Tuache kudanganyana, Ajira zina afadhali zaidi kuliko kujiajiri, watu wengi waliojiajiri ndio wapo kwenye utumwa

Unajua mzigo wa PAYEE?

Mfanyakazi anaukwepaje?

Hiyo frame si ni moja ya mtaji pia?

Anyways, hiyo gharama ya frame unalinganisha na mshahara/makato na mfanyakazi Wa level gani?

Bila wafanyakazi kulipwa mzunguko Wa fedha mtaani huwa ukoje?


Kiufupi tunategemeana.
Kuna jibu nilikuwa nalitafuta point 👇
Kutokana na mada hii, nilitaka kusema "bila shaka mtoa mada ni mtumishi/muajiriwa" na kwa bahati nzuri kuna mstari ndani ya chapisho unathibitisha hivyo.

Nilitaka kusema hivyo kutokana na ufahamu mdogo niliouona wa mtoa mada juu ya kodi. Anachokijua yeye kuhusu kodi ni VAT na PAYE tu na kwa maana hiyo anahisi wenaobeba mzigo mkubwa kuhusu kodi ni wafanyakazi na hawalalamiki kama wafanyabiashara.

Lakini kwa faida ya mtoa mada ni kwamba "biashara" ndo msingi wa kodi zote, bali kuna aina nyingi za kodi na tozo zinazotokana na biashara zinazolipwa na wafanyabiashara.

Kuwatazama wafanyabiashara kama "mawakala" wa serikali wa kukusanya kodi ya VAT inayolipwa na mlaji wa mwisho si sahihi. Nasema mtazamo huu si sahihi kwasababu kodi hii haimhusu mlaji wa mwisho tu bali pia mchuuzi (mfanyabiashara) kwakuwa na wao hununua bidhaaa au huduma wanazojihusisha nazo kwani maana ya biashara ni kuuza na kununua.

Baadhi ya kodi na tozo zinazowahusu wafanyabjashara ni kama ifuatavyo.
1. VAT
2. Corporate tax
3. Withholding tax
4. Railway development tax (RDL)
5. Import/export duty
6. Leseni za biashara
7. Tozo za kimamlaka kama vile PVOC, import permit, product registration kutoka TBS, TMDA, GCLA, FIre, OSHA, NEMC n.k kutegemea aina ya biashara husika
8. Tozo za leseni za biashara za halmashauri n.k
9. Tozo za usajili wa mtoa huduma/msambazaji kutoka GPSA n.k

Kwahiyo ili kujua ni nani mlipa kodi mkubwa kati ya wafanyabiashara na wafanyakazi inatakiwa kwanza viwango na aina ya kodi zinazowahusu na kabla kuhitimisha.
Hizi argument sio mara ya kwanza we are getting out of the point. Ila wewe ukiwaza mfanyabiashara unawaza machinga kwa sababu sio walipa kodi. Ila kodi nyingi sana zinatuhusu wafanyabiashara. .
 
kotekote kuzuri tu kama umekaa pazuri.

Sasa kama umeajiliwa na kazi unaijua na mshahara wako kwa mwezi ni 15m net au zaidi unashida gani zaidi ya kuenjoy.

Kama umejiajili na una kipato cha 15mil na zaidi kimesimama shida nini.. hapo ni kipato tu.
Ishu ni kipato, we unaejiajiri leo hii uanze mtaji wa laki 3 kuuza pweza vs mbunge baada ya miaka 5 huwezi kumfikia hata ugale gale
 
Inategemea umeajiriwa wapi au umejiajiri kwenye nini na kwa level gani, chukua graduate wa mwaka mmoja watano waliojiajiri na watano walio ajiriwa kisha linganisha maisha yao utapata jibu
Mtu aliejiajiri mwenye turnover ya zaidi ya 20M kila mwezi huyo huenda akawa anatengeneza more stake than waajiriwa wapya wengi.

Biashara nyingi halali faida kwa mwezi huwa 5-10% ya turnover ila kama ni mihadarati ama nyara huko ndio kuna faida za 100% au zaidi kila mwezi. Sadali akianza biashara ya ndumu leo baada ya miaka 5 huenda akawa kashajenga kabisa na ana hela ndefu kuliko hata mbunge.
 
Kuna kazi nyingine ni bora ujiajiri tu chukulia mtu analipwa 150,000 kwa mwezi huyu ni heri ajiajiri tu kwa sababu akikaza kwenye biashara yake anaweza kupata kipato zaid ya hicho kwa mwezi.
Nb:
Kujiari na kuajiriwa vyote muhimu inategemea mtu binafsi wapi anaona ana nafasi ya kuwa na kipato cha uwakika.
 
