Kujiajiri ni utumwa zaidi ya kuajiriwa, waliojiajiri wengi wanakosea kujiweka kundi moja na wamiliki wa biashara

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,407
19,070
Nimekuwa nikiona sana kuna kukosekana kwa uelewa juu ya utofauti wa mtu aliejiajiri (self employed) na mmilliki wa biashara (cusiness owner)

Mtu aliejiajiri ni mtu anaefanya shughuli zake yeye mwenyewe kwa asilimia kubwa ili kuzalisha kipato, mfano ni mangi mwenye duka, mtu mwenye duka anaeuza yeye kwa asilimia kubwa, fundi simu, wanaotengeneza mabango, n.k. Wengi hawana wafanya kazi na hata kama wapo bado watakuwepo kwa asilimia kubwa directly.

Wamili wa biashara (business owners) hawa wanakusanya rasili mali pamoja na kuzi organize ili kupata faida, huyu ana ajiri watu wamfanyie kazi, hapa ndipo kuna wale wenye car wash zao mtu anaenda jioni kukusanya hesabu yake kutoka kwa vijana kama 10 aliowaajiri n.k, hapa ndipo wanaingia kina Mo, Bakhresa, Gsm, vunja bei, n.k Wafanya kazi wao wanawahi kuamka kwenda kuwazalishia pesa huku wao hata wakiuchapa usingizi shuguli zinaendelea.

Waliojiajiri wengi hapa tz miaka nenda rudi unamkuta yeye ndie anaetoka jasho kwa asilimia kubwa kwenye biashara yake bila kupiga hatua ya kuwa business owner (mmiliki wa biashara).

Asikwambe mtu kujiajiri ni utumwa, yani muda wako na nguvu zako zitanyonywa mno tofauti na alieajiriwa ambae anaingia kazini saa 2 na kutoka saa 11, ana mshahara stable unaokua, anaweza kupata promotion, anapumzika umamosi, jumapili, siku kama 20 za sherehe za serikali na mwezi mzima anapewa likizo.

Kwa wenzetu, mtu akijiajiri anakubali kuwa mtumwa ili kufikia lengo la kuwa mmiliki wa biashara ila nashangaa hapa bongo, mtu kajiajiri miaka zaidi ya 10 yani bado hana lengo la kuwa mmiliki wa biashara.
 
Bora niitumikie nafsi yangu Kama mtumwa kuliko kutumikia mtu mwingine
Mkuu haya mawazo ya kikoloni tu, Tatizo wengi wanafikiri bado tupo kwenye ukoloni kwamba bosi anaweza kukutukana, kukupiga, n.k.

Mabosi mbona tupo nao ma ofisini hawana shida, Nao wanalipwa mishahara kama sisi, wakileta za kuleta hawana kazi, lazima heshima iwepo.

Hayo mambo ya mabosi labda huko kwenye ajira za private kuna kina kanjibahi (wahidi) wanatukana sana wafanyakazi ama kupiga kabisa, hizi sasa ndio ajira za kitumwa na hapo mtu analipwa kidogo sana.

Huku serikalini mambo yapo fresh tu, mshahara uhakika, posho zipo, bosi hana shida na wewe ana shida na mhahara wake, n.k maisha anenda vizuri tu.
 
Mkuu toka jaana naona upo busy na kupinga waliojiajiri , wamekukosea nini?
Halafu unapotoa mfano wa waliojiajiri kwa nini unachagua team za mchangani?
Ana pata tabu na waliojiajiri toka jana, kama kaajiriwa na yupo comfortable atulie ale maisha, kwann upande wa pili unamtesa??
 
Mkuu haya mawazo ya kikoloni tu, Tatizo wengi wanafkiri bado tupo kwenye ukoloni kwamba bosi anaweza kukutukana, kukupiga, n.k.

Mabosi mbona tupo nao ma ofisini hawana shida, Nao wanalipwa mishahara kama sisi, wakileta za kuleta hawana kazi, lazima heshima iwepo.

Hayo mambo ya mabosi labda huko kwenye ajira za private kuna kina kanjibahi (wahidi) wanatukana sana wafanyakazi ama kupiga kabisa, hizi sasa ndio ajira za kitumwa na hapo mtu analipwa kidogo sana.

