Rais Samia umetuteIekeza Wakulima wa Korosho?

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,277
6,673
Kama kuna Kipindi mkulima wa Korosho amepitia au anapitia mateso mheshimiwa Rais basi ni hiki Kipindi chako, huenda kuna mambo mengi unadanganywa na hawa uliowafanya Kuwa wasaidizi wako.

1. Bei za korosho zinashushwa Kiholela bila sababu za msingi.

2. Vyama vikuu vya ushirika hususani Tanecu Vinachelewesha makusudi malipo ya wakulima jambo ambalo linaaminika Kuwa na uchakachuaji ndani yake, mfano ... Unaweza kukuta mnada wa 3 una bei 4, 2050, 1995, 1960 na 1902 hapa Tanecu wanachakata na wengi wanalipwa 1902.

Rais, Ucheleweshaji wa malipo unawakwamisha wakulima ambao wanataka waanze maandalizi ya mashamba yao Kwa wakati.

Rais, Tunakuomba Ukutane na wakulima moja Kwa moja wakueleze madhila yao ili uone namna ya KuwaSaidia.

Mwisho tunakuomba sana mheshimiwa Raisi Uivunje hii Tanecu Kwani licha ya uchakachuaji nilioutaja hapo juu inazidiwa majukumu. Tunaomba Kuwe na TACU na NECU.

Rais tunakuomba uitumie Takukuru kuchunguza mali za Watendaji wa Tanecu na watu wa Karibu yao, wachunguzwe Pia Maafisa ushirika namna wana vyosimamia zao hili.
 
Shida ya Samia hasikilizi ushauri,yeye anaamini Watendaji wake wakati 90% ni wezi.Lile dongo la JK juzi linamuhusu yeye!
 
R.I.P Magufuli

Kipindi chako wakulima wa korosho tulineemeka hadi tukawa tunawanunulia soda mbuzi.
 
Nimefanya Sana biashara ya kununua korosho Kwenye kangomba lkn faida zake zimekuwa hasara Tu na sitaki tena kufanya biashara hiyo.

Mwaka 2021 nilikodi shamba ikawa kidogo kuna unafuu Fulani ya faida Ila Kwa kifupi biashara ya korosho ni pasua kichwa Sana hasa Kwa MTU mwenye mtaji mdogo
 
R.I.P Magufuli

Kipindi chako wakulima wa korosho tulineemeka hadi tukawa tunawanunulia soda mbuzi.
Kipindi Cha Magufuli ndio zao la korosho lilikumbwa na janga, ikiwemo kuwapora 200b zao za mfuko wa korosho. Tunamshukuru Mungu kwa kutuondolea kiongozi yule muovu.
 
Nape hawasaidii?
Yeye na chama chake ni sehemu ya tatizo la hilo zao la korosho. Na ukifuatilia vizuri usishangae kukuta baadhi ya makampuni yanayonunua korosho huko na kulalia wakulima, yeye ana mkono wake humo.
 
Back
Top Bottom