Tulikosea Wapi? Tufanyeje Kujirekebisha?

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,544
19,402
Hili ni jambo ambalo hunisumbua sana akilini mwangu, na ninaoma tulijadili kwa usikivu bila mipasho na ushabiki, ikiwezekana. Unaweza kuingia ofisini kwa mtu ukamkuta anaongea mambo ya kiumbea na rafiki yake kwenye simu wakismuliana jinsi mambo yalivyokuwa kwenye sherehe za harusi jana yake. Unaweza kumsubiri pale labda kwa saa moja, na atakapomaliza hawezi hata kukuomba radhi, badala yake anaweza kukupa maneno ya mnyanyaso mengi sana.

Vile imekuwa ni jambo la kawaida sana tunapopatwa na majanga, serikali huwa inakuwa msitali wa mbele kuomba misaada kutoka nje, kama kuwa hawakuwa wamejiandaa kwa matukio ya aina hiyo. Majanga mengi yamekuwa yanatokea nchini mwetu kila mara mara tena kwa pettern inayojiruidia rudia na wala hatujawa na mkakati wa kuyadhibiti.

Siku hizi imekuwa ni kawaida sana mtu kutajirika haraka sana akishaingia kwenye madaraka ya kiserikali na kufungua akaunti kubwa sana kwenye nchi za nje, wakati ambapo tunaambiwa eti serikali haina pesa.

Mambo ya aina hiyo na mengine yamenifanya kujiuliza kwa makini na kuhitimisha kuwa Tanzania:

(a) Hatujali kabisa ethics za kazi; nadhani hili linaeleweka sana.
(b) Hatujitumi kazini katika majukumu ambayo hayana rushwa; hatuogopi utendaji mbovu.
(c) Tunapowewa madaraka, tunaamini kuwa tuko entitled kuwa na madaraka hayo, na tunaweza kujipatia chochote kutokana na madaraka hayo.
(d) Tunathamini sana mali kuliko heshima; tuko tayari kulamba kiatu cha mwekezaji ili atupatie kitu kidogo.
(f) Tunapenda sana njia za mkato kwa kila kitu. Tukiwa na matatizo tunapenda kumtafuta mtu mwingine atutatulie
(g) Hatutaki kuwajibika wala kuwawajibisha tuliowapa majukumu. Kila wakati tunaamini kuwa tuko right, yanapotokea makosa katika mazingira yetu basi tunakuwa wa kwanza kutafuta mtu au kitu cha kulaumu; tukikosa kitu cha kulaumu basi tunamlaumu Mungu.


Mambo haya yameungana kiasi kuwa ni huwezi kuondoa moja ukaacha mengine. Kwa bahati mbaya mambo hayo ndiyo yanasoababisha tunashindwa kuendelea.

Kwa watu walioshi miaka ya sitini na ile ya sabini wakati bado kuna siasa za Ujamaa na Kujitegemea, mtakubaliana nami kuwa mambo hayo hayakuwamo miongoni mwa jamii yetu. Yalianza kukua kidogo kidogo mwanzoni mwa miaka ya themanini baada ya vita, na yakaua kwa kasi sana kuanzia mwishoni mwa miaka hiyo ya themanini, ambapo miaka ya leo hii tumefikia mahali ambapo ni alarming sana.

Nina maswali mawili ya kujiuliza:

(a) Ni wapi tulipokosea hadi tukajenga element mbovu hizo katika maisha yetu?

Nina imani hali ngumu ya uchumi iliyosababisha mapato halali ya wananchi kupungua vilisaidia kusababisha watu waanza kuachana na ethics za kazi kwa kutafuta rushwa, na kuanza kutumia nafasi za kazi zao kufanya biashara kinyume na masharti ya kazi. Lakini je kweli hiyo ndiyo iliyokuwa sababu pekee? Wizi wa mabilioni ya fedha za umma kweli ni kwa sababu ya hali ngumu ya uchumi?

