Tuache kudanganyana, Ajira zina afadhali zaidi kuliko kujiajiri, watu wengi waliojiajiri ndio wapo kwenye utumwa

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,094
Najua kwa haraka haraka mtafikiria kunijibu kwamba "Mwajiri hawezi fikia mafanikio ya Mo ai Bakhresa" ....vuta pumzi tulia!! Hao kina Mo watoe akilini mwako maana wapo kundi tofauti kabisa ni wafanyabiashara waliofikia mafanikio ya biashara zao kujiendesha hata wakiwa wamelala.

Mtu mwenye ajira hapa bongo serikalini ana nafuu zaidi maana mwisho wa mwezi mwajiriwa ana uhakika ila aliejiajiri ni juhudi zake, akipoteza mda imekula kwake.

Mwajiriwa hata akifiwa, akiumwa, akioa/kuolewa, anapewa kalikizo.. hapo kila jumamosi na jumapili yupo free, bado ana likizo ya mwezi moja kila mwaka, sherehe za serikali na za dini haendi kazini, Ana muda mwingi wa kuweza kupumzika na familia na kufanya shughuli za kijamii.

Wafanyabiashara wengi nawajua tangu nimepata akili za kuijua dunia mpaka leo hii wao siku ya kupumzika ni christmas tu, wenye nafuu huwa wanapumzika jumapili pekee, siku zingine hizo ni bampa to bampa wanaondoka alfajiri wanarudi usiku, yani hata muda wa kuspend na watoto hawana,

Ukiwa kwenye ajira unaweza kujiajiri pia

Nani mtumwa hapo
 
Kujiajiri hupelekea kila siku unaumiza kichwa na kupata pressure za ajabu ajabu juu ya biashara yako. Ndo maana wengi wao huzeeka mapema.

Hali kadhalika mawazo na hofu juu ya mwenendo na maendeleo ya biashara yako.

Kujiajiri kumesababisha watu wengi sana kuwa wachawi kwa ajili ya kuboresha vipato vyao.

Kujiajiri ni safari ya kupanda na kushuka, na pia haieleweki na hata Maendeleo ya watu wake hayaeleweki pia.
Na kikukweli wengi waliojiri ndio watumwa wa biashara zao.
 
Kiinua mgomgo chako kwa kazi yako utakacho lipwa. Ndio namiliki Bank.
Tofauti n PESA iliyoko kwenye mzunguko w bzness yangu.
Asante mungu kwa kunifanya niwe entrepreneur.
Jamani raha kuona PESA zako ziko ongezeka kidogo kidogo BANK mpk kua sw n kiinua mgomgo cha mtu.
Pia fresh money ni raha mnoooo. Pia likizo unajipangia uende wapi.
HII NI KWA NIA NJEMA TU
Kila mtu ashinde mechi zake.
 
Back
Top Bottom