Tuitizame hii hotuba - Part One

mh sikio la kufa ama kweli halisikii dawa,wanajipambanua wenyewe uchi wa fikra zao nba uduni wa sera zao.Mwanafalsafa mmoja aliwahi kusema heri uchi wa nyama kuliko uchi wa akili,hii sasa too much mh!Hivi mwalimu JK Nyerere aliondoka na na kila kitu ndani ya CCM?Inawezekana hakuacha kitu pale kuanzia busara,sera nzuri,uzalendo,imani na upendo ndani ya CCM.Ukiona mtu mzima anasimama mbele ya kadamnasi huku anatoa lugha chafu mbele ya watoto na wazee ujue kama si chizi basi anaelekea kuokota makopo.

Uchakavu huu wa fikra uana sababishwa na nini hasa mpaka mtu unatoa uchafu ambao hakustahili kupitia mdomoni.Mbaya sana amezungukwa na wazee tena wengine ni viongozi wanaojipambanua ni wapamabanaji wa ufisadiili hali wana cheza kijamaa huku wakiimba kibepari.Sipendi kuamin kama mchawi aliye waroga yupo hai.Shime wana wa Arumeru ni wakati wenu sasa kuchagua chua na mchele,sera zimemwaga,kama mnataka matusi CCM ndo hiyo na kama mnataka mabadiliko ya kweli dhidi ya madhalimu ndon wakati wenu kumchagua mgombea toka CDM.

Sera bila matusi zinawezekana na Tanzania yenye neema isiyo na mafisadi inawezekana.Kama kasi zaidi,nguvu zaidi na speed zaidi zimekita katika matusi tutegemee taifa la matusi na sera za halijojo.Na kama ndo mbuzi wa bwana ALLY amekula mahindi katika shamaba la bwana Ally basi tunapo elekea ni nusura ya maulana tu ndo itakuwa suluhisho la maadili mema ndani ya jamii yetu.Pole sana wana Arumeru,yaelekea ndani ya miaka hamsini mlipungukiwa matusi ndo maana sera ya matusi inachukua nafasi yake.
 
Jamaa anaitwa Livingstone Lusinde , ni mbunge wa mtera, kama tovuti ya bunge iko sawa basi amesoma jumla miaka nane, kasoma dara la kwanza hadi la saba halafu akasoma pale dodoma chuo cha ccm mwaka mmoja

haaa! Haaa! Mkuu umeniacha hoi, kumbe dogo ni mweupe kichwani. Ndo maana snitch kweli kweli.
 
Duh! Huyo dogo ana matatizo ya ubongo, aliwahi kusema wabunge wapimwe akili huyu haina haja ya kupima. Huyu ni mmbovu moja kwa moja.
 
Mungu wangu hivi,arumeru mmeenda kuaribu maadali na kufundisha watoto matusi.huu ni ujinga uliyopitiliza kama mmeishiwa hoja nyamazeni
 
CCM oyeee Oyeeee!

Mh mwenyekiti wa chama, waheshimiwa
viongozi wenzangu na wanachama wenzangu, nataka nianze kutofautiana hapahapa jukwaani na wenzangu, habari ya sisi kutukanwa halafu tunasema sisi hatutukani hatufanyi kazi ya kanisa hapa, kudadadeeeki matusi yakija nitatukana hoja zikija nitasema, potelea mbali

CCM oyeeeee.......oyeeee!

Jamani eti nae anajiita kiongozi, ni kiongozi gani huyu na anawaongoza watu gani? hivi hana watoto au wazazi? anaiga misemo ya akina Joti na mpoki? yaani sikuamini kama mtu mzima anapanda jukwaani kutukana vile.
 
Ni kweli hii hotuba mtoa mada hasemi uongo Mungu ndio shahidi wa hili. Halafu kuna mengine mi mwenyewe nliyasikia. Jamaa anasema " kama wewe ni mwanachama wa chadema uko hapa ukijifanya mjanja tutazaa na wewe" mara Nasari anasema ana uchungu na wananchi wa arumeru jamaa linasema " ana uchungu kwa sababu ana mimba ya sioi" nilikasirika nkataka nimpasue sema FFU wanayalinda haya mahuni.
 
Haya sasa wana wa Arumeru Mashariki kazi kwenu sasa hapo 1.4.2012 kuchagua pumba ni zipi na mchele ni upi. Kwa kuwa mpaka sasa sijasikia hatua yeyote aliyochukuliwa kwa ukiukwaji wa maadili ya kampeni ya uchaguzi aliofanya, basi kwa kuanzia mpeni adhabu ya kwanza anayostahili hapo 1.4.2012 kwa kumtosa mgombea wa chama chake kilichomlipia nauli kuja Arumeru kutoka Dodoma na kumlipa posho ya kujikimu kwa siku zote akiwa Arumeru akifanya kazi hiyo ya kutoa matusi!
 