(b) Je tufanye nini sasa ili kurekebisha makosa hayo?
 
Duuh! umeanzisha mjadala mzuri. Lakini leo wikendi nina mahangaiko kidogo. Nitarudi kuchangia, inshallah!
 
Duuh! umeanzisha mjadala mzuri. Lakini leo wikendi nina mahangaiko kidogo. Nitarudi kuchangia, inshallah!
Bila kutibu ugonjwa huo uliokwisha ingia vichwani mwa watanzania karibu wote, hata tukiletewa rais malaika Gabriel/Jibril, hatutakwenda popote. Ni lazima tuanza kupambana na hiyo changamoto ya tabia zetu kwanza ndipo tuangalie mbele.
 
Mkuu Kichuguu

(a) Hatujali kabisa ethics za kazi; nadhani hili linaeleweka sana.

Kuhusu hili mimi nadhani ujira mdogo wanaolipwa Wafanyakazi kwa kiasi kikubwa unachangia sana katika tatizo hili. Unakuta mshahara wa mtu unamtosheleza kwa siku labda 10 tu katika mwezi na siku nyingine 20 akili inamzunguka hajui ataishije ili kuweza kukidhi mahitaji yake muhimu kama yuko single au yale ya familia yake.

Kama kweli Watanzania tuna hulka ya uvivu inakuaje Watanzania waliozaliwa nchini, wakalelewa nchini na labda kufanya kazi nchini wanapopata nafasi ya kufanya kazi nchi za nje huwa ni Wafanyakazi hodari sana kiasi hata waajiri kuwasifia kwamba Watanzania ni wachapa kazi wazuri sana? Kwa maoni yangu hili la kulipwa ujira mdogo ni tatizo kubwa sana ambalo kwa asilimia kubwa linasababisha watu kutofanya kazi zao za kila siku kwa kujituma kama inavyostahili.
 
BAK

Si kila wakati ujira mdogo ndio sababu ya kuzembea kazini (angalia suala la Wabunge kuacha kikao cha Bunge la Bajeti kwenda promotion Kigoma).

Ninadhani ni kulelewa bila ya kuthaminishwa kazi. Hii linaanzia kwa wazazi na mashuleni.

Mtoto unamtuma, anafanya kazi uliyomtuma ila kwa kulipualipua na wewe mzazi wala humkosoi unaona "kheri imefanywa"
Anaondoka nayo tabia hiyo hadi kazini. Tunaona fahari na ujanja kuweza kufanyakazi nusu nusu
 
Last edited by a moderator:
BAK;

Chukulia mjadala huu katika mazingira ya nyumbani tukifuata mazingira ya nyumbani. Ni kweli tukishaenda nje ya nchi huwa tunafuata taratibu za huko: .....when in Rome, do as the Romans do.

Kama alivyosema Gaijin hapo juu, kuna watu wana mishahara mikubwa sana lakini bado hawana ethics za kazi kabisa. Chukulia mawaziri na wabunge wetu wanavyolipwa mishahara mikubwa sana lakini wengi wao hafuati ethics za kazi zao. Kitendo cha wabunge kupokea rushwa ili wapitishe mswada au waziri kupokea rushwa kwenye account huko Uswisi ili kuruhusus makampuni ya madini yaslipe kodi hakusababibishwi na mishahara midogo bali kunatokana na hulka yetu ambayo ndiyo mada ya thread hii.


Gaijin:

Je tabia ya kuheshimu ethics inaanzia nyumbani au inatokana na jamii? Iwapo hiyo ni kweli, je unaonaje point aliyosema BAK hapo juu kuwa tunapotoka kwenda kufanya kazi nje ya nchi huwa tunafanya kwa ufanisi sana? Ni nini kinachotubadilisha tuwapo nje ya nchi?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mi nadhani kila kitu kinatokana na impunity and lack of accountability. Tungekua tunachukua hatua nadhani watu wangejirekebisha. Asiefunzwa na wazazi atafunzwa na dunia, ikibidi atafunzwa na mahakama.

