Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,574
- 19,457
- Thread starter
- #41
Ogah Inawezekana kweli ndilo tatizo letu; ni ada yetu watanzania kutofanya mambo siriasi!! Teh!! teh!! teh!!!Mwl Kichuguu,
BTW.......unakumbuka tuliwahi kuwa na mijadala ya namna hii......na kuna sehemu tulifika kwenye ule mjadala tukaona tunachokosa ni Katiba inayokidhi yale tuyatakayo kama nchi..............tukaanza mchakato wa kukusanya maoni na mapendekezo yetu.....yaliyotokana na ule mjadala katiba ikiwemo......mpaka ikawekwa electronic copy ya katiba........tena nakumbuka wewe ulijitolea kuhariri maoni......hivi ile kazi iliishia wapi......au ndio matatizo yenyewe tuliyonayo?
Nadhani wakati tunashughulika na swala la kuhariri maoni yale ya katiba kuna jambo lililojitokeza, ambalo sasa silikumbuki tena lakini lilikuwa lina effect fulani katika ukusanyaji wa maoni. Ni takribani miaka mitano imepita sasa; inawezekana ni wakati tulipovurugwa vurugwa kutoka Jambo Forums hadi Jamiiforums au kulikuwa na jambo la kikazi lililoniingilia, au mjadala ule ulifutwa kwa namna fulani.
Swali langu la leo zaidi ni kuhusu tabia zetu kama watanzania kubadilika vile ingawa tulikuwa chini ya katiba hiyo hiyo. Ingawa sote tunayoosha kidole kwa uongozi na utawala kwa jumla, nadhani tukubalinae kuwa tabia zetu binafsi nazo ndizo zinazosababisha tuwe na uongozi mbuvu, siyo kweli kuwa uongozi mbovu ndio unaotuletea tabia mbaya. Hali ya uchumi ni sababu moja kama ambavyo wengi tunaamini ila kama DAR si LAMU alivyoainisha tena, na nimekubaliana naye ni kuwa tuna tabia ya unafiki sana wa kufanya mambo kiuongouongo na kibabaishaji ndiyo imezalisha hayo mengine mengi. Hata kama tutakuwa na katiba nzuri lakini tukajiendesha kwa mtindo huu huu wa kutokuwa na ethics, na unafiki basi katiba itabaki ni kijitabu tu. Ni kama ambavyo hivi sasa tuna sheria dhidi ya rushwa na tuna vyombo vya kupiga rushwa lakini hakuna linaloendelea. Inabidi kwanza tuangalie namna ya kutibu tabia zetu sisi wenyewe kabla ya kuangalia sheria zikoje; jambo ambalo kama Mkandara alivyoweka bayana ni kuwa tabia hizi zimejengwa kutokana na elimu duni na umaskini.
Last edited by a moderator: