True Story: Binti alivyotumia mbinu ya kijasusi ili kuolewa.

hiki kisa cha kweli kabisa! Baina ya binamu yangu (mwanaume), mwanaume na mdada mmoja. Mwanaume mweneyeji wa moshi) anafundisha shule moja ya sekondari nje ya mji wa morogoro na binti (mwenyeji wa mara) anafundisha shule iliyopo mjini morogoro.
Kwa mara ya kwanza mwanaume alikuwa "single") walikutana katika usahihishaji wa mitihani ya mock kidato cha nne - 2008. Baada ya hapo waliendelea kuwasiliana kama marafiki wa kawaida, walikuwa wakikutana mjini, kanisani (ikiwa kama mwanaume alitumwa kikazi mjini).

Mwaka 2010 mwanaume alipata nafasi ya kujiendeleza kielimu, elimu ya shahada, katika chuo kikuu kishiriki cha mwenge kilichopo moshi (nyumbani kwa mwanaume). Katika kipindi chote cha mawasiliano binti alimshinikiza sana mwanaum) kufika alikopanga bila ya mafanikio, lakini mwanaume aligoma.

Siku chache kabla ya mwanaume kwenda chuo alipata shinikizo kubwa kutoaka kwa binti, hivyo akaamua kwenda, kwani aliambiwa kuna jambo muhimu sana binti anataka kumwambia. Mwanaume alifika kwa binti ili kujua alichokuwa anaitiwa. Binti alimwambia mwanaume "mimi nipo single, niliwahi kuwa na uhusiano na mkaka mmoja nikiwa chuo, na wewe ndio chaguo la maisha, nimekuwa nikikuchunguza sana tangu ile siku ya kwanza kwenye kusahihisha, naomba uwe mume wangu wa kufa na kuzikana". Mwanaume alipata wakati mgumu sana kutoa jibu na kumwambia atatoa jibu baada ya tafakari.

Mpaka mwanzoni mwa mwaka 2011 mwanaume alikuwa hajatoa jibu lolote. Hapo ndipo binti alipofanya 'ujasusi' . Binti alijua siku mwanaume anayomaliza mitahani ya ue, hivyo, alimfungia safari kutoka morogoro hadi moshi bila ya mwanaume kujua. Binti alimjulisha mwanaume saa nane mchana ya kwamba yupo njiani (same) na anafuata jibu, huku mwanaume akiwa amewataarifu wazazi wake ya kwamba kesho yake angeenda nyumbani.

Mwanaume alipata mshtuko mkubwa, kwani hakuweza kumkatalia wala kumwambia mama yake ya kwamba hatokwenda kijijini. Binti alifika mjini moshi jioni, mwanaume akamtafutia gesti na wakaanza majadiliano.

Binti alipogundua ya kwamba mwanaume atakwenda kijijini siku inayofuata, alikwenda kununua vitenge doti mbili, sukari n.k. Na kumwambia mwanaume ni lazima waende wote kijijini ili apate kumsalimia mama 'mkwe'. Baada ya binti kuona mwanaume anaogopa sana na kusitasita alimwambia "naona hunitambui, tukifika kwa mama utanitambua vizuri". Walipofika kijijini, kabla ya mwanaume kumwelezea mama yake chochote juu ya uhusiano wake na yule binti, binti alipata muda wa kuongea na mama kidogo na kumpa zawadi alizonunua pamoja na hela.

Baadaye mwanaume alipomwelezea mama yake juu ya uhusiano wake na yule binti, mama alimwambia, mbele ya yule binti ya kwamba yule binti ndiyo mwali anayemtambua, kwani umri wa kijana wake ulikuwa umeenda (ana maika 30) na ajaonyesha dalili yoyote ya kuoa, pia yule binti ni sahihi kwani (ana miaka takribani 28) alikuwa tayari kuolewa na anaonekana ananidhamu (kumbuka binti alimpa mama zawadi pamoja na hela). Mama aliwaita wajomba wa wazee kadhaa ili kuwatambulisha mwali wake mtarajiwa na kuwaambia stori nzima, ndugu wote wabariki uhusiano wao.