Tukizungumzia kuzama kwa meli (mfano) mtu mmoja anaweza kujiuzulu na jambo likaishia hapo, watu wanaridhika kua amewajibika. huo sio uwajibikaji. anae mfata ataendelea na system ile ile. Ikiwa kutakua na utafiti, na wale wote watakao onekana wana makosa ya action, omission or negligence wakafutwa kazi, wakapelekwa mahakamani na kufungwa, kulazimishwa kulipa faini, jina zao na picha zao kutangazwa ili tuwazomee, na serikali ikalipa familia ya majeruhi wote, utaona na system itabadilika, kila mtu atajitahidi kuhakikisha jangaa lile halitokei tena.

Binafsi ninapo kutana na muhudumu ambae ananionesha dharau fulani (au sifurahii service yake) najaribu kuongea na line manager wake na kumripoti. sometimes they do nothing, but sometimes they take action. ikiwa kila mtu atafanya hivo huenda tukawalazimisha service providers kua more professionals na kuwajibika kwa makosa yao. we need to enforce sanctions and accountability.
 
Mwali, nani anamuwajibisha nani sasa? Ikiwa mfumo mzima ni wa kizembezembe tu kuanzia juu kushuka chini? Huyo boss wangu tu hana nafasi ya kuniwajibisha manake hata yeye binafsi haji ofisini on time, anatembelewa na hawara kazini, lunch anaenda 3 hours?

Gaijin, chukulia mfano wa mtoa maamuzi kwenda mkutano Davos akiacha mgomo wa madaktari. Kurudi mkutanoni he is the hero kwa sababu kawaita madaktari, kachekacheka nao na wakaahirisha mgomo kwa muda!

Mfumo mzima unafanya kazi zisiende. Hata mwenye ethics zake za kazi anaharibiwa na mfumo uliopo. Say issue imejulikana for several months na inawekwa mezani kwako siku mbili kabla ya deadline. Unahitaji collaboration kutoka kwa watu mbalimbali. In the end lazma ulipue ili usilale nacho kidagaa!
 
Last edited by a moderator:
Mwali, nani anamuwajibisha nani sasa? Ikiwa mfumo mzima ni wa kizembezembe tu kuanzia juu kushuka chini? Huyo boss wangu tu hana nafasi ya kuniwajibisha manake hata yeye binafsi haji ofisini on time, anatembelewa na hawara kazini, lunch anaenda 3 hours?

Gaijin, chukulia mfano wa mtoa maamuzi kwenda mkutano Davos akiacha mgomo wa madaktari. Kurudi mkutanoni he is the hero kwa sababu kawaita madaktari, kachekacheka nao na wakaahirisha mgomo kwa muda!

Mfumo mzima unafanya kazi zisiende. Hata mwenye ethics zake za kazi anaharibiwa na mfumo uliopo. Say issue imejulikana for several months na inawekwa mezani kwako siku mbili kabla ya deadline. Unahitaji collaboration kutoka kwa watu mbalimbali. In the end lazma ulipue ili usilale nacho kidagaa!
King'asti; uliozungumza liko kwenye hiiyo tabia ya kutokuwa responsible na kukosa accountability; ni miongoni mwa tabia mbaya tulizo nazo ambazo ndiyo ninazotaka tutafute mbinu za kuachana nazo. rais kuacha kushugulikia matatizo ya muhimu ni kuwa irresposnsible, na vile vile inatokana na kuamani kuwa madaraka aliyo nayo ni haki yake (entitled) na wala hakuna wa kumwajibisha. Watu kusahahu na kushindwa kuzungumzia mambo ya muhimu kwa sababu ya kuchekewa ba rais ni kuwa irresponsible kwa kusindwa kumwajibisha rais anapokuwa hakufanya majukumu yake ipsavayo. Kuna vicious circle kubwa sana katika tabia zetu.
 
Last edited by a moderator:
Mi nadhani kila kitu kinatokana na impunity and lack of accountability. Tungekua tunachukua hatua nadhani watu wangejirekebisha. Asiefunzwa na wazazi atafunzwa na dunia, ikibidi atafunzwa na mahakama.
Mwali, huoni kuwa unarudia swali hilo hilo ninaloongelea? Kuwa hatuna tabia ya kujituma mpaka ama tulazimishwe kwa namna moja ama nyingine: ama kwa vitishomvya kufukuzwa kazi au kwa incetive ya kupata rushwa. Hilo ni gogor lile lile. Na kweli wengine wetu tunaweza kwenda kulalamika kwa wakuu wa vitengo, lakini je una uhakika gani kuwa mkuu wa kitengo huyo atakusikiliza ilhali wote tuna hulka hiyo hiyo? Unaweza ukamkuta naye yuko kwenye simu akiongelea upuuzi wa namna hiyo hiyo.
Tukizungumzia kuzama kwa meli (mfano) mtu mmoja anaweza kujiuzulu na jambo likaishia hapo, watu wanaridhika kua amewajibika. huo sio uwajibikaji. anae mfata ataendelea na system ile ile. Ikiwa kutakua na utafiti, na wale wote watakao onekana wana makosa ya action, omission or negligence wakafutwa kazi, wakapelekwa mahakamani na kufungwa, kulazimishwa kulipa faini, jina zao na picha zao kutangazwa ili tuwazomee, na serikali ikalipa familia ya majeruhi wote, utaona na system itabadilika, kila mtu atajitahidi kuhakikisha jangaa lile halitokei tena.
Huo utakuwa ni utaratibu mzuri, lakini ni nani atakayemkamata waziri na kumpeleka mahakamni iwapo tuna system ya watu wanaoogopa kuwawajibisha subordinates wao labda kutokana na ukweli kuwa anayeishi kwenye nyumba ya vioo huwa hapendi kurisha mawe.
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli hiyo ndiyo hukla yetu, je ni kwa nini tumejikuta hapa? na ni njia gani tunayoweza kufanya ili tung'oke kutoka kwenye dimbwi hili?

Hatua ya kwanza katika kujikomboa kutoka kwenye hili dimbwi ni kulikubali hilo pungufu. Hatua ya pili ni kulichukia kwa hasira na hisia zote. Hatua ya tatu ni kufanya kweli ili kujitoa.
 
Mkuu Kichuguu

(a) Hatujali kabisa ethics za kazi; nadhani hili linaeleweka sana.

Kuhusu hili mimi nadhani ujira mdogo wanaolipwa Wafanyakazi kwa kiasi kikubwa unachangia sana katika tatizo hili. Unakuta mshahara wa mtu unamtosheleza kwa siku labda 10 tu katika mwezi na siku nyingine 20 akili inamzunguka hajui ataishije ili kuweza kukidhi mahitaji yake muhimu kama yuko single au yale ya familia yake.

na hii ndio manaa inaonekana kama vile wafanyakazi wa serilaki wana mgomo baridi. Mshahara mdogo, watu wana ripoti kazini then wanapotea na mambo yao. Serikali inawakopa wafanyakazi, na wafanyakazi hawatekelezi wajibu wao.

Tunahitaji ku overall civil servants. Ongeza mishahara kwa wafanyakazi, sheria za kazi zisimamiwe na tuache mambo ya hivyo hovyo

na ndio manaa inaonekana kama vile wafanyakazi wa serikali wana mgomo baridi. Mshahara mdogo, wana ripoti kazini then wanapotea na mambo yao. Serikali inawakopa wafanyakazi, na wafanyakazi hawatekelezi wajibu wao.

Tunahitaji ku overall civil servants. Ongeza mishahara kwa wafanyakazi, sheria za kazi zisimamiwe na tuache mambo ya hivyo hovyo
 
Ndivyo tulivyo.

Hii ni results ya colonial hangover, tabia ya kutothamini vitu vya uma.
Serikali nayo inatoa majibu mepesi mepesi kwa masali ya wafanyakazi.
Angalia wafanyakazi wa Vodacom na Airtel, hakuna uze,mbe kazini, watu wanafanya kazi hadi wanataka kufia kazini.
Institutions zote hazifanya kazi inavyotakiwa.
Hali yako ni kama favor.
Mfanyakazi wa mahakama anajiona kama anafanya kazi kwenye ubalozi wa marekeni....
 
Kichuguu,
Ndivyo Tulivyo inaambatana na ulemavu wa UTU kutokana na Umaskini, Ujinga na Maradhi..Hao wote walioendelea ukitazma kwa makini wamepigab hatua kubwa sana kuondoa kwanza maadui hao ktk jamii zao. Hata tukisema Kenya wao wamesoma kuliko sisi, sii maskini kama sisi na poengine naweza sema hata vifo ni vichache zaidi kwa sababu unapoondoa Ujinga na umaskini hata maradhi na vifo pia hupungua..

Sisi kwa kuacha vita yetu, tumeingia ktk Ubepari bila Mtaji isipookuwa Kiburi, kile kiburi cha maskini jeuri na ndi maana hata tunapoomba msaada husema huwezi kunipangia nitaufanyia nini, wewe kama unanipa nipe halafu mimi nitajua la kufanya kama vile msaada ni sadaka au Zaka. Na kwa ujinga ule ule hufikiria neno MSAADA ni lina maana unapewa bure na hudaiwi wala hauna riba.

Kwa Umaskini na Ujinga tulokuja nao ktk Ubepari tumejikuta sisi wenyewe ni virusi vya maendeleo yetu wenyewe. Hatuwezi kuwa na Ethics mkuu wangu haiwezekani. Umaksini wetu ndio adui wa maendeleo yetu wenyewe. hatukurogwa wala kurudishwa nyuma zaidi ya sisi wenyewe kushindwa kujipanga kuweka mfumo bora zaidi ktk kuhakikisha Umaskini, Ujinga na maradhi vinaangamizwa..

Na Unapokuwa na kilema hicho ustaarabu nao unatoweka.. Nimeshatoa mfano zamani ya kwamba Jaribu siku moja weka makundi mawili ya watu. Kundi la kwanza wapange mezani kila mtu na sahani yake ale kwa kisu na uma, halafu kundi la pili wamwagie sinia la biriani mkekani halafu uone tofauti ya jinsi watu hawa watakavyo behave ktk chakula.
Wa mkekani hawataweza kula na uma na kisu wala hata kijiko maana it's about speed, quantity na shibe..Wa mezani wakaweka ustaarabu fulani na pengine hata kuwacheka walioko mkekani, lakini hata yule mtu alokuwa mezani jana ukimweka mkekani kesho utamwona akigombania nyama na yule wa mkekani ukimweka mezani utamwona akibadilika.

Hivyo mimi na wewe mkuu wangu tumekuja huku mezani umebadilika na kuwa na ustaarabu fulani lakini tukikumwaga Bongo tu haitachukua miezi sita wewe mwenyewe utaanza kugombania biriani.. lazima utatia akili..

