True Story: Binti alivyotumia mbinu ya kijasusi ili kuolewa.

Kimbori

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
5,417
3,154
Hiki kisa cha kweli kabisa! baina ya binamu yangu (mwanaume), mwanaume na mdada mmoja. Mwanaume mweneyeji wa Moshi) anafundisha shule moja ya sekondari nje ya mji wa Morogoro na binti (mwenyeji wa Mara) anafundisha shule iliyopo mjini Morogoro.
Kwa mara ya kwanza Mwanaume alikuwa "single") walikutana katika usahihishaji wa mitihani ya Mock Kidato cha Nne - 2008. Baada ya hapo waliendelea kuwasiliana kama marafiki wa kawaida, walikuwa wakikutana mjini, kanisani (ikiwa kama mwanaume alitumwa kikazi mjini).

Mwaka 2010 mwanaume alipata nafasi ya kujiendeleza kielimu, elimu ya Shahada, katika Chuo Kikuu kishiriki cha Mwenge kilichopo Moshi (nyumbani kwa mwanaume). Katika kipindi chote cha mawasiliano binti alimshinikiza sana mwanaum) kufika alikopanga bila ya mafanikio, lakini mwanaume aligoma.

Siku chache kabla ya mwanaume kwenda chuo alipata shinikizo kubwa kutoaka kwa binti, hivyo akaamua kwenda, kwani aliambiwa kuna jambo muhimu sana binti anataka kumwambia. Mwanaume alifika kwa binti ili kujua alichokuwa anaitiwa. Binti alimwambia mwanaume "mimi nipo single, niliwahi kuwa na uhusiano na mkaka mmoja nikiwa chuo, na wewe ndio chaguo la maisha, nimekuwa nikikuchunguza sana tangu ile siku ya kwanza kwenye kusahihisha, naomba uwe mume wangu wa kufa na kuzikana". Mwanaume alipata wakati mgumu sana kutoa jibu na kumwambia atatoa jibu baada ya tafakari.

Mpaka mwanzoni mwa mwaka 2011 mwanaume alikuwa hajatoa jibu lolote. Hapo ndipo binti alipofanya 'ujasusi' . Binti alijua siku mwanaume anayomaliza mitahani ya UE, hivyo, alimfungia safari kutoka Morogoro hadi Moshi bila ya mwanaume kujua. Binti alimjulisha mwanaume saa nane mchana ya kwamba yupo njiani (Same) na anafuata jibu, huku mwanaume akiwa amewataarifu wazazi wake ya kwamba kesho yake angeenda nyumbani.

Mwanaume alipata mshtuko mkubwa, kwani hakuweza kumkatalia wala kumwambia mama yake ya kwamba hatokwenda kijijini. Binti alifika mjini Moshi jioni, mwanaume akamtafutia gesti na wakaanza majadiliano.

Binti alipogundua ya kwamba mwanaume atakwenda kijijini siku inayofuata, alikwenda kununua vitenge doti mbili, sukari n.k. na kumwambia mwanaume ni lazima waende wote kijijini ili apate kumsalimia mama 'mkwe'. Baada ya binti kuona mwanaume anaogopa sana na kusitasita alimwambia "naona hunitambui, tukifika kwa mama utanitambua vizuri". Walipofika kijijini, kabla ya mwanaume kumwelezea mama yake chochote juu ya uhusiano wake na yule binti, binti alipata muda wa kuongea na mama kidogo na kumpa zawadi alizonunua pamoja na hela.

Baadaye mwanaume alipomwelezea mama yake juu ya uhusiano wake na yule binti, mama alimwambia, mbele ya yule binti ya kwamba yule binti ndiyo mwali anayemtambua, kwani umri wa kijana wake ulikuwa umeenda (ana maika 30) na ajaonyesha dalili yoyote ya kuoa, pia yule binti ni sahihi kwani (ana miaka takribani 28) alikuwa tayari kuolewa na anaonekana ananidhamu (kumbuka binti alimpa mama zawadi pamoja na hela). Mama aliwaita wajomba wa wazee kadhaa ili kuwatambulisha mwali wake mtarajiwa na kuwaambia stori nzima, ndugu wote wabariki uhusiano wao.

Kwa sasa wanaendelea vizuri, pande zote mbili za wazazi zinauhusiano mzuri na wanaandaa ndoa kufunga ndoa mwakani pindi mwanaume atakapohitimu masomo.

Poleni kwa kuwachosha, kwani habari hii ni ndefu sana. Kwa wale 'single ladies' ukiona inakufaa tumia, na sisi bachelors, ikitutokea tusishangae. Naomba kuwakilisha.
 
Scofied ...."kwa wale single ladies, ukiona inakufaa chukua, kwa sisi bachelors, ikikutokea usishanage"
 
Nzuri...lakini sidhani kama hii ni mbinu ya kijasusi...mbona nyepesi hivyo? au kwakuwa amemkuta mwanaume mwenyewe naye mwepesi??
 
Huyo mwanaume inawezekana na yeye alikuwa anampenda huyo dada ila tu alikuwa domo zege! Katika hali ya kawaida, si jambo rahisi kumlazimisha mwanaume kuoa! Ni sawa na kumlazimisha punda anywe maji mtoni, hawezi kunywa mpaka amependa mwenyewe!
 
Duh, midume mingine yalainika kirahisi, mie mpaka ufike kwa mama Ni issue nzito sana.
 
Sasa intufundisha nini hiyo? tuonane na wazee na tuendelee na wabariki kuzini kwetu au?
 
huyo jamaa alikua 1st year au???mbona mbinu rahisi sana...kwani amgempotezea pale Moshi angempata wp???Unamzimia simu then unaendelea na mengine.....alimpenda tuu.....
 
Ingawa huyu binti yangu kapata alichopania, ndoa siyo jambo la kuziana ujanja. Anaweza kuwa mjanja leo kesho ikawa vinginevyo. Tumewaona wengi waliofanya hivyo mwisho ukawa mbaya. Neno ninakupenda na nitakuoa si la kulazimisha. Huja lenyewe kutokana na msukumo uliomo ndani ya mhusika. Ikitokea ukafinyangwa msukumo huo mwisho wake utakuwa mbaya tu ingawa mie si mtabiri wa mabaya.
 
Mi nimewaza labda mwanamke kamshikia jamaa bastola kumbe.....dah! Umenichosha! Hebu wataarifu mods wabadilishe hiyo title!
 
Wanaume wengi ni mpaka wakaliwe kooni na wanawake/wachumba zao ndipo wanaoa, otherwise wangependa waendelee kufanya nao uasherati tu, huku wakidhani atatokea mwanamke aliye bora au mrembo zaidi ya huyu.
Natuurallywanaume si waoaji!
 
Nzuri...lakini sidhani kama hii ni mbinu ya kijasusi...mbona nyepesi hivyo? au kwakuwa amemkuta mwanaume mwenyewe naye mwepesi??

Hii ingenoga kama ingekuwa hivi:

"Mwaka 2010 mwanamke alipata nafasi ya kujiendeleza kielimu, elimu ya Shahada, katika Chuo Kikuu kishiriki cha Mwenge kilichopo Moshi (nyumbani kwa mwanaume). Alipokuwa huko aliwasiliana na mwanaume na kumuomba amuelekeze kwao ili akawasalimie wazazi wake kama rafiki tu, mwanaume akamuelekeza. basi mwanamke akaenda kule kwa wazazi wa mwanaume na zawadi chungumzima na kujitambulisha kwamba yeye ni mchumba wa mtoto wao. wazazi wa mwanaume walimpokea kwa bashasha na binti alikarimiwa kama mwali. lakini wazazi walipowasiliana na mtoto wao, alionekana kushangaa na kukataa kuwa na uhusiano na mwanamke huyo na akadai kwamba hajawahi kumtamkia kwamba atamuoa, lakini wazazi wa mwanaume walipuuza kwa kujua kwamba kijana wao labda hajatulia na anataka kumchezea binti wa watu, hivyo hawakumweleza yule binti juu ya yale majibu ya kijana wao.