Kwangu mimi, kadiri wanavyozidi kubanwa na CHADEMA na kukutaliwa na wananchi kunapojidhirisha wazi, ndivyo wanavyozidi kupanic na kutoa matusi...wamekabiliwa na msongo wa mawazo kwa kipindi kirefu pasipo kutafuta tiba muafaka ,sasa wanaugua ugonjwa wa akili.Matokeo yake sasa hawazisumbui tena akili zao kufikiri ..wala hawajali mbinu wazotumia kusaka kura..Nani ,kama yupo,awaeleze watu hawa wajirekebishe, ikiwa kila mmoja ndani ya CCM ni mtaalamu wa mikakati ya siasa .Hata wale ambao hawakupaswa kuongoza eneo lolote isipokuwa familia zao, sasa ndio wanaounda kamati ya ufundi ya kampeni za chama.
Kwa muda sasa,maandishi yamekuwa dhahiri ukutani, lakini kwa kuzoea mvinyo wa utawala,wamemeviza uwezo wao wa kuelewa kilichoandikwa.
Kwa kuwa,kimaadili wananchi hawapendi kusikia matusi,Wana Arumeru, kwa niaba ya watanzania, wamejitolea kuonyesha kwa vitendo chuki yao dhidi ya ukosefu wa staha, utu na heshima ulioonyeshwa na watu wanaopenda kuvalia mavazi nadhifu ya kijani na suruali nyeusi na waliolewa fikra za kutawala milele vichwani mwao.
Toto hili CCM ,kwa kuonyesha utovu mkubwa wa nidhamu, inapendekezwa lipewe suspension kama adhabu.Kwa utukutu wake,linaitwa na wananchi wa Arumeru,likiwa na wazazi ,ndugu,wapambe,wafurukutwa ,jamaa na marafiki zake ,kwenda kuchukua barua ya kusimamishwa masomo ,kwa muda usiojulikana tarehe 1 April.
 
Nilishtuka niliposikiliza maneno ya Mh. Lusinde kweli nasema ndiye game changer katika uchaguzi huu. Yaani ama CCM itamlaumu kwa kusababisha kushindwa au itamsifu kwa kusababisha kushinda. Factor kubwa hakika ni speech ya Lusinde.
 
hii itanishangaza sana, itaniambia ni nyuma kiasi gani wana arumeru wapo, itaniambia ni kazi kubwa kiasi gani mbele yetu ipo
 
Kwangu mimi, kadiri wanavyozidi kubanwa na CHADEMA na kukutaliwa na wananchi kunapojidhirisha wazi, ndivyo wanavyozidi kupanic na kutoa matusi...wamekabiliwa na msongo wa mawazo kwa kipindi kirefu pasipo kutafuta tiba muafaka ,sasa wanaugua ugonjwa wa akili.Matokeo yake sasa hawazisumbui tena akili zao kufikiri ..wala hawajali mbinu wazotumia kusaka kura..Nani ,kama yupo,awaeleze watu hawa wajirekebishe, ikiwa kila mmoja ndani ya CCM ni mtaalamu wa mikakati ya siasa .Hata wale ambao hawakupaswa kuongoza eneo lolote isipokuwa familia zao, sasa ndio wanaounda kamati ya ufundi ya kampeni za chama.
Kwa muda sasa,maandishi yamekuwa dhahiri ukutani, lakini kwa kuzoea mvinyo wa utawala,wamemeviza uwezo wao wa kuelewa kilichoandikwa.
Kwa kuwa,kimaadili wananchi hawapendi kusikia matusi,Wana Arumeru, kwa niaba ya watanzania, wamejitolea kuonyesha kwa vitendo chuki yao dhidi ya ukosefu wa staha, utu na heshima ulioonyeshwa na watu wanaopenda kuvalia mavazi nadhifu ya kijani na suruali nyeusi na waliolewa fikra za kutawala milele vichwani mwao.
Toto hili CCM ,kwa kuonyesha utovu mkubwa wa nidhamu, inapendekezwa lipewe suspension kama adhabu.Kwa utukutu wake,linaitwa na wananchi wa Arumeru,likiwa na wazazi ,ndugu,wapambe,wafurukutwa ,jamaa na marafiki zake ,kwenda kuchukua barua ya kusimamishwa masomo ,kwa muda usiojulikana tarehe 1 April.

Mkuu you made my day!!

Your Post? It was a very meaningful and logical!

I also share the same view concerning your signature!

Lets Conquer HOFU na WOGA for true human development!!
 
Lazima utakuwa na matatizo kichwani, au pengine tumbo linakupelekesha. Hakuna mtu wa kawaida anayeweza kushabikia matusi. Una mapungufu sana !!!!!!
hiyo ndio siasa. Katika uchaguzi mkuu wa 2010 jimbo la Kigamboni mgombea mmoja asiye wa CCM alimtukana matusi mazito mgombea urais kupitia tiketi ya CCM mwaka huo. CDM wakishindwa uchaguzi Arumeru wafungue mashtaka mahakamani ya udhalilishaji wa kijinsia na utumiaji maneno ya uchochezi.
 
Sometimes people are mad and some are always mad! Sijaona sera iliyotamkwa hapo ili wananchi wavutiwe wamchague Sioi. Au mi ndo sielewi sera ya uchaguzi wa Arumeru Mash ni matusi!!!! (If legal action can take place immediately, please)
 
Yani hapo kajiandaa wiki nzima kutamka hayo,Je kama asingejiandaa si angeanza kutukana wakwe zake na hata Mwenyekiti wake wa ...matusi ya nguoni kabisa. NAFIKIRI YUPO DODOMA NA HOSPITALI YA MILEMBE NAYO IPO DODOMA HAHITAJI NAULI KWENDA AU KUPELEKWA.
 
Back
Top Bottom