Tulia, Prof. Kitila, Chongolo, Prof. Kabudi jibuni hoja za Kijana Mzalendo mkataba wa Bandari

Shakari

Senior Member
Jul 6, 2022
157
440
Kijana Mzalendo, David Levi Nkindikwa amekuja na uchambuzi wa hoja lukuki zikihusisha matashi ya Spika wa Bunge Tulia, Prof Mkumbo, Katibu Mkuu Chongolo kuhusu mkataba wa Bandari uchambuzi ambao umesambaa katika mitandao mbalimbali ikiwemo JF.

Lakini amehoji kuhusu ukimya wa Baba wa Mikataba Prof. Kabudi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusiana na Mkataba wa Bandari.

Viongozi hao wote tunaomba mjitokeze hadharani mjibu hoja za Kijana Mzalendo.

Tulia-Ackson.jpg

Tulia Ackson

20200312_102711_UNIT_PHOTO_18_CUSTOM_PAGE_Prof. Kitila A.K.Mkumbo.jpg

Kitila Mkumbo

download.jpg

Daniel Chongolo

pic-kabudi.jpg

Baba wa Mikataba, Prof. Kabudi

d3d3edff295778ac3f1ba8b1d9fb855b.jpeg

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Feleshi
 
Hawatumii akili wanatumia matumbo yao kujibu chochote kinachohusiana na Huu mkataba.Ni wapumbavu tu waliobahatika kupita darasani kukusanya vyeti lakin wote hao akil hakuna hata 1
 
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Kijana Mzalendo, David Levi Nkindikwa amekuja na uchambuzi wa hoja lukuki zikihusisha matashi ya Spika wa Bunge Tulia, Prof Mkumbo, Katibu Mkuu Chongolo kuhusu mkataba wa Bandari uchambuzi ambao umesambaa katika mitandao mbalimbali ikiwemo JF.

Lakini amehoji kuhusu ukimya wa Baba wa Mikataba Prof. Kabudi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusiana na Mkataba wa Bandari.

Viongozi hao wote tunaomba mjitokeze hadharani mjibu hoja za Kijana Mzalendo.

View attachment 2696888
Tulia Ackson

View attachment 2696900
Kitila Mkumbo

View attachment 2696901
Daniel Chongolo

View attachment 2696902
Baba wa Mikataba, Prof. Kabudi

View attachment 2696903
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Feleshi
MAZINGIRA YENYE UTATA KUHUSU MKATABA WA BANDARI

Kuna mazingira yenye utata mkubwa na yanayoibua hisia na maswali mengi kutoka hatua ya MoU, kusainiwa na kuridhiwa kwa mkataba huu wa IGA, nitaongelea vipengele vitano kama ifuatavyo.

(a) Kampeni za wazi, Spika wa Bunge kuandaa ziara mwezi Februari 2023 ya wabunge 60 kutembelea maeneo ambayo DP World amewekeza na maeneo mengine Duniani ili kujifunza uwekezaji wa sekta binafsi katika uendeshaji wa bandari. Zoezi hili lilifanyika wakati mkataba haujatangazwa wala kufahamika kwa wananchi na wabunge wenyewe lakini pia ziara hiyo inatuhumiwa na wananchi kugubikwa na rushwa kubwa ili kulishawishi
Bunge kuipa upendeleo Kampuni ya DP World.

(b)Baadhi ya Viongozi na watendaji wa Nafasi za juu serikalini kuondolewa kwenye Nafasi zao bila Maelezo yoyote akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari, Eric Hamis aliondolewa tarehe 4/7/2022, Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Katanga na Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa, Kamishna Diwani Athumani ambao waliondolewa kwa pamoja tarehe 3/1/2023. Viongozi wote hawa waliondolewa ndani ya kipindi cha
mchakato wa MoU na Kuridhiwa kwa mkataba huu na Bunge.

(c) Kuchukua kipindi kirefu cha miezi 8 kuingia Mkataba tangu kusainiwa MoU na katika kipindi hicho Serikali haikufanya tathmini wala feasibility study kujua mahitaji na manufaa ya mradi.

(d)Kutangaza kufanyia marekebisho ya Sheria ya Manunuzi na Sheria za Ulinzi wa Rasilimali kabla ya kuingia Mikataba ya HGAs baina ya TPA na DP World.

(e) Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Mbarawa na timu ya Serikali ya majadiliano kuendelea kutoa Ufafanuzi wa Mkataba wa IGA badala ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Jaji Dk. Eliezer Mbuki Feleshi na Baba wa Mikataba na Baba Negotiation, Mhe. Profesa Palamagamba Aidan Mwaluko Kabudi. Viongozi hawa wamekaa kimya badala ya kujitokeza hadharani wawaeleze watanzania ukimya wao unasukumwa na nini?

Back
Top Bottom