Kwa sasa wanaendelea vizuri, pande zote mbili za wazazi zinauhusiano mzuri na wanaandaa ndoa kufunga ndoa mwakani pindi mwanaume atakapohitimu masomo.

Poleni kwa kuwachosha, kwani habari hii ni ndefu sana. Kwa wale 'single ladies' ukiona inakufaa tumia, na sisi bachelors, ikitutokea tusishangae. Naomba kuwakilisha.

bila strategies mnafikiri inakuwaje usawa huu!safi sana binti
 
zomba huwezi kuukumbatia mbuyu kwa mikono dr.slaa ni mbuyu kwako babu wewe ,alafu wewe sio msafi kivile kumwona mwenzio ni mzinzi sana zomba watu wengi tunadhambi na tunaishi kwa toba na rehema za mungu tu,kila thread unayochangia MMU lazima umtaje huyo mzee ule ni mbuyu kwako kamwe huukumbatii utabakia kutokwa povu tuuuuuu.mwenzako ashatubu wewe kila siku unapiga kichwa chini kuomba toba ila ukirudi nikuendelea kuhukumu tuu unamsaidia mungua au fanya yanayokuhusu acha ya Mungu afanye mwenyewe

Zinaa ni zinaa awe Slaa au wewe haiteteeki. Na hakuna ubaya kukataza yaliokatazwa na Mwenyeezi Mungu mbya ikiwa ntaanza kukataza yasiokatazwa. Upo hapo ulipo? au wewe kuzini unaona ni jambo zuri? na kwa ubuyu wa Slaa wako anaonesha mfano mzuri kwa jamii?

Pata darsa kidogo:

Qur'an 3:110. Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa Watu wa Kitabu nao wameamini ingeli kuwa bora kwao. Wapo miongoni mwao waumini, lakini wengi wao wapotovu.
 
what is drasa by the way zomba u are totaly right ila kumbuka kuna kitu kinaitwa toba watu wanatubu ,na sio vizuri kumtaja kila kwenye kosa linalofanana nalo how many times wewe unamkashifu kuwa ni mzinzi je lii kheri kuendelea kuzini ovyo au kualalisha je ina maana gani hii majuzi wengi wawaislam hufunga ndoa takatifu ili awe safi anapoingia kwenye mfungo si ndio! sasa basi li wapi kosa la huyo slaaa.acha hiyo tabia kabisa usimchafue mtu kwa itikadi zako za kidini hamna msafi kamwe tunaishi kwa toba na rehema za Mwenyezi Mungu tu.UNGEKUWA WEWE NI SAFI USINGESWALI 5 KILA SIKU INAMAANA UNAMKOSEA MUNGU KILA WAKATI NA KULITAMBUA HILO UNAKWENDA KUSWALI
 
Kuna darwesh mmoja maarufu sana akiitwa darwesh kibendera, alikuwa akiongea kuhusu haya haya ya kuzini ya kulewa ya kusengenya watu, na mwoshowe ansema, anekasirika "ndio yeye huyo".

Sasa ndio sifa yake hiyo huyo, hutaki isemwe au wewe unaona kiongozi wa Kitaifa anafaa kufanya anayoyafanya Slaa? hivi anafundisha maadili yepi kwa umma? iwe Kikristo, Kiislaam au Kwa wasio na dini, basi kama nchi haina maadili? ingawa haina dini?
 
Itakuja kum-cost siku za mbele, coz hapo inaonesha mwanaume hana mapenzi ya dhati kwa huyo mwanamke, so ajiandae na small house
 
Inamaana mama mkwe anakalainika na vitenge kiasi ambacho hata mwanawe hakumsikiliza?
 
Inamaana mama mkwe anakalainika na vitenge kiasi ambacho hata mwanawe hakumsikiliza?
 
kusema ukweli hapo kijana atakua alikua anampenda binti maana hakuna kitu kibaya kama kulazimisha mapenzi sembuse ndoa??ndoo maana Mpoki alisema "kupenda usipopenda ni sawa na kusubiri meli Airport".
 
Back
Top Bottom