TRA wanataka 18% mfanyabiashara faida 2-4%

Inamana kabla ya hizo mashine za EfD hao wafanyabiashara walikuwa hawalipi kodi??
Ni rahisi kukwepa kodi kwa kutumia hizo mashine kuliko tunavyodhani.

Sent from my Nokia Lumia using Tapatalk

Hata kama ipo mbinu ya kukwepa kodi kwa kutumia hizi mashine lakini KUKAMATIKA NI RAHISI SANA, na utakapokamatwa ukwepaji wako wako kona utajionyesha in detail in terms of amount and time. Hili ndilo linalowaogopesha wafanya biashara.
 
Tatizo letu kubwa ni kuwa kila mtu ni mwanasiasa, hivi hiyo 18% unayoizungumzia si ni VAT? Hiyo inalipwa na mfanyabiashara au mnunuzi? Mbona hutoi mifano ya PAYE? Au mfanyakazi tu ndio alipe kodi huyu mfanyabiashara aachwe tu? Sio kila kitu cha kupinga jamani, tuondoe mentality hii....
 
ukiuza toa risiti,
ukinunua dai risiti
TRA pamoja tunajenga taifa

yaani nilipo soma ID yako na comment yako.
nimecheka mpaka basi....... maana ni wa Tz wachache sn, wanadai risiti
wengi hawajari hasa kipindi hk cha privatelization,

hizo mashine nyingi hazitumiki sababu wanunuzi hawajali risiti
 
Katika kutafuta maisha mimi nimeshafanya biashara na mpaka sasa nafanya japo si kwa kiwango cha zamani. Labda niseme tatizo lipo kwenye UKUBWA WA KODI ambayo mfanyabiashara anatakiwa kulipa. Hili ni tatizo la muda mrefu lakini wafanyabiasha hawajawahi kulalamika kwa sababu miaka nenda miaka rudi wamekuwa wanakwepa kulipa kodi halisi. wafanyabiashara wengi kwenye maduka kama Kariakoo wanakuwa na vitabu viwili vya risiti, kimoja halali na kingine haramu. Sasa hizi mashine zimeziba huo mwanya, kwa hiyo watu sasa wanaanza ku-feel ile ''nguvu'' ya ukubwa wa kodi. Kusema ukweli sababu zinazotolewa na wafanya biashara zote ni za UONGO ila sababu kubwa ni kuwa UKILIPA KODI KADIRI INAVYOPASA faida itakuwa ndogo sana au hakuna kabisa. Naona wangeeleza tu ukweli na sio kuzunguka zunguka mbuyu

Big 'LIKE'
 
Jamani Lipeni kodi tuendeshe nchi!! tena ni vema hizo mashine ziwepo hadi bar!!
 
Kinachotakiwa ni elimu kwa mlipa kodi itolewe, mtu aone umuhimu wa kurequest TRA receipt kila anapofanya manunuzi, kwa sababu anaelipa kodi si mfanya biashara anaelipa kodi ni mwananchi ( end user) mfanyabiashara anachofanya ni kukusanya kodi kwa niaba ya TRA kwa kila kitu anachouza, napendekaza pia TRA waje na kodi ya kuwakata wafanyabiashara (Pay e) apa namaanisha baada ya kupeleka kodi walizokusanya kwa niaba ya TRA faida wanayopata wakatwe pay e, mfano mzuri ni kwa mfanyakazi analipa pay e na akinunua kitu kwa mfanya biashara analipa tena VAT, tufike mahali tuone umuhimu wa kulipa kodi tuache siasa.
 
Hivi karibuni tumeshuhudia migomo ya wafanyabiashara ktk mikoa mbalimbali humu nchini. Mtu makini anaweza akajiuliza kulikoni mtu aache kufanya shughuli halali zinazomuingizia kipato na kuna uhusiano gani kati ya mlipakodi, TRA na mashine za EFD ? Bila shaka lipo tatizo linalohitaji suluhisho

1 Nani ni mlipa kodi halisi? Bila shaka mlipa kodi halisi ni kila mwananchi au mlaji anunuapo bidhaa yoyote isiyokua na msamaha wa kodi
2 Nani hasa ni wakala wa kukusanya kodi toka kwa mwananchi/mlaji na kupeleka TRA? Bila shaka hili ni jukumu la wafanyabiashara

TRA ni nani? Hiki ni chombo au mamlaka iliyoundwa kisheria na serikali ili kuratibu mipango ya kukusanya ushuru na kodi mbalimbali ili kuwezesha gharama kuendesha serikali.

CHANGAMOTO
Yapo matatizo mengi yanayolalamikiwa na wafanyabiashara kama
-Kukosa uaminifu kwa baadhi ya maafisa wa TRA ambao hutoza au kumkadiria mfanyabiashara kiasi kikubwa cha fedha ili kulazimisha/ kushawishi utoaji rushwa na hivyo ni kiasi kidogo kinachofika serikalini

-Mfumo au fomula ya kodi ya ongezeko la thamani (18%VAT) bidhaa moja yaweza kulipiwa zaidi ya 54% yaani
(A)Kiwandani-ajent/jumla 18%
(B)Jumla-Rejareja 18%
(C)Rejareja-mlaji 18%
Zote hizi pamoja na nyinginezo ni kodi ambazo mwisho wa siku hubebwa na mlaji

-Mashine za EFD ambazo mfanyibiashara analazimishwa kununua tena kwa bei mbaya ni vitendea kazi vya TRA vilivyostahili kutolewa bure

-Kodi itozwe kutokana na faida aipatayo mfanyabiashara na sio mauzo nk.
NATOA RAI KWA SERIKALI KUSIKILIZA PIA MAONI YA WAFANYABIASHARA ILI WALIPE KODI YA HAKI.
 
Back
Top Bottom