Tabaka la Wahafidhina linavyo Mkwamisha Rais Mwinyi Zanzibar

Deogratias Mutungi

Senior Member
Oct 1, 2019
139
179
TABAKA LA WAHAFIDHINA LINA MKWAMISHA RAIS MWINYI

Deogratias Mutungi

Nianze Makala haya kwa kurejea viongozi hawa nguli , Hastings Kamuzu Banda rais wa zamani wa Malawi, na Waziri Mkuu wa Zamani wa Uingereza Winston Churchill, Banda wakati fulani aliwai kusema, ” Kiongozi mwenye utashi wa kuongoza watu ataonekana kwa matendo yake na dhamira ya utumishi kwa watu kutokana na falsafa zake za utawala” aidha Churchill naye akasema “ Ukiwa unasafiri na ukaruhusu kutupa jiwe kwa kila mbwa anayebweka hutoweza kuendelea na safari”

Naam!!! kwa nukuu hizi za Banda na Churchill, tunaiona dhamira ya uongozi wa rais Mwinyi kuwa njema kifalsafa na yenye dira ya utatuzi wa ombwe la matatizo ya wazanzibar licha ya kelele na changamoto za wahafidhina, hata hivyo ili kukabiliana na wahafidhina ndani ya serikali na chama ni sharti rais arejee kwenye usemi wa Winston Churchill.

Wahafidhina wanao jengewa hoja hapa ni wale wasio kuwa na nia njema na rais pamoja na serikali yake, ni wale wahafidhina nuksi, Kwa miongo mingi sasa CCM imekuwa na wahafidhina wenye sumu kali katika ustawi wa maendeleo ya vitu na watu. Mwl. Nyerere aliwai kusema wapo watu wa kuogopwa kama ukoma, na wahafidhina wa namna hii ni sawa na ukoma kwa ustawi wa dira ya maendeleo ya Wazanzibar.

Kwa muhtsari turejee kauli ya rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt.Jakaya Kikwete aliyoitoa mwaka 2010 “CCM hatuaminiani mpaka hata kwenda msalani unaogopa kuacha glasi ya maji unayokunywa kwa waliokuzunguka kwa kuhofia usalama wako” hii ni kauli nzito ambayo ililenga kuonesha tabia za uhafidhina ndani ya mifumo ya chama kuwa ni hatarishi zaidi kuliko inavyofikiriwa, na kauli hii ya JK bado inaishi miongoni mwa wana CCM, uaminifu ni mdogo baina ya mwana CCM na mwana CCM.

Kundi hili la wahafidhina ni kundi lenye mifumo ya unyonyaji na ufisadi ndani yake lenye kulinda zaidi maslahi binafsi kuliko ya umma, ni watu wasio na utu wala soni, wahafidhina hawa uwa wakali pale maslahi yao yanapoguswa kwa namna moja au nyingine ni miongoni mwa makundi hatarishi katika medali za siasa hasa siasa za mabadilko kutoka kwenye mifumo ya zamani kwenda kwenye mifumo mipya.

Ifahamike kuwa rais Hussein Mwinyi anayo nia njema ya kuijenga Zanzibar yenye falsafa bora za uchumi wa kisasa na siasa zenye mrengo wa ustawi wa amani kwa wazanzibar wote, bahati mbaya jitihada za rais Mwinyi zinakwamishwa kwa namna moja au nyingine na baadhi ya wahafidhina waliopo ndani ya mifumo ya serikali na Chama Cha Mapinduzi CCM, kundi hili la wahafidhina nia yao kisiasa ni ovu, siasa zao na utumishi wao ni kuikwamisha serikali ya awamu ya nane sambamba na kuifitinisha kwa wananchi, wanayo nongwa ya kuiona serikali inakwama kiutendaji na kimfumo.

Genge hili la wahafidhina linao mtandao ulio ndani ya chama na serikali, wachache wanajitokeza wazi kukosoa serikali ya rais Mwinyi, wengineo wanaratibu na kufadhiri mipango ya kukwamisha maendeleo na mikakati ya rais wakiwa nyuma ya pazia, Ifahamike kuwa kukosoa serikali si dhambi kisiasa wala jinai kikatiba, bali ukosoaji wa mifumo na utendaji wa serikali uambatane na hoja, ushauri na namna bora ya kuleta maendeleo ya wananchi na si vijembe na lugha zisizo na staha kwa rais na taasisi zake.

Ikumbukwe kuwa mnamo January 25, mwaka huu Simai Mohamed Said alitangaza kujiuzulu kama Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, kimantiki hoja za kujiuzulu kwake zilikuwa hoja zenye uhafidhina ndani yake na udhaifu wa mantiki katika medani za siasa, aidha matamshi na kauli alizowai kutoa Balozi Karume juu ya rais Mwinyi ni nongwa za kihafidhina na zenye mtandao hasi dhidi ya utawala wa awamu ya nane, sambamba na matamshi ya Mzee Baraka Mohamed Shamte dhidi ya rais Mwinyi ni porojo za uhafidhina zilizo lenga kufitinisha mamlaka na wananchi wake.

Mantiki ya siasa inaonyesha penye uhafidhina na misuguano ya kisiasa ni nadra maendeleo ya kweli kushika hatamu kwa sababu muda mwingi uwekezwa kwenye hujuma, majungu na mikwaruzano ya kisiasa badala ya kujenga na kutatua kero za wananchi mambo ambayo ni hasi kwa uchumi wa nchi na watu wake.

