Watu wengi wanaoponda ajira ni umasikini / utumwa mara nyingi wazazi au ndugu zao wana ajira za chini sana

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,034
Oh, Ajira ni utumwa
Oh, kuajiriwa ni manyanyaso

Huwa hawanaga utofauti sana na wale waliokulia maisha ya kimasikini ambao ni rahisi sana kuwajua siku hizi, ukisikia mtu anatumia sana msemo maarufu " Tafuta pesa" ni kwamba huyo kuna uwezekano mkubwa sana kakulia maisha ya kimasikini sana.

Basi ndivyo ilivyo kwa wanaoponda sana ajira, mara nyingi ni kwamba wao wamejionea maisha ya ajira kwa wazazi au ndugu walioajiriwa private kwenye malipo madogo na manyanyaso ama ikiwa serikalini basi ni hizi ajira zenye mishahara midogo, fursa chache za kuongezwa vyeo, n.k.

Kuna watumishi wa serikalini wako poa tu wanasomesha watoto shule za private, wana nyumba nzuri, magari hadi watoto wanawanunulia, n.k. na hapo mambo huwa yanakuwa matamu zaidi mtumishi akipiga hybrid yani ana biashara zake pia.

Watu wanakula maisha vizuri tu kwa ajira tusikaririshane kwamba ajira zote ni umasikini,

Mtu ana likizo ya siku 30 kila mwaka, kila jumamosi na jumapili ni off, akiumwa anapewa likizo hadi apone, saa 11 jioni ashatoka kazini anaenda kuspend na familia yake, sioni kigezo cha kumponda kiasi hicho kwamba huyu mtu ni mtumwa .

Offcourse biashara ndio inapesa zaidi lakini pia tukumbuke kwenye biashara kuna upande wa kikatili zaidi ambao wengi huuficha, kuna kufirisika, ushindani mkali, kodi, n.k. so biashara ni tamu lakini nayo tuwe tunaiangazia upande wake wa kikatili, uanweza ukawa unajadiliana na mtu aliejiajiri hata elf 10 kwa siku kuingiza ni shughuli lakini ghafla anajitetea kwamba ajira utumwa kina Mo na Bakhresa (wawekezaji) hawajaajiriwa, hataki kusema yeye kila siku lazima afungue ofisi, kurudi usiku, hana likizo, madeni, n.k.
 
Tatizo ni hizo ajira tamu na nono zipo chache sana, tofauti na ajira nyingi ambazo hazina masirahi..
You just imagine mtu ukute analinda huko na analipwa laki moja!,huyu mtu anafamilia wakati kwa mwengine hiyo laki moja anaweza itengeneza aidha kwa siku mbili au Moja ama masaa tu!..

Lazima watu watazisema tu ajira maana nyingi za ajira hazina marupurupu kama ulivyoainisha hapo,mshahara haujatoka tayari ushaishia kwenye madeni!. Plus ukute na unapofanyia kazi Kuna minyanyaso so unahitaji kunyenyekea ndo kabisa hadi mwili unakondeana unakuwa kama moja..😂
 
Watu wote hawez kuajiriwa ndo maana hata system ya ajira na mfumo wote wa utumishi watu wake hawafiki hata million 5 Wakati watanzania tuko zaidi ya milion 50.

Pamoja na yote sector binafsi (private ) ndo inaonekana kutoa ajira nyingi kuliko hyo serikali, kikubwa kila mtu afuate anachoona yeye mwenyewe kinamfaaa
 
Oh, Ajira ni utumwa
Oh, kuajiriwa ni manyanyaso

Huwa hawanaga utofauti sana na wale waliokulia maisha ya kimasikini ambao ni rahisi sana kuwajua siku hizi, ukisikia mtu anatumia sana msemo maarufu " Tafuta pesa" ni kwamba huyo kuna uwezekano mkubwa sana kakulia maisha ya kimasikini sana...
Kweli kabisa.
Kwa Hali iliyopo mtaani kwa Sasa, bora ajira, biashara kutembea imekuwa ngumu sana.

Ila ukitaka kuwa tajiri, jiajiri na hakikisha una mtaji na plan ya kutosha.
 
Mshahara wa shilingi ngap huko srikalini unaosema ambao sio wa kimaskini.
 
Back
Top Bottom