Toothless TAKUKURU: Uchaguzi UVCCM watawaliwa na rushwa na vurugu

Babu rushwa, baba rushwa, watoto rushwa na wajukuu rushwa waaache wamalizane wenyewe chama cha rushwa hicho bila pesa hauwezi kuwa kiongozi kwa kina magamba bila pesa
 
Kurudiwa uchaguzi hilo haiwezekani kwa kuwa haitabadili matokeo yoyote kama mgombea aliyeshinda alitoa rushwa, labda kama wapiga kura nao wawe watu wengine kabisa.

Yaliyotokea Arumeru Mashariki wakati wa uteuzi wa Sioi yalikuwa funzo kubwa kwa JK kuwa mbegu ya rushwa aliyoipalilia katika chaguzi za CCM imemea vizuri na haitang'oka tena!!
 
Kumekucha dodoma,mwenye kisu ndiye anakula nyama,wengine mtaishia kunawa.CCM CHAMA KUBWA LA MAFISADI NA WALA RUSHWA!
 
Hata uchaguzi huo urudiwe mara ngapi ni kazi bure tu. Kwa kuwa wapiga kura ni walewale na wagombea ni haohao matokeo yatakuwa ni hayohayo piga ua. Kura tayari zimekwisha uzwa na kununuliwa. CCM ilikufa na Mwalimu mwaka 1999. CCM hii ya sasa ni kitu kingine kabisa.
 
Kuna msemo wa kiha usemao "Inthozi zigomba guhona zimela amoya"...yaani siafu wanapokaribia kufa huota manyoya!! Sasa ndo haya manyoya yanaota CCM na Mwenyekiti anazidi kutia lishe ili yaote haraka haraka (ref. Hutuba yake kwa UWT, badala ya kuchukua hatua yeye anacheka nao). Waacheni wazikane tu kwani na wakubwa mwendo si ndo huohuo??
 
Wakuu mlioko karibu na tukio tunaomba mtupie picha za hayo matukio ili tuburudike zaidi.
 
UWT nako kulikuwa na malalamiko ya rushwa kama UVCCM wanakataa uongozi mpya hata UWT walitakiwa kufanya hivyo chama ni kimoja maamuzi lazima yafanane.

Madhara ya huu uchaguzi utayaona ukikaribia uchaguzi mkuu wa 2015. Kamba hukatikia pembaa. Kama KANU naona yanakaribia CCM.
 
Rushwa kitu kibaya sana! Ukiingia madarakani kwa misingi ya rushwa ni ngum sana kukemea rushwa. Hivi TAKUKURU Kazi yao ni kudeal na rushwa uchwara!
 
Hivi Kweli Kuna Kijana ambaye akili Yake inafanya Kazi sawa sawa bado yupo na Gamba?? Achanene nao Hao!! sasa wamekula rushwa wanategemea nini?
 
Naombeni matokeo ya Le Mutuz kama naye kashinda au kapigwa nyama chini!
 
Hawa jamaa zangu wananifurahisha kweli,baada ya kulishwa vitumbua huko nzega na bastola kulindma,dom sijui wanapewa nini na huko tusitegemee bastola tena wanaweza wakatumia ata mabomu au vifaru
 
Back
Top Bottom