Hata hivyo ukirejea takwimu za kiuchumi tangu rais Dkt. Hussein Mwinyi aapishwe kama rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar mnamo novemba 2, 2020 ni takwimu za kijani na zenye ustawi kwa wazanzibar, Uchumi umekuwa kwa kasi ya wastani wa asilimia 7.1 kwa sasa, ikilinganishwa na wastani wa asilimia 5.1 kwa mwaka 2021, ikiwa lengo la ukusanyaji wa mapato kuvukwa kwa asilimia 1.7, huku nakisi ya urari wa biashara ikiongezeka, takwimu hizi ikiwa ni kwa mujibu wa benki kuu ya Tanzania.

Hivyo uwepo wa uhafidhina ndani ya chama na serikali ni hulka na tabia ya baadhi ya viongozi wenye ghiriba za kuikwamisha serikali ya awamu ya nane kwa agenda zao wenyewe na si vinginevyo, ni wazi kuwa ndani ya chama wapo wahafidhina wenye msimamo mkali (fundamentalists), wanaopinga kila badiliko lenye tija linalofanywa na rais liwe la kiuchumi, kisiasa kijamii, michezo au kisayansi wao ni kupinga tu hamna jema kwao.

Siasa za namna hii ni za kihuni na hazina heri wala mashiko kwa mwananchi wa kawaida, kama ambavyo Balozi Humphery polepole amekuwa akisema mara kadhaa kuwa siasa za hivi ni siasa za kihuni hazikubaliki katika mifumo yetu ya uongozi hapa nchini.

Tabaka la wahafidhina waliopo ndani ya serikali na chama ni wale wasio kubali mabadiliko, ni kundi la wanasiasa na watumishi wanaoendelea kushikilia ukale pasipo kutaka mabadiliko ni watu wenye vinasaba vya uchoyo na uroho wa madaraka na udini ndani yake, ni vikundi vidogo vyenye mavazi ya ngozi ya kondoo kwa juu lkn ndani ni chui, makundi haya ni mfu kifikra na kifalsafa katika mabadiliko yanayoendelea visiwani Zanzibar kwa lengo la kuimarisha uchumi imara na wenye tija na ushindani ndani na nje ya Afrika.

Genge hili la wahafidhina ni hatari na wamejipanga kuikwamisha serikali ya awamu ya nane kwa namna yoyote ile, Japo kwa jitihada za kiintelejensia, siasa safi na falsafa za rais Mwinyi zinazoendelea visiwani Zanzibar ni ngumu wahafidhina hawa kufikia dhamira waliyo nayo ya kuikwamisha serikali ya awamu ya nane.

Umaskini wa Afrika kwa upande mwingine unachangiwa na tabaka la watu wenye tabia za kutokubali mabadiliko wenye hulka na dhana ya “ukalelism” uwezi kukwepa mabadiliko ya kisiasa na kimuundo, usipo yakubali yatakubadilsha yenyewe.

Kila rais na falsafa yake, nyakati utofautiana, kila zama na jambo lake, dunia hii mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi kamwe hayakwepeki, ni vema wahafidhina wakasoma alama za nyakati na kujumuika na upande wa pili wenye dhamira ya kustawisha watu kupitia fursa za maendeleo jumuishi, Mabadiliko ya kisiasa ni sawa na mkondo wa maji husipo upisha shati ukosombe tu.

Stori ndeeeefu nitamalizia kusoma baadae, ungetaja majina kadhaa at least! Otherwise hii nayo ni chai tu labda useme ati waarabu wapemba wajuana kwa vilemba,sisi kwa sisi kina yakhe, machogo haiwahusu!!
 
New Chawa in Town!

Huyu kasahau kuweka mawasiliano yake.

Ana nia njema na Zanzibar ndio aingie madarakani kwa kura za wizi na mauwaji? Mnadhani watu wamesahau?

The end doesn't justify the means.

Mwinyi - kama wanasiasa wengine walivyo - yupo kwa maslahi ya familia yake, sio vyenginevyo.
 
Hueleweki vizuri, umeandika kirefu kwa ufasaha lakini mantiki ya uchambuzi wa hoja zako ni duni.
Huo uhafidhina ndio nini hasa katika andiko lako?
Ulitaka Mwinyi asikosolewe au kupingwa?

Waziri wake aliyeamua kujiuzuru kwa kutofautiana naye, kwanini umeone amekosea, wakati ndivyo ilipaswa?

Msimamo wa Karume unafahamika siku zote, kuutoa dhidi ya serikali ya Mwinyi, kuna shida gani?
 
Stori ndeeeefu nitamalizia kusoma baadae, ungetaja majina kadhaa at least! Otherwise hii nayo ni chai tu labda useme ati waarabu wapemba wajuana kwa vilemba,sisi kwa sisi kina yakhe, machogo haiwahusu!!
Mkuu kwasababu umesema hujasoma mpaka mwisho alafu unashauri eti angetaja majina machache, sasa hayo majina machache hayapo kwenye mada? Husomi mada yote alafu unakurupuka kutoa opinion, kazi kweli kweli🙄
 
Kwa muhtsari turejee kauli ya rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt.Jakaya Kikwete aliyoitoa mwaka 2010 “CCM hatuaminiani mpaka hata kwenda msalani unaogopa kuacha glasi ya maji unayokunywa kwa waliokuzunguka kwa kuhofia usalama wako” hii ni kauli nzito ambayo ililenga kuonesha tabia za uhafidhina ndani ya mifumo ya chama kuwa ni hatarishi zaidi kuliko inavyofikiriwa, na kauli hii ya JK bado inaishi miongoni mwa wana CCM, uaminifu ni mdogo baina ya mwana CCM na mwana CCM.
Tunaongozwa na Kundi la Hamasi Tanzania😆😆
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom