DOKEZO Trafiki na Polisi wanaotumia pikipiki Sumbawanga wanawatesa wamiliki wa vyombo vya usafiri kwa rushwa iliyokithiri

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

JET SALLI

JF-Expert Member
Dec 1, 2014
1,992
1,197
Ndugu zangu Watanzania serikali yetu ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania inapaswa kutambua kwamba katika majeshi ambayo ni shida na mateso kwa Watanzania hususani wenye vyombo vya usafiri Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani na polisi wanaotumia pikipiki ni tatizo kubwa kwa Watanzania.

Jeshi la Polisi kupitia traffic na polisi wenye pikipiki wanafanya kazi ya kujikusanyia fedha kinyume na sheria na taratibu zilizowekwa, Watanzania wengi wanateseka sana. Leo nimepata kisa kimoja huko Sumbawanga manispaa matraffic na polisi wanaotumia pikipiki wamegawana zoezi la kukusanya fedha yaani wamekaa sehemu wanakusanya hela tu na hakuna mazungumzo ni hela tu.

Wanatesa bodaboda, bajaji na wenye magari, yaani ni Rushwa imetawala sana. Traffic na polisi hao wenye pikipiki wanafanya kazi ya kukusanya pesa zao na haziendi serikalini. Na ninaamini hili tatizo halipo Sumbawanga tu au Mkoa wa Rukwa lipo maeneo mengi ndani ya Tanzania hii.

Hivi tujiulize maswali, hivi siku Watanzania wakiasi kutokana na mateso wanayopitia nani atalaumiwa katika nchi hii, ni mara ngapi wanasheria wameshauri jeshi hili la Polisi kuundwa upya na sababu ni moja tu jeshi bado lina mkao wa kikoloni.

Ninaamini waziri anapita humu na viongozi wetu wengi tu wa serikali, jueni kwamba wananchi wanapita katika mateso na wana hasira iliyojirundika siku ikilipuka hapatatosha. Saidieni Watanzania, naamini mateso haya yako nchi nzima.
 
Sumbawanga si mnasifika kwa mambo ya uchawi ebu walazeni utupu hao maskari yani wamke wajikute sokoni wapo watupu wiki moja mfurulizo wataacha wasumbuq
 
Back
Top Bottom