Huku serikalini mambo yapo fresh tu, mshahara uhakika, posho zipo, bosi hana shida na wewe ana shida na mhahara wake, n.k maisha anenda vizuri tu.
Nenda Nssf ukawaone wajinga wenzanko waliokuwa wameajiliwa wanavyoteseka kudai mafao yao halafu urudi hapa.
 
Nenda Nssf ukawaone wajinga wenzanko waliokuwa wameajiliwa wanavyoteseka kudai mafao yao halafu urudi hapa.
Kwenye swala la pensheni wa kulaumiwa ni serikali na sio wastaafu, ni wizi wa mchana kweupe kabisa, haina utofauti na wale task force waliokuwa wana nyang'anya pesa za wafanya biashara na kuwafanya wawe maskini, siwezi kuwaita hao walionyang'anywa pesa mazuzu, ila kama wewe umeona neno sahihi la kwaita wanaoibiwa pesa ni wajinga, basi sina cha kufanya.

Lakini pia kukosa elimu ya fedha nak kumefanya wengi uyumba kiuchumi wakistaafu, majanga yakitokea kwenye biashara , n.k

Wapo wacheza mpira walioingiza mabilioni ila kwa kukosa maarifa ya fedha leo hii wamefulia.

Wapo wafanya biashara waliopiga sana hela ila kukosa maarifa ya fedha leo hii wanatia huruma.

Na pia wapo hao waliokuwa na kazi nzuri tu, mtu analipwa milioni 3 kila mwezi lakini kaishia hana hata nyumba na yote hii ni kukosa maarifa ya fedha.

Binafsi mimi nimeajiriwa lakini pia ni business owner, kuna sehemu nimeweka mtu anizalishie pesa, mimi huwa naenda kukagua tu
 
Faida ya kujiajiri ni kujicontrol mwenyewe, hakuna manyanyaso wala kumsujudia mtu! Mwamzoni kweli mambo yanakuwa magumu, lakini muda unavyozidi kwenda ugumu hupungua kwa kuwa unapata uzoefu wa biashara. Ukisikia historia ya mzee wetu Baressa, watakuambia alianza na u-shoe shine, lakini leo ukiona biashara zake huwezi kuamini. Hivyo, ni kweli utateseka mwamzoni lakini mwisho wa siku huyu aliyeajiriwa akuja kuomba kazi kwako.

Ni muhimu sana kwa walioajiriwa kujifunza ujasiriamali, kwani kuna wakati katika maisha yako hutakuwa kwenye ajira, hivyo ni ujasiriamali pekee ndio utakaokusaidia. Kumekuwa na tabia katika jamii zetu mfanyakazi kumdharau mjasiriamali mdogo, anasahau kuwa huyu kesho ndio atakuwa Baressa (au Mo). Kuna msemo kuwa mbuyu ulianza kama mchicha, vivyo hivyo hata katika kujiajiri.
 
Hao uliowatoa kama mfano sidhani hata kama waliwahi kujiajiri, halafu ni mifano dhaifu sana

Natoa ushamba, Wabngo wengi wamejiajiri hawajafikia hatua ya kuitwa business owners.

Walikuwepo kina jokate na nikki wa pili, walivyopewa ukuu wa wilaya hawakufukiria mara mbili
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Mkuu haya mawazo ya kikoloni tu, Tatizo wengi wanafikiri bado tupo kwenye ukoloni kwamba bosi anaweza kukutukana, kukupiga, n.k.

Mabosi mbona tupo nao ma ofisini hawana shida, Nao wanalipwa mishahara kama sisi, wakileta za kuleta hawana kazi, lazima heshima iwepo.

Hayo mambo ya mabosi labda huko kwenye ajira za private kuna kina kanjibahi (wahidi) wanatukana sana wafanyakazi ama kupiga kabisa, hizi sasa ndio ajira za kitumwa na hapo mtu analipwa kidogo sana.

Huku serikalini mambo yapo fresh tu, mshahara uhakika, posho zipo, bosi hana shida na wewe ana shida na mhahara wake, n.k maisha anenda vizuri tu.
Ukishaajiriwa tayari unakosa uhuru wako, bosi ni mungu mtu wako na utawajibika kwake hadi unastaafu, halafu uki pata milioni 150 zako ndo unakuja kukumbuka kujiajiri na biashara usizozijua matokeo yake pesa ya pension inapotea yote .
Idea za kujiajiri ni kuchukua changamoto zinazokuzunguka na kuzifanya fursa , simple like that
Bahati mbaya white collars huwa mefungwa na mentality za kiofisi, ofisi , kwamba workmate akikopa gari benk , basi kila office mate anajua historia nzima ya gari hilo.
Huyo mangi mwenye duka unaweza kumuona haendelei kumbe mwenzio ana project kubwa sehemu nyingine na kwakuwa anacheza na akili zenu mnamuona kama mjinga .kwanza usikute ana Atm Card kadhaa za walimu na pin number wamemuachia kwa ajili ya huduma walizokopa .
 
Hao uliowatoa kama mfano sidhani hata kama waliwahi kujiajiri, halafu ni mifano dhaifu sana
Sasa ndugu yangu tukisema tuajiriwe wote serikali itaweza kutuajiri? Sikuizi ajira imekuwa ngumuu watu mnapeana kindugu tuu eee tuache na kujiajiri kwetu wewe pambana na ajira yako.
 
Mkuu haya mawazo ya kikoloni tu, Tatizo wengi wanafikiri bado tupo kwenye ukoloni kwamba bosi anaweza kukutukana, kukupiga, n.k.

Mabosi mbona tupo nao ma ofisini hawana shida, Nao wanalipwa mishahara kama sisi, wakileta za kuleta hawana kazi, lazima heshima iwepo.

Hayo mambo ya mabosi labda huko kwenye ajira za private kuna kina kanjibahi (wahidi) wanatukana sana wafanyakazi ama kupiga kabisa, hizi sasa ndio ajira za kitumwa na hapo mtu analipwa kidogo sana.

Huku serikalini mambo yapo fresh tu, mshahara uhakika, posho zipo, bosi hana shida na wewe ana shida na mhahara wake, n.k maisha anenda vizuri tu.
Serikalini kama ni mwalimu bosi wa juu ni mkurugenzi, ofisa elimu mkoa, wilaya na kata mabosi hawana neno na wafanyakazi walio chini yao, hakuna kukoromeana, mkuu wa shule ndio kabisa hawezi leta za kuleta kwa walimu wake, kazi zinafanyika kwa uhuru
 
Kitu muhimu panapo kucha na makucha yake kila kiumbe kina future yake wengine kwa maduka wengine kwa supermarket.
Falsafa za Unju Bin Unuq
 
Mkuu haya mawazo ya kikoloni tu, Tatizo wengi wanafikiri bado tupo kwenye ukoloni kwamba bosi anaweza kukutukana, kukupiga, n.k.

Mabosi mbona tupo nao ma ofisini hawana shida, Nao wanalipwa mishahara kama sisi, wakileta za kuleta hawana kazi, lazima heshima iwepo.

Hayo mambo ya mabosi labda huko kwenye ajira za private kuna kina kanjibahi (wahidi) wanatukana sana wafanyakazi ama kupiga kabisa, hizi sasa ndio ajira za kitumwa na hapo mtu analipwa kidogo sana.

Huku serikalini mambo yapo fresh tu, mshahara uhakika, posho zipo, bosi hana shida na wewe ana shida na mhahara wake, n.k maisha anenda vizuri tu.
Tena Kama maboss wengine Ni wazee wa totoz tukienda nao site mbona furesh.mkishapewa za night yenu kila mmoja na lodge yake na Mambo yake..kukutana Ni asubuhi kwenye gari then Safari..boss lazima tu awe mkali kdg akupige mikwara kdg ila hamna jipya kwa maboss kikubwa unafanya kazi na sio mtoro Basi.
 
Serikalini kama ni mwalimu bosi wa juu ni mkurugenzi, ofisa elimu mkoa, wilaya na kata mabosi hawana neno na wafanyakazi walio chini yao, hakuna kukoromeana, mkuu wa shule ndio kabisa hawezi leta za kuleta kwa walimu wake, kazi zinafanyika kwa uhuru
Kwa mfano me boss wangu hata sionani naye Sana labda asubuhi tunapo sign na pale anapotutuma kazi Basi ..ila Mambo mengine kila mtu na zake Tena boss wangu me tukienda mazingira yetu ananichukulia na bia za mafungu tatu.
 
Back
Top Bottom