Haswaa! Na hilo jina la Tyson linatokana na huo mnyukano wa kisiasa, kwani bila ubabe asingepata ubunge kwa chama cha upinzani miaka hiyo.
Mkuu acha kuchekesha watu,kweli jamaa ni 'handsome' wa kijiji.

Hapana, lile jina kalipata kutokana na SURA YAKE TATA!
Tyson nae alibwagwa ndo akakimbilia NCCR au?
inachokumbuka atu ni kuwa aliwahi kwenda NCCR.Ubunge......?Tyson unamaanisha Stephen Wassira??, aliwahi kuwa mbunge kupitia upinzani huyu?? Historia zetu wengine ni fupi kidogo!!!

Hapana, lile jina kalipata kutokana na SURA YAKE TATA!

HAKUNA HUYU DINGI ALISHAMKATA MAKOFI MSAIDIZI WAKE NDO WAKAMWITA TYSON! ILA NI HANDSOMEEE,MWENYE PICHA YA MWANAWE NA MY WIFE WAKE NAOMBA AWEKE TUWAONE NA WAO
Huyu bwana alimsurubu sana Mbowe miaka ile. Ajabu, alipopigwa chini kura za maoni 2005 kwenye chama lao la magamba akataka kuchepukia CDM. Sijui baadaye aliishia wapi!
Fedastus Limbu 1995 NCCR Magu mjini
Mpesya 2010 mbeya mjini
Nicas Mahinda. Soon tunategemea kuongeza Edward Lowasa na Andrew Chenge..
Mateo Qares aliangushwa kwao Babati na wala sio Rufiji;alichokwa kwao kwa kauli zake za kukera kwa wapiga kura hasa walipomuomba akiwa Mbunge 1990 awatafutie soko la vitunguu na yy kuwajibu kuwa "wakikosa soko waunge vitunguu vyote kwenye mboga zao";Aliyeangushwa Rufiji ni Waziri Mbonde baada ya kuingia Prof Mtulia;nipo tayari kukosolewa anyway!LKN swahiba wake mkuu Mkapa akamkumbuka kwa kumpa RC-Mbeya;kwa sasa sijui yupo wapi jamaa huyu machachari
Hii huenda ni sahihi kabisa.

. Baada ya kusoma thread zote ambazo zinaelezea kwa nini Wassira anaitwa Tyson nimepata picha kweli kuna upotoshaji mkubwa na watu wanapost tu vitu wasivyovijua. Hii inaonyesha wengi ni watoto hamjui hata hata source ya jina hilo na kinachofuata hapa ni ubishani na kujaza kurasa za JF zisizokuwa na maana. Ukweli ni kwamba Wassira aliwahi kuhamia NCCR-Magaeuzi baada ya kubwagwa kwenye uchaguzi miaka ya 1995, na alivyohamia mwandishi wa habari wa gazeti la Majira siku moja alimuuliza maswali, kwa muujibu wa Wassira alidai yalikuwa mwaswali ya maudhi. Wassira alimnasa vibao. Kesho yake gazeti la majira lilikuwa na headline iliyosomeka "TYSON WASSIRA AMPIGA MAKOFI MWANDISHI WA HABARI". Kuanzia hapo ndio alibatizwa hilo jina.Natoa ushauri kama mtu hujui kitu wakati mwingine bora uwe msomaji tu, kuliko kupoteza nguvu zako kuposha watu ndani hili jamvi.