TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (T-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)

- Maeneo gani? (Tukifahamu maana ulipo, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate msaada toka kwa wakala wetu aliye karibu nawe)

- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?

- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza.

- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Zifuatazo ni ofisi zetu za huduma kwa wateja ndani ya jiji la Dar es Salaam.

1. POSTA
Mtaa wa Samora, jengo la Extelecom ghorofa la Chini.

2. KARIAKOO
Mtaa wa Makamba/Msimbazi, jengo la Akamba Bus Service.

3. UPANGA
Mtaa wa Magole/Maliki, karibu na Diamond Jubilee.

4. MAGOMENI
Mtaa wa Minaki/Fundiki, karibu na Manispaa ya Kinondoni.

5. KIJITONYAMA
Kijitonyama Sayansi, barabara ya Ali Hassan Mwinyi/ Rose Garden.

6. OYSTERBAY
Barabara ya Haile Selassie.

7. UBUNGO
Jengo la Ubungo Plaza/ Ghorofa la chini.

8. MBEZI BEACH
Mbezi Makonde/ Jengo la Shamo Tower.

9. TABATA
Tabata Bima, barabara ya Segerea karibu na kanisa la Romani Katoliki.

10. CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM.
Jirani na tawi la benki ya NBC, jirani na kilipo kituo cha polisi cha UDSM.

11. BARABARA YA PUGU
Barabara ya Mwalimu Nyerere, karibu na Sigara.

12. WAGENI
Uwanja wa ndege.

13. PUGU
Jengo la Quality Centre, ghorofa la chini.

14. KISUTU
Mtaa wa Mchafukoge/Libya jengo la Haad Plaza.

15. TEGETA SHOP
Jengo la Kibo Complex, ghorofa la chini.

16. MWANANYAMALA SHOP
Mwananyamala A, barabara ya Mwinjuma yalipo makutano ya Mwananyamala A.

17. KURASINI
Kurasini Exchange Area, jirani na Chuo cha Diplomasia.

Wasiliana nasi:
022 210 0100
0738 151 511
www.ttcl.co.tz

#RudiNyumbaniKumenoga
View attachment 1529645

Karibu.

Rudi Nyumbani Kumenoga
Naota kama ttcl hua inahujumiwa na kampuni binafsi za simu na mawasiliano kupitia mameneja na hata wakurugenzi wake wasio wazalendo. Sio hivyo hata tbc hufanyiwa hivyohivyo na radio na television binafsi.
Mfano ni vipi itv/ radio one isikike kote nchini vizuri kabisa wakati tbc ya serikali hata dar tu radio huipati vizuri?
 
Unaota?
 
Tumia hii 0733600060
Kiongozi, hivi hizi huduma za Fiber Internet ni hadi uombee HQ (Extelcom) au hata kwenye hizi zonal office like TTCL Nyerere Rd! Nauliza kwa sababu pale HQ nimeshakosa imani napo manake haiwezekani mtu unajaza fomu kisha wanadai watatuma mtu na mtu hatokei hata baada ya kufanya follow-up! Wale wa Nyerere Rd kama hawajabadilika, zamani walikuwa fasta sana!! Mara mbili walishanipa huduma kwa kuja home within 24 hours!! Labda kwavile wana-deal sana na business community, na wao wame- adapt ile culture.
 
Hapana, unajaza kwenye ofisi yoyote Ile ya TTCL Customer Care. Baada ya hapo atatafutwa fundi aliye karibu na wear ili aje kukufikishia huduma unayotaka.

#RudiNyumbaniKumenoga
 
Kwa nini Hamboreshi Network yenu Kingamboni.Eneo la Nyumba za WHC-Watumishi House. Matikiti? Network ya Hovyo mno. Alafu mnasema nyumbani kumenoga!
 
Makampuni karibu yote yamesha hama kwenye 2G. TTCL bado wapo 2G. Boresheni huduma zenu vizuri. Kwa sasa Voda wameanza na 5G. Sijui TTCL yetu tutahamia lini kwenye 3G.
 
nahitaji link ya hii ttcl mifi niweze kuingia kwenye configuration panel. msaada please
 
Mkuu nipe moyo tena. Oktoba ndio hii ishafika nusu .

Hivi hapa Tz kuna watu wanauza cable za fiber kama hizi zinazopita kwenye nguzo. .
Na huwa wanauza pesa ngapi kwa mita.

Nimejaribu kupitia hii www.fiberoptic.co.tz website sijaona bei zaidi ya email yao.
Mkuu pole sana aisee.
Kama vipi jiongeze tu nenda kanunue zako vifaa vyote kisha tunakuja kukufungia FREE!
Ukiendelea kusubiria vifaa, mpaka mzigo utakapowasili.
Vifaa unaweza kuvipata hapa jirani na stendi ya mwendokasi ya KISUTU kuna duka la Tronic au unaweza kuwasilana na muuzaji huyu 0718814556 ambaye yupo hapo dukani.
 
Kiongozi, hivi hizi huduma za Fiber Internet ni hadi uombee HQ (Extelcom) au hata kwenye hizi zonal office like TTCL Nyerere Rd! Nauliza kwa sababu pale HQ nimeshakosa imani napo manake haiwezekani mtu unajaza fomu kisha wanadai watatuma mtu na mtu hatokei hata baada ya kufanya follow-up! Wale wa Nyerere Rd kama hawajabadilika, zamani walikuwa fasta sana!! Mara mbili walishanipa huduma kwa kuja home within 24 hours!! Labda kwavile wana-deal sana na business community, na wao wame- adapt ile culture.
Mkono mtupu haulambwi na kumbuka kwenye uzia penyeza rupia
 
Back
Top Bottom