TRA wagonga hodi kwa Wakulima

Ndo maana tunasema tanzania upinzani ulishakufa ,hivu hii nguvu mnayoitumia kuonesha wakulima wazalendo watanzania kuwa wanaonewa na serikali yao, kwanini msingeitumia kuwaelimisha umuhimu wa kuchangia au kulipa kodi kwa moyo mkunjufu maana wao ni jukumu lao kujenga nchi sababu ni watanzania na nchi haiwezi jengwa na na watu wa nchi jirani?
Serikali imewajengea uwezo hao wakulima unaosema wanatakiwa kuijenga nchi yao?
 
Baada ya matajiri kuisha sasa ni zamu ya wanyonge kulipa kodi na kufilisiwa. Kwani nasema uongo ndugu zangu?
Kwahiyo aliyeandikiwa hiyo barua ni mnyonge ausio!? Acheni ushabiki wa kijinga; tembelea Mang'ola uwaone mabwanyenye. Utaratibu wa wenye mashamba makubwa kulipia kodi ya mapato upo siku zote na ukifuatilia barua hiyo anapewa maelekezo ambayo alitakiwa kuwa ameyatekeleza kabla ya hiyo notice.

Anyway, lazima tulipe kodi ili tuweze kujitegemea; endeleeni kutegemea ubeligiji.
 
Kinachwauma wadau wengi hasa wadogo wadogo ni kodi kukusanywa kwenye penalties na sio mapato
Nakupa mfano:
HUYO MWENYE SHAMBA HUENDA AKAWA NA SUPERVISOR MMOJA NA WAFANYA KAZI WATATU kila mmoja anamlipa 50,000 kwa mwezi.

Kodi ya SDL inatakiwa kulipwa na mwajiri mwenye wafanyakazi wanne, ila wafanyakazi wa mashambani wako excluded (direct shamba boys) ila sio supervisor. Kitakachomkuta ni hiki:
Mishahara 4 x 50,000= 200,000
SDL tax ( 200,000-150,000)x 4.5%=2250

Kimbembe kinaanzia hapa: 2250 x 12 (mwaka)=27,000
Penalty 225000 x 12= 2700,000
Hiyo nimekupa hesabu ya SDL kwa mwaka mmoja, interest inategemea BOT rates. Sasa imagine miaka kumi hajalipa.

KINACHOWAUMA WADAU NI KODI KUBWA KUWA INALENGWA NJE YA FAIDA.
Penalty ya 2,700,000 kwa kushindwa kulia 27,000.

Yaani wakukute kuna kikorokoro kidogo let say with hold tax ya 8000, yaan ulilipia professional service flan tuseme miaka 5 iliyopita ukasahau au ukaacha kulipa hiyo kodi ya zuio 8000 maana yake ni 8000 x interest ya BOT
MZIKI WA PENALT 225000 X 12X 5=13500,000....

ALL IN ALL TULIPE KODI ila nao watunzi wa sheria za kodi wajitadhmini
Kwahiyo aliyeandikiwa hiyo barua ni mnyonge ausio!? Acheni ushabiki wa kijinga; tembelea Mang'ola uwaone mabwanyenye. Utaratibu wa wenye mashamba makubwa kulipia kodi ya mapato upo siku zote, na ukifuatilia barua hiyo anapewa maelekezo ambayo alitakiwa kuwa ameyatekeleza kabla ya hiyo notice.

Anyway, lazima tulipe kodi ili tuweze kujitegemea; endeleeni kutegemea ubeligiji.
 
Mkuu hivi unawafahamu wakulima kweli?Wakulima huuza mazao yao wakati mwingine yakiwa bado shambani.Hao wanaotunza stock ya mazao ni wafanya biashara au wachuuzi wa mazao.Mfano kule Kahama kuna wafanyabiashara wakubwa wanama godown ya kuhifadhi mpunga hata miaka mitatu wakisubiri bei ipande.

Wakulima wengi hawawezi kuwa na uwezo huo wa kuvumilia bei ipande
Hata hivyo hao si walishalipa ushuru wakati wananunua?.
 
Ieleweke tu kwamba hakuna jiwe litasimama bila kugeuzwa....

Target ni 2 trillion per annum, tutakoma mwaka huu. Bado kodi za birthday, ushereheshaji, kashata na kahawa, machinga, gengeni, usukaji nywele, upakaji ina, upakaji wanja kukata nyusi na rangi kwa kina mama! Ndio, hiyo ndiyo TRA yetu, wavivu wa kufikiri, kupenda kuumiza watu wa vipato vya chini na kupenda vya kunyonga...

Hapo utaambiwa anayeshauri hayo ana Masters ya Tax!
Hakuna kufikiri nje ya box wala nini, vihiyo wa ukweli..
 
Uzuri upotoshaji mara nyingi huwa upo kwenye media tu hasahasa social media tu.
John piga kazi usigeuke nyuma.
 