Uchumi wa nchi za kiafrika ni sawa kabisa na sinia la mkekani, hatukufanya maandalizi ya mageuzi ktk mfumo wa kiuchumi kwa kutazama kwanza WATU na MAZINGIRA tulokuwepo ila tuliiga tu Ubepari wa nchi za Ulaya.. Huweiz chukua watu wmaskini, wajinga na wenye matatizo makubwa ya kifaya ukawapachika mfumo wa Ulaya.. Sisi tulipigania Uhuru lakini tulichopewa ni Demokrasia hatua ambayo haikulingana na mazingira yetu..Hivyo kwetu sisi maskini hata hata kama tukiacha biriani tukawekewa vianzi vya mbatata (Fries) na kuku bado watagombania. Na yule ulomweka(msomi) Jikoni atajiona yeye ndio mwenye shughuli, mpishi na mgawaji chakula na bila shaka ataona ni haki yake kuacha chakula kingine pembeni abebe nyumbani kwake baada ya shughuli mbali kabisa na malipo alopewa.

Kwa Umaskini, Ujinga na maradhi, usitegemee kabisa kwamba kuna kujituma hapa. Sisi wote ni waaliwka tu ktk dunia hii ya demokrasia maana hatujui kilichopikwa. Zamani tulikuwa tukisisitiza zaidi Kilimo na kusema ndio uti wa mgongo, Tukipambana na Umaskini, Ujinga na maradhi lakini badala yake tukaletewa Demokrasia na ndio ikawa vita yetu kwa sababu Ulaya ndio wanachopigania na wachosisitiza. Sasa wewe nambie kwa Mtanzania maskini, mjinga na mwenye afya mbovu hii demokrasia itamsaidia nini zaidi?..Yet ukiwauliza watu wengi sasa hivi kila mtu atakwambia Demokrasia, demokrasia kaa vile UTU wa binadamu aumaendeleo ya Mtanzania yatathaminika kwa Demokrasia..

Kwa kumalizia tu ni kwamba sisi tupo ktk mfumo mbaya usolingana na WATU wala MAZINGIRA yetu..Tumeacha maadui wetu na kuvamia maadui wa nchi za magharibi na ndio maana hadi leo sisi bado ni watumwa wa kimfumo. Umaskini hautakwisha na wala Ujinga hautakwisha kkutokana na kwamba sisi tuna maradhi tofauti kabisa.. Tunaumwa Malaria wanatupa dawa za mafua kwa sababu tu mafua inaua watu wengi Ulaya nasi tumeweka vituo na karantini za matibabu ya mafua - Tutapona wapi?..
 
Kwa watu walioshi miaka ya sitini na ile ya sabini wakati bado kuna siasa za Ujamaa na Kujitegemea, mtakubaliana nami kuwa mambo hayo hayakuwamo miongoni mwa jamii yetu. Yalianza kukua kidogo kidogo mwanzoni mwa miaka ya themanini baada ya vita, na yakaua kwa kasi sana kuanzia mwishoni mwa miaka hiyo ya themanini, ambapo miaka ya leo hii tumefikia mahali ambapo ni alarming sana.
Baada ya vita ndio hasa mambo yalipoanza kuharibika kwa ile sera ya "Tufunge mkanda". Tuliahidiwa kuwa hali hiyo itakuwa ya muda wa miezi 18 tu. Masikini Watanzania siye tukaamini. Miezi 18 ikapita, miaka 18...28 hadi sasa ni miaka 34. Bado tunaambiwa "kuweni wavumilivu, hali ngumu ya uchumi si Tanzania tu, tupeni muda, tumeanza kuyashughulikia, mikakati kabambe imeanza, uchambuzi yakinifu utafanyika....." Wakati sisi tulianza na kufunga mikanda hadi tumeishia kuzuwia suruali kwa kamba ya mgomba , viongozi wetu mikanda yao imemaliza tundu wanatoboa nyengine; ufanisi utakuja wapi?

Nadhani cha kufanya ni kufumua mfumo huu mzima uliooza na kuanza upya. Tupate viongozi wazalendo, sio watawala na wanyapara tulionao sasa.

