TRA wanataka 18% mfanyabiashara faida 2-4%

Android 00

JF-Expert Member
May 23, 2013
774
221
Tujiulize je Hawa TRA wamewapa mitaji ya kufanya biashara hawa wafanyabiashara?

Ikiwa wao wako maofisini wanataka wakusanyiwe pesa nyingi zaidi kuliko faida anayopata mfanyabiashara kwa kila bidhaa anayouza nani tutegemee atawakubalia?

Serikali inashindana na nguvu ya umma lkn kwa hili lazima watarudi kwenye meza.

Kulikua na utaratibu wa makadirio ya kila mwaka kila mfanyabiashara, huu ulikua mpango mzuri sana lkn kwakua maofisini kumekosekana watendaji waaminifu imeonekana mashine ndio zinafaa kudhibiti upotevu wa pesa.

Wametolewa watendaji wa tra kwenda kusomea uendeshaji wa mashine Dubai na zimetumika pesa nyingi sana za walipa kodi badala yake yaneletwa mambo yasioeleweka.

Ninachopenda kuwashauri TRA kama wanapenda waendelee kukusanya kodi kwa umakini wapange safu nzur maofisini na waendelee kuwatathimini wafanyabiashara kama zamani ila sasa waje na utaratibu huu:

Duka la nguo la aina yoyote kodi ni 200000 kwa mwezi.

Duka la mchele 150000.

Duka la viatu ......

Duka la simu .......

Duka la ice cream .......

na inaendelea ivo ivo, isipokua kodi zitofautiane na maeneo ya duka lilipo.

mf: kariakoo kodi yao
mbagala Kodi yao
mwenge kodi yao
arusha kodi yao
na kwengineko.

ahsante

nawakilisha.
 
wAFANYAKAZI WANALIPA KODI INAYOLINGANA NA HIYO, KWANI HAWA TRA WALIWATAFUTIA HIZO KAZI? AU WALIWASOMESHA KWENYE HIZO PROFESHENI ZAO?? ACHENI UJANJA UJANJA LIPENI KODI.......
 
Wafanyabiashara wanaona shida kulipa kodi maana visingizio vimekuwa vinabadilika kila siku mara zina bei kubwa, mara hazirekodi manunuzi, mara 18% kodi, tupate elimu kwanza n.k
EFD imekuwa kero kwa wafanyabiashara kwasababu inatunza kumbukumbu za biashara za kila siku kwahiyo ile fursa ya kuwahonga watumishi wa TRA katika ukadiriaji wa kodi imeondolewa na wao wamezoea kukwepa kodi.
EFD inawahusu wafanyabiashara ambao hawajasajiliwa kwenye VAT ambao Mauzo ghafi yao kwa mwaka ni shilingi milioni 14 na zaidi. Kwa Nchi nzima walengwa ni kama laki mbili tu kati ya wafanyabiashara zaidi ya milioni moja na nusu ambao wamesajiliwa kulipa kodi.
Kuhusu kutozwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya asilimia 18. Sasa watatozwaje VAT wakati hawajasajiliwa kwenye VAT kodi yao ni ileile ya mapato .
Wafanyabiashara wanaogomea EFD ni wakwepa kodi mbona watumishi wanakatwa kodi hawagomi.
Hakuna nguvu ya umma katika hili kinachotakiwa ni wafanyabiashara kulipa kodi. Nguvu ya umma ni katika kusimamia matumizi ya kodi zetu.
 
Inamana kabla ya hizo mashine za EfD hao wafanyabiashara walikuwa hawalipi kodi??
Ni rahisi kukwepa kodi kwa kutumia hizo mashine kuliko tunavyodhani.

Sent from my Nokia Lumia using Tapatalk
 
Weee Asad, una miaka mingapi kwanza, usikute unamiaka 14yrs old, biashara imeanza mwaka gani tanzania? Na kama walikuwa hawalipi au wanakwepa serikali ilikuwa wapo miaka yote hiyo? Elewa kila mtu anawwza uza milioni kumi na nne ila je kwenye hayo mauzo faida yake ni ngapi? Na anampa TRA ngapi?
 
