Treni ya Mwakyembe bado sana, SUMATRA waikwamisha

Mimi kitu ambacho sijakielewa ni cha kuwa na treni moja tu asubuhi na moja tu jioni. Kutoka Ubungo hadi mjini na Mjini hadi Ubungo. Hii kweli inalipa gharama zote za miundo mbinu na uendeshaji na kuwafanya watu wawahi makazini na kupunguza msongamano? Kwa maoni yangu ningeona afadhali zingekekuwa mbili kwa asubuhi na mbili kwa jioni.

Hii inaweza sababisha nauli ziwe kubwa ili kugharamia gharama za uendeshaji labda ndio maana SUMATRA wana kigugumizi.
Tusubiri tuone kwanza tusianze kuvuka daraja kabla hatujafika.

Hili la treni moja asubuhi na moja jioni sidhani kama kweli litasaidia kupunguza foleni na msongamano wa watu kwenye madaladala ukizingatia kuwa treni yenyewe inabeba watu 950 pekee.

hapa kuna umuhimu wa mwakyembe et al wajipange vizuri ili tuone kweli matunda ya usafiri huo na impacts zake
 
Napendekeza iundwe tume kuchunguza ni kwanini treni haijaanza kubeba [si kusafirisha] abiria
 
Wabongo bwana, wote ni kama tomaso. Mkiambiwa kuwa usafiri wa treni mjini haulipi mnabisha. Gharama za uendeshaji treni ni za juu kuliko mnavyofikiri.

Ndio maana wataalam wa usafiri walipendekeza usafiri wa mabasi yaendayo haraka. Na mradi huu wa mabasi unatekelezwa kwa ufasaa na sio kwa kukurupuka kama Tren ya Mwakyembe.

Tu-unge mkono mradi wa mabasi ili utuondolee hii hadha ya usafiri Jijini Dar es Salaam.
 
Back
Top Bottom