Tuache drama maandamano ni mambo ya kawaida kisheria

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,609
8,753
Serikali inajaribu kukuza mambo ambayo yanatakiwa kuwa utamaduni wa kawaida.

Maandamano ni sehemu ya demokrasia na maandamano sio fujo ni haki ya kujieleze. Badala ya kujaza Polisi wa wanajeshi kama vile kuna vita kunatakiwa kuwa na pikipiki za Polisi kama maandanamo ya sabasaba au Mei Mosi.

Mabadiliko kwenye jamii yeyoye ni mambo ambayo hayazuiliki ukizuia hili litakuja lile kwasababu Mungu kaumba hii Dunia na watu kwa mabadiliko kila siku.

Hata kama hukubaliani na watu zile nyakati za kuzuia haki kwa watu zimepitwa na wakati.

Nchi yetu sasa inaanza kuwa nchi ya kibiashara hasa za mazao, tunajenga treni hivyo tutakuwa na raia wa nchi jirani wengi sana, tunakuza utalii, tunataka ku host michezo ya kimataifa haya ni maaendeleo lakini yanakuja na mabadiliko.

Raisi mfano wamekaa na Mbowe na kuongea mara nyingi sana sasa leo Mbowe hakubali jambo na kutaka kuandamana ghafla amekuwa mtu wa fujo wakati alikuwa anaongea na Raisi kwenye kiti!!.

Tanzania kama tunapenda nchi yetu kweli ni lazima tujue tuko watu tofauti wenye fikra tofauti na tutatofautiana kama binadamu.

Lakini sheria zetu wenyewe tuzifuate maandamano kisheria yanaruhusiwa na tuheshimu sheria zetu wenyewe.
 
Umeandika vyema
Nchi ya ajabu sna hii. Maandamano ya kumpokea makonda akienda lumumba yalikuwa ni sawa na hakuna shughuli binaadamu zilizoathirika. Wengine wqkiandamana ni fujo na vurugu na kuzuia watu kujiingizia kipato
 
Back
Top Bottom