DOKEZO Waziri Mchengerwa huyu mkurugenzi wa Tunduru, Chiza Marando na PS wake Prisca Nyoni wananyanyasa watumishi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

saigilomagema

JF-Expert Member
Jun 5, 2015
4,173
6,156
Waziri wa TAMISEMI huyu mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru akishirikiana na personal secretary(PS) wake wanawanyanyasa sana watumishi hasa walimu.

Huyu PS anaficha barua ya mtumishi hasa inayohusu uhamisho. Kuna mwl alipata uhamisho kutoka TAMISEMI mwaka jana alikaa na barua ya yule mtumishi kuanzia mwezi wa pili mpaka mwezi wa 7. Yule mwl kila akifuatilia anaambiwa nani alikuambia kuna barua yako. Mwishoni alivyoamua kumwona mkurugenzi, mkurugenzi alimfukuza ofisini.

Yule mwl babake alikuwa anaumwa sana na tegemeo pekee ilikuwa yule mwanaye. Yule mzee alikuja kufariki.
Swali ni kwamba ni nini kazi Ya PS? Na kwanini anashirikiana na mkurugenzi kunyanyasa watumishi? Bila shaka ana uhusiano na mkurugenzi asingekuwa na ile jeuri.

Ni wakatili wasio na huruma, mtumishi anaomba uhamisho TAMISEMI kwasababu ana matatizo, TAMISEMI inampatia uhamisho, mkurugenzi kwa kushirikiana na PS wake wanaficha barua wanaficha barua, kwa maslahi gani? Mh. Waziri ingilia kati wasaidie watumishi wako dhidi ya hizi dhulma na unyanyasaji.

Huyo PS ni maarufu pale wilayani, ni jeuri, ni katili, anapata wapi ule ujeuri? Anahusika na mambo ya uhamisho? Alishiriki kumwajiri mtumishi yoyote? Mkurugenzi ana maslahi gani na Prisca Nyoni mpaka washiriki kunyanyasa watanzania?

Rais wetu ndiyo mtumishi namba 1, ndiye mwajiri mkuu ila ni mama mwenye huruma nyingi, ushahidi uko wazi, ndiyo kiongozi mkubwa wa nchi alienda kumwona Tundu Lissu Nairobi. Kwanini mkurugenzi asijaribu kufanana na mwajiri wake? Amekuwa Mungu mtu pale Tunduru.

Mheshimwa waziri walinde watumishi dhidi ya hao miungu watu, huyo mkurugenzi na PS waondoeni hapo ikibidi peleka sehemu nyingine
 
Walogeni tu hamna namna,huyo PS Prisca aanze ku-bleed kuanzia tarehe 1 mpaka 31 non stop,huyo Mkurugenzi mlogeni asimamishe uume kuanzia tarehe 1 mpaka 31 non stop,wataacha ufedhuli wao
 
Hapo mwisho umemaliza vibaya hata kukusaidia ni ngumu, kwa kukusaidia kwa vile ni kilaza, uhamisho wa walimu wote majina na barua nakala zao zinakuwa kwa REO + website ya TAMISEMI sidhani kama PS anaweza kuficha na wakati barua zinakuwa kwenye mfumo.
 
Mambo mengine ni kuendeleza ujinga tu. Yani PS na Mkurugenzi wake ni wakushtaki kwa waziri kweli? Hao unaowaona wewe mwenyewe uso kwa uso na issue inaisha. Wasikutishe kwa chochote.
 
Back
Top Bottom