Tusijidanganye Watanzania na tusijipe matumaini ya upofu; matatizo tuliyonayo hayataisha kwa kubadilisha mawaziri, makatibu wakuu na wakurugenzi tu; wala hayatakuja kuisha kwa kuioondoa CCM madarakni tu. Tunahitaji sote kama taifa, kama kitu kimoja kubadilika kimawazo na kifikra, fikra zilizooza kwa miaka 50. Tunahitaji uadilifu, tangu wa viongozi hadi wa wanaoongozwa.
 
Mkandara umetoa jibu zuri sana na la kina; unaloongea ni kama vile mtu aliyekuwa anapanda mlimani kutafuta asali halafu kabla hajafika huko mlimani akaona ndani ya shimo kuna maji ya taka yanayoonekana kama asali huku yakiwa yamezingirwa na nzi walioonekana kama nyuki, basi yeye bila kuwa makini kujiuliza kama kweli ile ni asali akaamua kujirusha humo kwenye shimo la taka bila ya kuwa na ngazi na hivi sasa amebaki hana asali na wala hawezi kujitoa humo shimoni mpaka apatikane mtu wa kumletea ngazi. Swali sasa ni wapi tutapata ngazi ya kututolea huko shimoni kwenye maji machafu tulikojitupa tukidhani ni asali? Kwa maana nyingine ya swali langu hili ni kuwa, je tutapambanaje na hao maadui wa wakuu wakati tumeshajiweka katika mazingira ambayo ni vigumu tena kupambana nayo?

Asilimia 90 ya watoto wetu hawapati elimu nzuri ya kuwafanya waone mambo kwa kina, na hao ndiyo generation ya kesho: kwa hiyo adui ujinga anazidi kukua. Huduma za afya ndiyo hivyo tena, tuliowapa mamlaka ya kuteletea huduma za afya nzuri wao wanatibiwa nje ya nchi na kutuacha tukiwa hatuna huduma zozote; na mbaya zaidi wanatufukuzia hata waganga wetu tubaki bila kuwa na waganga. Ardhi yenye raslimali yote imeuzwa na viongozi wetu kwa wageni, na kutuacha sisi bila chochote; hivyo kuzidi kututumbukiza kwenye dimbwi la umaskini. Bila elimu, tukikabiliwa na maradhi na kuzungukwa na umaskini, ni kweli kuwa wengi wetu tunakuwa hatuni mambo kwa mbali na kila mara tunakuwa tunafanya kazi kwa ajili ya kesho tu.

Kwa vile matatizo haya hayawahusu viongozi wetu, wamekuwa hawayashughulikii kutokana na tabia hizo hizo nilzosema hapo juu: wao wanajiskia kuwa wako entitled kila kitu kizuri, hawawabijiki kwetu, na wala hawalazamiki kufanya kazi zao kama inavyotakiwa, na hatuwachukulii hatua yoyote.
 
.............
Nadhani cha kufanya ni kufumua mfumo huu mzima uliooza na kuanza upya. Tupate viongozi wazalendo, sio watawala na wanyapara tulionao sasa. ......................
MAMMAMIA
..................hilo haswa ndilo jawabu, lakini je wazalendo hao tutawatoa wapi iwapo wote wameshaharibika? Kumbuka kuwa unahitaji kuondoa karibu mahakimu wote, polisi wote, wanajeshi wote, watumishi wa serikali karibu wote.
 
Last edited by a moderator:
na hii ndio manaa inaonekana kama vile wafanyakazi wa serilaki wana mgomo baridi. Mshahara mdogo, watu wana ripoti kazini then wanapotea na mambo yao. Serikali inawakopa wafanyakazi, na wafanyakazi hawatekelezi wajibu wao.

Tunahitaji ku overall civil servants. Ongeza mishahara kwa wafanyakazi, sheria za kazi zisimamiwe na tuache mambo ya hivyo hovyo

Je unajua kuwa kuna watumishi wa serikali wenye mishahara mikubwa sana lakini utendaji wao umejaa rushwa tu?
 
Back
Top Bottom