Wafanyabiashara wanaona shida kulipa kodi maana visingizio vimekuwa vinabadilika kila siku mara zina bei kubwa, mara hazirekodi manunuzi, mara 18% kodi, tupate elimu kwanza n.k
EFD imekuwa kero kwa wafanyabiasharau kwasababu inatunza kumbukumbu za biashara za kila siku kwahiyo ile fursa ya kuwahonga watumishi wa TRA katika ukadiriaji wa kodi imeondolewa na wao wamezoea kukwepa kodi.
EFD inawahusu wafanyabiashara ambao hawajasajiliwa kwenye VAT ambao Mauzo ghafi yao kwa mwaka ni shilingi milioni 14 na zaidi. Kwa Nchi nzima walengwa ni kama laki mbili tu kati ya wafanyabiashara zaidi ya milioni moja na nusu ambao wamesajiliwa kulipa kodi.
Kuhusu kutozwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya asilimia 18. Sasa watatozwaje VAT wakati hawajasajiliwa kwenye VAT kodi yao ni ileile ya mapato .
Wafanyabiashara wanaogomea EFD ni wakwepa kodi mbona watumishi wanakatwa kodi hawagomi.
Hakuna nguvu ya umma katika hili kinachotakiwa ni wafanyabiashara kulipa kodi. Nguvu ya umma ni katika kusimamia matumizi ya kodi zetu.

mbona hatuioni hio nguvu ya umma unayosimamia kodi zetu?

mbona siioni nguvu ya umma inayosimamia tembo na twiga wetu?

wewe kama so mwanasiasa ni EPA.
 
hawa wanaojidai ni waajiliwa hawajui kujitetea hivyo kwa uoga wao wasituunganishe na sie wadai haki. ikumbukwe kuwa wafanyabiashara ni kama kuku wa kienyeji kila kukicha ni kujitafutia serikari ni kama mwewe akitua ana huruma ilimradi tu vifaranga vyake wafanyakazi waneemeke. kwako wewe mfanyakazi unayetea uozo. wajua ni wafanyabiashara wangapi wanakufa kwa presha? unajua wanaofilisiwa na mabenki ni nani?
 
Wafanyabiashara wanaona shida kulipa kodi maana visingizio vimekuwa vinabadilika kila siku mara zina bei kubwa, mara hazirekodi manunuzi, maura 18% kodi, tupate elimu kwanza n.k
EFD imekuwa kero kwa wafanyabiashara kwasababu inatunza kumbukumbu za biashara za kila siku kwahiyo ile fursa ya kuwahonga watumishi wa TRA katika ukadiriaji wa kodi imeondolewa na wao wamezoea kukwepa kodi.
EFD inawahusu wafanyabiashara ambao hawajasajiliwa kwenye VAT ambao Mauzo ghafi yao kwa mwaka ni shilingi milioni 14 na zaidi. Kwa Nchi nzima walengwa ni kama laki mbili tu kati ya wafanyabiashara zaidi ya milioni moja na nusu ambao wamesajiliwa kulipa kodi.
Kuhusu kutozwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya asilimia 18. Sasa watatozwaje VAT wakati hawajasajiliwa kwenye VAT kodi yao ni ileile ya mapato .
Wafanyabiashara wanaogomea EFD ni wakwepa kodi mbona watumishi wanakatwa kodi hawagomi.
Hakuna nguvu ya umma katika hili kinachotakiwa ni wafanyabiashara kulipa kodi. Nguvu ya umma ni katika kusimamia matumizi ya kodi zetu.

Ikiwa wewe ni mtumishi wa serikal itakuwa imekupa ajira ina haki ya kukufanya inavotaka, na inahaki ya kukupangia maisha yako uishi VIP, ngese wewe
 
waendelee kuwatathimini wafanyabiashara kama zamani ila sasa waje na utaratibu huu:

Duka la nguo la aina yoyote kodi ni 200000 kwa mwezi.

Duka la mchele 150000.

Duka la viatu ......

Duka la simu .......

Duka la ice cream .......

na inaendelea ivo ivo, isipokua kodi zitofautiane na maeneo ya duka lilipo.

you-cannot-be-serious-bro.jpg
 
mbona hatuioni hio nguvu ya umma unayosimamia kodi zetu?

mbona siioni nguvu ya umma inayosimamia tembo na twiga wetu?

wewe kama so mwanasiasa ni EPA.

wafanyabiashara wengi elimu ni tatizo na hujuma za wafanyakazi wa TRA ndizo zinakwamisha matumizi ya mashine hizi.
 