Yule binti aliendelea kuwa anakwenda nyumbani kwa wazazi wa mwanaume kila apatapo nafasi na alikuwa akienda na zawadi na pia alikuwa akisaidia kazi zanyumbani kama vile ni mtoto wa pale.

Ilitokea kijana alipata likizo hivyo akawapigia wazazi wake simu kwamba atakwenda nyumbani kwa ajili ya likizo. Binti alipoelezwa na wazazi wa mwanaume kwamba mtoto wao atakuja likizo. aliona kwamba huo ndio wakati muafaka wa kutekeleza azma yake. hivyo alikwenda kijijini siku inayofuata, akiwa na zawadi mbalimbali lakini pia alimnunulia mwanaume mashati na vitambaa vya suruali.

Baadaye mwanaume kufika nyumbani kwao alishangaa kumkuta binti kajaa tele na pale nyumbani anatambulika kama ni mchumba wake. Alipomwelezea mama yake kwamba hana uhusiano na yule binti na wala hana mpango wa kumuoa, mama alimwambia, mbele ya yule binti ya kwamba yule binti ndiyo mwali anayemtambua, kwani umri wa kijana wake ulikuwa umeenda (ana maika 30) na ajaonyesha dalili yoyote ya kuoa, pia yule binti ni sahihi kwani (ana miaka takribani 28) alikuwa tayari kuolewa na anaonekana ananidhamu (kumbuka binti alimpa mama zawadi pamoja na hela). Mama aliwaita wajomba wa wazee kadhaa ili kuwatambulisha mwali wake mtarajiwa na kuwaambia stori nzima, ndugu wote wabariki uhusiano wao.

Kwa sasa wanaendelea vizuri, pande zote mbili za wazazi zina uhusiano mzuri na wanaandaa ndoa kufunga ndoa mwakani pindi mwanamke atakapohitimu masomo."

Si mnaona jinsi ambavyo ingependeza eh....!
Sasa huu ndio tungeita ni UJASUSI.....................................LOL
 
Mi sioni kama huyo dada atafaidika na hiyo kwasababu ni yeye ndo kapenda bila kuangalia kama mwenzake anampenda au la. Yawezekana huyo kaka kakubali tu kwakulazimishwa hana mapenzi na huyo dada lakini ndi keshalazimishwa. Nahisi baadae Itamcost sana huyo dada kwa anachokifurahia leo kesho atalia na kujutia uamuzi alioufanya.:spy:u
 
zomba huwezi kuukumbatia mbuyu kwa mikono dr.slaa ni mbuyu kwako babu wewe ,alafu wewe sio msafi kivile kumwona mwenzio ni mzinzi sana zomba watu wengi tunadhambi na tunaishi kwa toba na rehema za mungu tu,kila thread unayochangia MMU lazima umtaje huyo mzee ule ni mbuyu kwako kamwe huukumbatii utabakia kutokwa povu tuuuuuu.mwenzako ashatubu wewe kila siku unapiga kichwa chini kuomba toba ila ukirudi nikuendelea kuhukumu tuu unamsaidia mungua au fanya yanayokuhusu acha ya Mungu afanye mwenyewe
 
Last edited by a moderator:
Kichwa cha habari kinasema "kuolewa" utumbo hauoneshi harusi! huyu anataka kuhalalisha zinaa hakuna zaidi.
 
Gia la Mwanamke wa kikurya kiboko na asubiri baada ya muda itabidi ajifunze boxing, maana ile ilikuwa kumbana mwanamme muoga asijaribu nje, tena mwalimu wa Sekondari za wanawake?
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom