nipeukweli
JF-Expert Member
- Jul 16, 2012
- 656
- 348
habari zenu wadau...
hivi ni athari zipi zilizopo wapenzi wanapokuwa na tofauti za kiuchumi/kifedha? tafakari mfano huu...
kuna kijana na binti wanapendana sana, yaani saaaana. kijana ni mtu aliyefanikiwa sana kifedha mapema, amesoma ana nyumba kadhaa, magari na mali zinginezo za kuhamishika na zisizohamishika. mbali na juhudi zake za kimaisha, kijana anatokea familia inayojiweza sana. Binti amemaliza chuo kama miaka miwili iliyopita na anafanya shughuli zake bila kutegemea network ya kijana. kipato cha binti ni cha kawaida (wastani wa laki 5 kwa mwezi) na anatokea familia ya kipato cha kati.
wawili hawa wanataka kufunga pingu za maisha ila wazazi wa kijana wanatia ngumu kwasababu binti hatoki katika familia yenye daraja lao la kifedha.
swali langu; kwani huo utofauti wa kifedha baina ya hao wawili au familia zao unaweza ukawa na athari zipi katika ndoa yao?
karibuni tujadili....