To KUB Mh. Mbowe

Ajabu
  1. Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bunge Hayupo wala msaidizi au aliyeteuliwa (maana J3 alkua Zitto) kwa kweli hawatutendei haki maana hii ni fursa adhimu
  2. Mpaka sasa hakuna swali kuhusu mgomo wa madaktari
  3. Karibu maswali yote spika anasema ni very specific
  4. Maswali ysiyo na mshiko yanaulizwa
  5. ...................kwamba bado kipindi hiki kipo......................hakina mshiko kwa watanzania
  6. Waziri Mkuu anasema mimi si waziri wa mambo ya ndani, mimi ni Waziri Mkuu........!!!! ameshindwa kujibu swali la machali.......najiuliza maana ya WAZIRI MKUU...najiuliza pia kwamba siku hizi hakuna VIKAO VYA BARAZA LA MAWAZIRI?
  7. ...ni kushangaa tu hiki kipindi....HAKINA MVUTO
ivi jamani makamanda mko wapi? Nafasi yakumuuliza maswali pm ndo hii..
 
Leo alitakiwa awe wa kwanza kuuliza maswali kwa waziri mkuu, na hasa suala la POSHO na MGOMO WA MADAKTARI ila SPIKA kasema Mbowe hayupo , najiuliza amekwenda wapi kama sio hujuma hiii,

ana kuhujumu kivipi?uwe unafikiria kabla ya kuandika.kamanda wa anga tunamwamini sana na daima akiwa kamanda mkuu pamoja na wengine wenye upeo na nia njema CDM itakuwa salama na daima watz wenye mapenzi mema watasema IN CHADEMA WE HOPE AND TRUST.kwanza kuna taarifa kuwa yuko safarini, after all asiyekuwepo ni mbowe na sio kiongozi wa upinzani kwani kuna naibu wake na anafuatia mnadhimu mkuu na halafu kiongozi wa cdm bungeni.kwa maana hiyo wa kuwabana kama wapo bungeni ni zitto,lissu na mnyika.
 
Napata hisia kuwa UPINZANI uona ni kupoteza muda na energy kumuuliza PM maswali kutokana na majibu yake ya aina moja kwa maswali yote..!

ivi mtu hanaga majibu zaidi ya ooh serikali ipo kwenye mchakato...... ooh tunalishugulikia...... ooh serikali italifuatilia...! na mambo ya kuita watu wajomba, shangazi na rafiki... wakati watu wako kazini.
 
Hivi kwa mtizamo wa haraka, maswali ya papo kwa papo kwa WM yameleta ama yana tija gani kwa Taifa letu. Msisahau kuwa ni WM huyu huyu aliyetoa machozi mbele ya wabunge wakati wa kipindi hicho cha maswali na watu wengi wakashauri kuwa ni bora hiyo session ya maswali kwa WM ikaondolewa kwa kuwa inamdhalilisha.

Kwa maoni yangu, session zote za maswali bungeni zingefutwa ili kupunguza muda wa wabunge kukaa hapo Dodoma na hii ingepunguza gharama ambazo sio za muhimu na fedha zinazotumika kuwalipa zingeelekezwa kwenye sekta nyingine za muhimu kama elimu na afya.
 
Ndugu zangu hatuna tena bunge! Maswali kwa waziri mkuu yanapangwa? Mbona hakuna mbunge aliyemuuliza huyu bwana juu ya hizi hot issues.... mgomo wa madaktari na posho za wabunge? Hizi issues Waziri mkuu kachichanganya na anatakiwa atoe maelezo...hakuna aliyemuuliza! Kwa kweli bunge linenishtua kwa jinsi linavyoenda!
 
nilijua tu nilivyoona ile thead yako ya zito nikajua kwamba wewe ni wale wale wliokunywa uji wa mgonjwa.

hivi leo chadema inaweza kuivunia nini? madaktari walikuwa online tv ili kuona msimamo wa chadema. kumbe holaaaaaaaaaa.
 
Inaonekana suala la POSHO limewashock sana Wabunge (sitangulizi wah makusudikaly.) ...yaani wanaonekana na mawazo sana.....nadhani kila mmoja alishaandaa MPANGO MKAKATI.............sasa umeyeyuka....

Maswali NANE yameisha kwa kweli ni synonimous na kipindi cha kawaid cha maswali kwa mawaziri.................NAANZISHA KAMPENI YA KUDAI KIPINDI HIKI KIFUTWE............
 
Leo Mbowe alitakiwa awe wa kwanza kuuliza maswali kwa waziri mkuu, na hasa suala la POSHO na MGOMO WA MADAKTARI ila SPIKA kasema Mbowe hayupo , najiuliza amekwenda wapi kama sio hujuma hiii,

ameanza kupenda safari kama mwenyekiti wa ccm,nasikia kaacha kampeni uzini kakimbilia marekani!
 
Ajabu
  1. Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bunge Hayupo wala msaidizi au aliyeteuliwa (maana J3 alkua Zitto) kwa kweli hawatutendei haki maana hii ni fursa adhimu
  2. Mpaka sasa hakuna swali kuhusu mgomo wa madaktari
  3. Karibu maswali yote spika anasema ni very specific
  4. Maswali ysiyo na mshiko yanaulizwa
  5. ...................kwamba bado kipindi hiki kipo......................hakina mshiko kwa watanzania
  6. Waziri Mkuu anasema mimi si waziri wa mambo ya ndani, mimi ni Waziri Mkuu........!!!! ameshindwa kujibu swali la machali.......najiuliza maana ya WAZIRI MKUU...najiuliza pia kwamba siku hizi hakuna VIKAO VYA BARAZA LA MAWAZIRI?
  7. ...ni kushangaa tu hiki kipindi....HAKINA MVUTO

Unashangaa nini wakati tunaongozwa na serikali inayoshangaa?
 
Ivi uyu madam spika ananini lakini?maswali anaulizwa waziri mkuu yeye anatetea eti swali liko specific. Mama ovyo sana. Mwache ajibu si kajitosa anajua kila kitu..mama ovyo sana

Ni matokeo ya dual loyalty: anashindwa kujielewa nafasi yake ni nini, anataka kuwa serikalini na hapohapo awe spika
 
Mkuu tupo kwenye mazungumzo ya muafaka hivyo si busara kuiuliza serikali maswali chokonozi. Hali ya hewa inaweza kuchafuka katika mazungumzo yanayoendelea kati ya Serikali na CDM. Mazungumzo bwana inabidi KUB ale kona.
 
Ni aibu wabunge wetu hawajui aina gani ya maswali ya kisera, wapitie hata JF basi leo kuna swali aliomba Mtanzania haswa liulizwe na KUB Mh.Mbowe kwa kuwa Mbowe hayupo basi mbunge mmoja angeweza kuliuliza kuliko kuja na maswali ya soko la Himo, polisi kuhamiswa Kasulu. Heko Mdee (janga la mafuriko), Prof Kahigi( pesheni za wastaafu wetu) na mbunge anayeulizia Bima za magari ya serikali.
Ushauri kwa Spika kama Mh. Mbowe hayupo ni lazima yupo anayekaimu nafasi ya Kiongozi wa Upinzani apewe nafasi. Kama tutaendelea na maswali ya namna hii kwa waziri Mkuu posho yenu ipunguze na ipelekwe kwa madiwani, walimu, madaktari au watumishi wengine.
 
Back
Top Bottom