Umenena vyema japo wapo wakulima wa aina nyingi. Huwezi kusema sumry Ncha Kali aliyelazimika kuachana na biashara ya mabasi akaingia ktk kilimo hana uwezo wa kusubiri bei!!!!! Vivyohivyo kwa mtoto wa mkulima mr kayanza.

Huyo unaye ona kalimwa barua ujue TRA wamesha fuatilia mwenendo na wanajua anaendeshaje kilimo chake. Tusicho kijua ni kwamba huwenda pia wamesha nusa mamilioni kwenye account yake.

Kumbuka hao jamaa hawajihangaishi bila kunusa kuwa mahala fulani wanaweza kupata chochote. Ukisha sikia kaambiwa miaka mitatu ujue mamilioni yanamhusu.

Kumbuka ya st. Jude school.
Nilitaka kutafutia hati shamba langu, ngoja niache tu. Nimekuwa na vibarua kati 10-40 wakati wote, japo sijawahi kupata chochote. Nimetumia zaidi ya shilingi milioni 800. Kwa hali inavyoenda, ni aheri kusimama kwanza. Umepoteza hela, halafu hawa maharamia TRA wanaweza kuja kubambikia kodi ya ajabu.

Ni kubakiza tu walinzi kama watano, wote ndugu basi. Walinde kama shamba la familia.

Mungu akitujalia uhai, maendelezo yafanyike baadaye. Kwa sasa kuviziana kumezidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa tafiti za kitaalam na kwa uzoefu, hakuna faida unayopata kwa kufanya kilimo cha mazao ya chakula na hiyo ni kwa Dunia nzima. Ndiyo maana mataifa ya wenzetu, wakulima wa mazao ya chakula hupewa ruzuku.

Tanzania, ruzuku hakuna. Pembejeo bei juu. Miundombinu ya mashambani hakuna. Halafu eti wahuni wa TRA wanataka mkulima alipe kodi. Wakazane kudai na kuwabana wakulima, jibu litapatikana mapema sana. Lazima kutatokea upungufu wa chakula, mfumuko wa bei utapaa. Na kila mmoja atalalamika maradufu ya sasa kuwa maisha magumu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na kodi ya baiskeli wasisahau pia.
Warudishe kodi ya kichwa, waanzishe kodi ya kichwa kwa wanyama - ng'ombe, mbuzi, nguruwe, kondoo, mbwa, paka, kuku, sungura, kanga, na njiwa. Pia waanzishe kodi ya gurudumu itakayohusu baiskeli na mikokoteni yote.

Lazima miradi wa reli, bwawa la Nyerere ba ununuzi wa ndege, ikamilike.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo kitu nzuri sana inakuja kuwalinda wafanyakazi maana watalipa Kodi kwa Tin number hivyo itabidi wapewe mikataba.
 
Warudishe kodi ya kichwa, waanzishe kodi ya kichwa kwa wanyama - ng'ombe, mbuzi, nguruwe, kondoo, mbwa, paka, kuku, sungura, kanga, na njiwa. Pia waanzishe kodi ya kurudumu itakayohusu baiskeli na mikokoteni yote.

Lazima miradi wa reli, bwawa la Nyerere ba ununuzi wa ndege, ikamilike.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio sera za ufipa
 
Huku no sawa na kukama ng'ombe maziwa bila huduma yakinifu . ( Utatoa damu mwisho was siku)
Mkulima huyu amejengewa mazingira Bora ya kilimo?
Anapatiwa masoko?
Mpunga mpka Sasa upo maghalani Bei no sawa na kipindi Cha mavuno, serikari haishughuriki na chochote.

Wakulima wengi ni wadogo wadogo hawana hata uwezo wa pump ndogo za maji ili kumwagilia, Sasa ivi wanaangalia mawingu.

Alafu unataka kumtoza ushuru kwa kipato gani, kwa huduma gani anazopata toka serikalini?
Mkuu hapa haongelewi mkulima mdogo mdogo, huyo anayeongelewa ni mwekezaji tena ameajiri wafanyakazi kwenye shamba lake, ndio aachwe asilipe kodi???
 
Bado wabeba mizigo nao wajiandae

Au nasema uongo ndugu zanguu
 
Ieleweke tu kwamba hakuna jiwe litasimama bila kugeuzwa....

Baada ya hapo kifuatacho eti sijui umebeba Vigunia vyako vya mchele kutoka Igunga unakuja kuzunguusha Tandale Sokoni, angalau ili watoto waende chooni mara paap unashusha tu Vigunia vyako TRA hao wanataka risiti ya efd huna faini milioni tatu wakati mtaji wa hiyo biashara hata milioni haufiki

MAENDELEO YANA CHAMA ILA SIO CCM!!!
 
Back
Top Bottom