Wapi Minja Johnson men ulitakiwa kupewa kile kiti kikubwa cha TRA u rock president please meet the guy anaipenda nchi yake, linda uhai wake please
 
Wafanyabiashara wanaona shida kulipa kodi maana visingizio vimekuwa vinabadilika kila siku mara zina bei kubwa, mara hazirekodi manunuzi, mara 18% kodi, tupate elimu kwanza n.k
EFD imekuwa kero kwa wafanyabiashara kwasababu inatunza kumbukumbu za biashara za kila siku kwahiyo ile fursa ya kuwahonga watumishi wa TRA katika ukadiriaji wa kodi imeondolewa na wao wamezoea kukwepa kodi.
EFD inawahusu wafanyabiashara ambao hawajasajiliwa kwenye VAT ambao Mauzo ghafi yao kwa mwaka ni shilingi milioni 14 na zaidi. Kwa Nchi nzima walengwa ni kama laki mbili tu kati ya wafanyabiashara zaidi ya milioni moja na nusu ambao wamesajiliwa kulipa kodi.
Kuhusu kutozwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya asilimia 18. Sasa watatozwaje VAT wakati hawajasajiliwa kwenye VAT kodi yao ni ileile ya mapato .
Wafanyabiashara wanaogomea EFD ni wakwepa kodi mbona watumishi wanakatwa kodi hawagomi.
Hakuna nguvu ya umma katika hili kinachotakiwa ni wafanyabiashara kulipa kodi. Nguvu ya umma ni katika kusimamia matumizi ya kodi zetu.

Katika kutafuta maisha mimi nimeshafanya biashara na mpaka sasa nafanya japo si kwa kiwango cha zamani. Labda niseme tatizo lipo kwenye UKUBWA WA KODI ambayo mfanyabiashara anatakiwa kulipa. Hili ni tatizo la muda mrefu lakini wafanyabiasha hawajawahi kulalamika kwa sababu miaka nenda miaka rudi wamekuwa wanakwepa kulipa kodi halisi. wafanyabiashara wengi kwenye maduka kama Kariakoo wanakuwa na vitabu viwili vya risiti, kimoja halali na kingine haramu. Sasa hizi mashine zimeziba huo mwanya, kwa hiyo watu sasa wanaanza ku-feel ile ''nguvu'' ya ukubwa wa kodi. Kusema ukweli sababu zinazotolewa na wafanya biashara zote ni za UONGO ila sababu kubwa ni kuwa UKILIPA KODI KADIRI INAVYOPASA faida itakuwa ndogo sana au hakuna kabisa. Naona wangeeleza tu ukweli na sio kuzunguka zunguka mbuyu
 
Mashine zinazuiya WIZI wa kodi ndiyo maana wafanyabiashara wanaziogopa, mimi niko upande wa serikali, tatizo siyo mashine, tatizo ni MFUMO WA KODI, mashine ni sawa na mtumishi mwaminifu asiyedanganyika, mliozowea kukwepa kodi huu ndiyo mwisho wenu, kodi inalipwa na mwananchi mlaji wa mwisho kabisa, nyie ni mawakala tu kusanyeni pesa muipelekee serikali, anayetakiwa kulia ni mwananchi siyo mfanyabiashara. Serikali imeshaonesha msimamo wake, anayeona anaweza kuendelea na biashara aendelee, anayeona mashine ni kikwazo AACHE BIASHARA! Na wanaoshabikia ni watu ambao hata hhizi mashine haziwahusu, wafanyabiashara wa kweli tayari walishanunua mashine toka awamu ya kwanza! TUDAI RISITI ZA MASHINE, KODI NI JUKUMU LETU SOTE, MBONA WAFANYAKAZI HAWAANDAMANI JUU YA KODI?!!
 
