuna watu hawajamwelewa ukiwemo wewe.

Watanzania tuko wa aina tatu
1. Kundi la kipato cha juu na watumishi wa umma, matajiri na wafanyabiashara wakubwa. Hili ndilo kundi pekee ambalo wanaweza kuishi kwenye lockdown. Hawa wako wachache nchi ikiamua kufanya lockdown, wataendelea kulipwa even by doing nothing, na wataninua mahitaji yao yote na kujifungia ndani. Hawa ni watu wenye magari yao na wanaweza kununua mahitaji yote supermarkets. Kwenye kundi hili, they've made money and now, they use money work for them.
Yaani wanapesa ambapo wanaweza kukaa na kuitumia pesa kuwafanyia kazi. Kati ya watu milioni 50 ya Watanzania, kundi hili lina watu 10% ambao ni watu milioni 5.

2. Kundi la pili ni watu wa kipato cha kati, the working class, hawa ni wafanyakazi waajiriwa, wazalishaji mali na wafabiashara wa kati. Hawa wanafanya kazi, wanatoka jasho ndipo wapate pesa. Ikitokea lockdown hawa uzalishaji utasimama, biashara zitasimama, uchumi utatikisika na the working class watapoteza kazi, hivyo hawawezi ku survive kwenye lockdown. Hawa they work for money to live, yaani wanafanya kazi na kuvuja jasho kutafuta pesa ili waitumie hiyo pesa kuishi na kuendesha maisha yao. Ikitokea lockdown hawawezi kufanya kazi na hawawezi kupata pesa hivyo hawawezi kuishi. Kundi hili lina 20% ya Watanzania ambao ni watu milioni 10.

3. Kundi la mwisho ni kundi la watu wenye kipato cha chini, hawa they live hand to mouth, kundi hili ni kundi la wakulima, wafugaji, wavuvi na wafabiashara wadogo ambao ili waishi lazima wawahudumie, makundi yale mawili, kukitokea lockdown, kundi hili ndio most hit, watakufa njaa inabidi wagawiwe chakula, kundi hili lina 70% ya watu milioni 50, ambao ni watu milioni 35. Hawa they don't make any money, they only struggle to survive.

Uamuzi wa rais Magufuli wa no lockdown una lengo la kuzuia kuporomoka kwa uchumi wetu sio ili to make money but kuzuia watu wetu wasife njaa, kama ni kufa kwa kakolona heri wachache wafe kwa Corona, kuliko kufanya lockdown na kuua wengi kwa njaa.

P
Lakini serikali inabidi igawe barakoa ,igawe sanitizer bure kwa wananchi hao wa kipato cha chini wakati wakifanya shughuli zao kuepuka kuenea zaidi kwa ugonjwa!!
 
Back
Top Bottom