Tujadili ukweli wa Mixtape ya Antivirus ya Sugu na wenzake

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,237
103,894


Kwa tuliokuwa tunafuatilia kwa karibu Hip Hop ya Bongo tunaikumbuka vizuri Mixtape ya Antivirus. Hii ni mixtape iliyokuwa engineered na Joseph Sugu na wenzake wakiwepo Mapacha, Rado na wengine. Wakati tukiwa Chuo Rado alikuwa mwenetu na mara kadhaa alitutembelea getto. Siku moja mwenetu akaja na CD kwa mara ya kwanza tukaskiza dissing tracks za kiwango cha juu sana. Pamoja na kufahamu ubeberu wa Clouds Media lakini jamaa walifanya deep sana. Waliweka kumbukumbu za vizazi.

Nyimbo ya I Wanna Kill U unaopatikana kwenye mixtape hiyo ulipelekea Sugu kuitwa na kuhojiwa na polisi. Pamoja na mistari ya nyimbo hiyo kuwa mikali kidogo, lakini je, ni kweli kuwa Sugu anataka kuua au ni utundu tu wa mashairi? Hapana ilikuwa ni kufikisha ujumbe tu.

Mixtape hii iliibua hoja kadhaa, moja ikiwa ya uhusiano kati ya redio na wasanii, pamoja na nafasi ya redio katika kukuza sanaa na hata nafasi ya redio kuuwa sanaa. Clouds ilitajwa kuwa ni media yenye upendeleo.

Pamoja na yote, mashairi ya Sugu na wenzake katika mixtape hii yaliweza kuangaliwa katika pande mbili. Pande ya kwanza, ni kuwa mashairi yao yanachochea chuki na hata kuleta fujo. Pande ya pili, ni kuwa mashairi yao yanaongea ukweli mtupu, na lugha kali waliyotumia ni kutokana na kuchoshwa na unyonyaji katika sanaa ya bongo flava.

Inawezekana pia Sugu aliamua kujitoa muhanga na kutuonesha roho ya udhubutu, kwani Watanzania tuna sifa ya kukubali yaishe. Je,ni kweli Sugu ndio alituonesha njia, kama Bob Marley alivyoimba Get Up Stand Up.

Swali, je Mixtape ya Antivirus ilitetea muziki wa bongo flava dhidi ya wachache waliouyumbisha au ilitaka kuchochea fujo zinazotokana na chuki kibinafsi?
 
Baada ya Antivirus kutoka ruge alienda kumshitaki sugu kwamba sugu amemtishia kumuua !

So polisi wakamkamata sugu, kwenye mahojiano na polisi sugu akawaambia polisi waangalie kwenye dictionary maana ya kill ni nini? Kumbe hta kuondoa inaweza kutumika neno "kill"...kwa hiyo ikabidi polisi wamwachie sugu bila ya kupenda maana hakuwa amevunja sheria yoyote.
 
Back
Top Bottom