Watanzania hawapendi maandamano au hawajui haki zao?

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
670
Achana na maandamano ya CHADEMA, miaka kadhaa iliyopita kulikuwa na maandamano ya wamachinga. Mtu mmoja ambaye alitajwa kuwa msemaji wa wamachinga alirekodiwa akiwataka watu wengine wasiandamane kwa kuwa wakivunjwa miguu watakaoathirika ni wao na sio walioandaa maandamano.

Nilipoona video ile nikaona ni mtu anayekataa kudai haki zake kwa kuwa anaona si haki yake kudai haki yake. Yaani hana sauti lakini hataki kutumia namna zinazotambulika kupaza sauti yake. Akisema kuna kuvunjwa miguu, maana yake alikuwa anaona ni haki kwa polisi kuwapiga badala ya kuwalinda ili sauti zao zifike mbali.

Hiyo si mara ya kwanza kwa wananchi kuonesha kuwa hawako tayari kutumia haki zao kupaza sauti zao. Mwaka jana kama nakumbuka, kulikuwa na ugomvi kwenye mziki wa kizazi kipya kati ya wakenya na watanzania. Mimi ni mtanzania lakini ile diss track ya "Bongo Favor" aliyoandika Kaligraph Jones ilikuwa na ujumbe maridhawa kwa wasanii wa Tanzania. Hata hivyo wasanii wa Tanzania wakawa wanai-diss Kenya "Eti wamezoea kuandamana". Yaani kupitia musiki msanii anawaona wanaotumia haki yao wanakosea. Hii ilinipa maswali sana kwa watu wanajiona wako-consicous kushindwa kutambua haki zao za msingi kiasi cha kuwadiss wanaosimamia haki hizo.

Suala hili halijaishia hapo, hivi karibuni, kumekuwa na maandamano ya CHADEMA miji mbalimbali, ni maandamano ya amani. Lakini kinaibuka chombo kudhihaki maandamano hayo. Najiuliza kama kweli wananchi wote wamelewa kwa kuamini wao ni serikali au ni kweli wananchi hawataki kupaza sauti zao kupitia maandamano.

Nawaza kama maandamano hayahitajiki, mbona sioni watu kudhihaki maandamano ya kusapoti vitu mbalimbali. Je wananchi hawaoni wanaongea ugumu kwenye maandamano ambayo yanalenga kudai haki? Haki ni tofauti na maandamano ya kusifia au kusapoti kitu.

Inakuwaje wananchi wanakubali kuzuiwa maandamano ya kudai haki kuziwa lakini hawahoji maandamano ya kusifu hayazuiwi. Je ni sahihi kuzuiwa kudai haki.?

Mbali na yote najua wananchi wana ujinga mwingi kuliko uwezo wakuchanganua mambo, hivyo ni wito kwa asasi za kiraia za kutetea haki za raia kufanya jambo kwa watu hawa ili kuongeza ufahamu. Fuatilia makala zangu za awali kuhusu elimu ya uraia
 
Back
Top Bottom