Katika kutafuta maisha mimi nimeshafanya biashara na mpaka sasa nafanya japo si kwa kiwango cha zamani. Labda niseme tatizo lipo kwenye UKUBWA WA KODI ambayo mfanyabiashara anatakiwa kulipa. Hili ni tatizo la muda mrefu lakini wafanyabiasha hawajawahi kulalamika kwa sababu miaka nenda miaka rudi wamekuwa wanakwepa kulipa kodi halisi. wafanyabiashara wengi kwenye maduka kama Kariakoo wanakuwa na vitabu viwili vya risiti, kimoja halali na kingine haramu. Sasa hizi mashine zimeziba huo mwanya, kwa hiyo watu sasa wanaanza ku-feel ile ''nguvu'' ya ukubwa wa kodi. Kusema ukweli sababu zinazotolewa na wafanya biashara zote ni za UONGO ila sababu kubwa ni kuwa UKILIPA KODI KADIRI INAVYOPASA faida itakuwa ndogo sana au hakuna kabisa. Naona wangeeleza tu ukweli na sio kuzunguka zunguka mbuyu

Umenena hakika kabisa mkuu, wengi tumepita huko, mimi nimejifunzia biashara kwenye kampuni ya wageni, kodi tuliyokuwa tunakwepa haisemeki, hata mimi nilivokuja kuanza kazi za uchuuzi za binafsi nilikopi tu mbinu za ukwepaji na kuzihamishia kwangu, TATIZO WALA SI BEI ZA MASHINE, TATIZO MASHINE ZINABANA UKWEPAJI (japo zinachakachulika pia)
 
umesema ukweli lkn bado huko muwazi, iweje ujifunze kuiibia serikal kulipa kodi kwenye vitabu uje ushindwe kuidanganya kwenye mashine, unajua nikwambie kinachotafutwa ni haki na si dhihaka.

Kama ni mashine hata wachina hawashindwi kutoa kopi na karatasi kama hizo ambazo wanazotoa hao TRA na wafanyabiashara wakaendelea kukwepa kama kawaida.
 
Kuhusu kutozwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya asilimia 18. Sasa watatozwaje VAT wakati hawajasajiliwa kwenye VAT kodi yao ni ileile ya mapato .
Hizi mashine ni 'automatic'.. Ukipitisha ile 'threshold' ya kukadiriwa kodi (mapato ghafi ya zaidi ya Shilingi milioni 40), inakusajili moja kwa moja kama mlipaji wa Kodi ya Ongezeko la Thamani(VAT). Kwa hiyo haihitaji ofisa wa TRA kuja kukusajili.
Na pia unaposajiliwa VAT moja kwa moja unakuwa wakala wa TRA wa kukusanya kodi hiyo ya 18%.
Hii ni kiboko ya wafanyabiashara wakwepa kodi.
Lakini ni kukosa uelewa tu.. unaweza kukwepa kodi kwa urahisi kama ukisajiliwa VAT, sawa na makampuni makubwa. 'Just' kucheza na sheria zilizopo..
 
The bottom line ni kwamba EFD zinaziba loopholes zote za ukwepaji kodi hizo kelele nyingine ni propaganda tu.Eti mtu yuko k.koo bado ana complain 18% hata aibu haoni mbna before kuambiwa anunue mashine alifanyiwa assesment na bado akalipa 18% kwenye return zake mbna hawakugoma toka mwanzo the only difference ni kwamba mwanzo hawakufeel tax burden coz loopholes zilikua nyingi lakini sasa mashine inaziba so lazima atafeel tax burden.LIPA KODI KWA MAENDELEO YA TAIFA
 
Kulikua na utaratibu wa makadirio ya kila mwaka kila mfanyabiashara, huu ulikua mpango mzuri sana lkn kwakua maofisini kumekosekana watendaji waaminifu imeonekana mashine ndio zinafaa kudhibiti upotevu wa pesa.

Wametolewa watendaji wa tra kwenda kusomea uendeshaji wa mashine Dubai na zimetumika pesa nyingi sana za walipa kodi badala yake yaneletwa mambo yasioeleweka.

Ninachopenda kuwashauri TRA kama wanapenda waendelee kukusanya kodi kwa umakini wapange safu nzur maofisini na waendelee kuwatathimini wafanyabiashara kama zamani ila sasa waje na utaratibu huu:

kiongozi,
hapo ktk watendaji wa aaminifu, ni kweli lakini cku hizi ukiwa mwaminifu unaonekana wa Zamani.

pia hawa TRA wangekuwa wanaelimisha jamii kwanza kabla ya utekelezaji wa gafla.
 
Back
Top Bottom