Kuna kazi nyingine ni bora ujiajiri tu chukulia mtu analipwa 150,000 kwa mwezi huyu ni heri ajiajiri tu kwa sababu akikaza kwenye biashara yake anaweza kupata kipato zaid ya hicho kwa mwezi.
Nb:
Kujiari na kuajiriwa vyote muhimu inategemea mtu binafsi wapi anaona ana nafasi ya kuwa na kipato cha uwakika.
Vizuri.
 
Pesa ndo inageuza maisha haya kuwa utumwa.

Tatizo sio kujiajiri au kuajiriwa bali ni pesa.

Pesa unayoipata ikiwa haitoshi kugharamia maisha yako lazima uishi maisha ya kitumwa.

Kuna mijamaa mingi tu imeajiriwa na inakula Kwa mrija , kadhalika mabingwa ambao wana run business zao zenye return kubwa .

Imagine wakurugenzi wa almashauri kwa package walizonazo, posho daily, usafiri wa Bure, nyumba unalipiwa na serikali , na rushwa zinazoingia na kutoka kwenye issue za tender. Mfanyakazi kama huyu utamshawishi vipi akajiajiri ?

Maisha kama haya wanayo wakurugenzi, maofisa waandamizi wa taasisi za serikali, wanasiasa, wabunge etc.

Kujiajiri kusikie tu, kama sio kampuni nenda kafanye tathimini mwenye unafuu ni bosi na mke wake tu , ila ukiwatazama wasaidizi utaona jinsi wanavyo struggle

The bottom line is that ...tafuta kazi inayolipa , iwe ya kujiajiri au kuajiriwa ikiwa unataka kuobdoka kwenye utumwa wa pesa.

Ila kitu unachopaswa kufahamu dunia imetengenezwa kuwepo na ma boss wachache na wasaidizi wengi ambao maisha Yao yatamtegemea boss.

The good thing is that wealth is accumulative. unaweza amua Leo kizazi chako Cha pili au tatu kua tofauti kwa kuanza uwekezaji leo
 
So Mwalimu nyerere, ma engeneer kama mfugale madaktari kama Dr. Masawe ambao wote walikua waajiriwa hawajaacha alama yoyote?
So Mwalimu nyerere, ma engeneer kama mfugale madaktari kama Dr. Masawe ambao wote walikua waajiriwa hawajaacha alama yoyo
Ukilima na trekta linaacha alama at that level. Lakini uhalisia mwenye kuacha alama ni mwenye kulitumia kwa matashi yake. Mfugale ni kama trekta in this case. Sidhani alikuwa na ndoto ya kujennga daraja tofauti na kutimiza agizo.

Kwa case ya Nyerere yeye alijiajiri as a politician. Level ya self actualization however is limited kwa politician maana anasimamia utashi wa raia na sio ndoto binafsi.
 
Sio siri unyama mwingi sana kujiajiri. Sisemi kwa nia mbaya, sababu nipo sehemu nimeajiriwa ila hizo ndombolo anazoniletea boss balaa! Yaani hapa nafanya mwisho mwezi huu tu! Mpuuzi mmoja huyu


NB: jitahidi kwenye mtihani wa maisha uwe na maksi ya kuvutia
 
Kujiajiri ni bora zaidi kama utakua na biashara za maana…la sivyo utapambana na unakuja kupata hela ya maana umezeeka..!kuajiriwa inategemea na position ulionayo..mfano mtu kama mkuu wa majeshi hv au gavana BOT
Ukiwaambia wafungue frem kariakoo hawakuelewi unajua..
Bottom line matajiri wakubwa duniani wamejiajiri..fact
 
Jamani jamani. Hebu tuweni wakweli kidogo. Asilimia kubwa ya Watanzania wana kipato cha chini maana yake ni kwamba wachache ndio wenye capital za kuanzisha na kuendesha biashara ikasimama kweli na kuleta faida ya uhakika. Hizi biashara ambazo zinaanzishwa, hasa hizi za kujiajiri (in most cases) ni zile zenye cashflow ndogo pia assets zake. Maana yake hata turnover inakuwa ni ndogo vile vile.
Biashara hizi zikiwa nyingi mfano machinga zinaua biashara ambazo atleast zinasimama na zinalipa kodi. Kwa sababu wengi wao kodi wanayolipa ni chache mno kuliko wale wafanya biashara ambao wana mitaji inayoeleweka.
Ni heri tuwe na waliojiajiri wachache wenye capital kubwa waweze kuwaajiri wengi kwa kukidhi na kuboresha matakwa ya wafanyakazi pamoja na stahiki zao.
Kuliko kila mtu awe mfanyabiashara ama kila mtu ajiajiri kama viongozi wanavyowaambia vijana. kwa sababu tunalitengeneza tatizo kubwa hapo baadae.
 
Back
Top Bottom