TTCL fiber na Voda Supakasi ipi yafaa kwa matumizi ya home intaneti?

Wakuu habari zenu.

Natumai mu wazima.

Kutokana na mabando kuwa juu, niliamua kwenda maduka ya TTCL na Voda shop kuangalia home internet.

TTCL walinipa hii details.
View attachment 2097538

Kulingana na matumizi yangu nilipenda hicho cha 55k.

Lakini sijajua wakoje kihuduma plus kununua DSL modem.

Nikaamua kucheki Voda Supa kasi

View attachment 2097542

Voda wana laki 115000 lakini nimeenda Voda Shop Ubungo plaza wananiambia wana Laini ya Supakasi Unlimited 50k kwa mwezi.

Watalaamu naomba ushauri ni ipi reliable isiyo na speed ya kusua sua ili nichukue nihustle kutafuta hela.

Mabando ya 3k kila siku yanaumiza alafu unatumia kibahili sio.

Naombeni msaada sana.

Shukrani in advance.
Boss hapa mjini kampuni tatu tuh ndo zina true unlimited bundles ambazo speed hazishuki
1.Zuku fiber
2.CTV
3.TTCL

Usikubali kununua internet za dish, hizo zinakua na downtime mara nyingi
 
Wao watakuwa wanamaanisha unlimited bundle ila kimsingi huenda ikawa connected na speed twists. ISP wengi wa kibongo ni matapeli
Ila hawajafafanua kama ni
  • Unlimited data bundle au
  • Unlimited speed au
Vyote unlimited kwa pamoja
Terms and condition zipo wazi tunaamu tu kuzikimbia.

Home internet ni unlimited bundle hupimiwi, nimetumia TTCL, Zuku, na wengineo.

Speed sio unlimited unalipa kutokana na speed unayotaka na sio dedicated ni up to.

Ila kutokana na capacity ya fiber kuwa kubwa kibongo bongo bado sana kuijaza, waya mmoja unapeleka hadi 10gbps,

Ndio maana unaona ukilipa cha 10mbps wa wanakupa 20, ukilipa 40 wanakupa 100 etc.
 
Back
Top Bottom