Tuheshimiane

Kitty Galore

JF-Expert Member
May 24, 2011
345
100
Wewe tumefahamiana katika mazingira ya kistaarabu, tumezoeana kama binadamu wengine bila kuvuka mipaka, najua umeoa ila mimi hujui status yangu kama nimeolewa au niko single, kutokana na kwamba haikuhusu, sasa kinachokufanya unipigie simu saa 5 kasoro 7 usiku ni nini? wakati hata huo mchana huna la maana la kuniambia? Najuta kukupa namba yangu, kama matumizi yako ya simu ndo haya. Wanaume wengine mnakera sana
 
Wasilianeni kwa pm. Habari za kupeana namba zinaleta uzushi uzushi tu.
 
alikuwa anakusalimia tu jamani!..kwa hiyo kama hukataka akupigie simu umempa namba ya nini?acha hizo bana.au kosa hakutuma ile vocha(natania).mia
 
Haujui siku hizi kuanzia 4-1 asubuhi tigo-tigo ni bure kuanzia dk ya 3.

Hiyo inaitwa bana matumizi.
 
hayupo humu JF, hii ni kero nimeona ngoja nije kuitolea JF angalau moyo wangu utulie, nimekwazika sana

kama hayuko Jf ina maana hataupata ujumbe wako na ataendelea kukusumbua.

Mimi huwa msichana akinipa huwa namuuliza masharti ya kumpigia simu. Kwanza simu za usiku ni za kitoto.
 
hayupo humu JF, hii ni kero nimeona ngoja nije kuitolea JF angalau moyo wangu utulie, nimekwazika sana

sijui ulikutana wapi na jamaa ingawa huwa kuna mazingira unalazimika kutoa namba bila kupenda ila kama ni mambo ya kimtandaoni usirudie.
 
Wewe tumefahamiana katika mazingira ya kistaarabu, tumezoeana kama binadamu wengine bila kuvuka mipaka, najua umeoa ila mimi hujui status yangu kama nimeolewa au niko single, kutokana na kwamba haikuhusu, sasa kinachokufanya unipigie simu saa 5 kasoro 7 usiku ni nini?wakati hata huo mchana huna la maana la kuniambia? Najuta kukupa namba yangu, kama matumizi yako ya simu ndo haya. Wanaume wengine mnakera sana
Hapo palipokolezwa.Hukupaswa kumpa namba wakati hata mchana hana la kukwambia.kwa akili zake chafu alifikiri unampa ili akupigie wakati ana la kukwambia(usiku) kwa kuwa anajua kuwa unajua mchana hana la kukwambia.
 
Wewe tumefahamiana katika mazingira ya kistaarabu, tumezoeana kama binadamu wengine bila kuvuka mipaka, najua umeoa ila mimi hujui status yangu kama nimeolewa au niko single, kutokana na kwamba haikuhusu, sasa kinachokufanya unipigie simu saa 5 kasoro 7 usiku ni nini? wakati hata huo mchana huna la maana la kuniambia? Najuta kukupa namba yangu, kama matumizi yako ya simu ndo haya. Wanaume wengine mnakera sana

Ndio mkome kutoa namba kwa vinega
 
Back
Top Bottom