TLS na ukimya juu ya Leseni ya Wakili Fatuma Karume, kilichofanyika ni haki?

Kb Ulayaulaya

JF-Expert Member
Jan 5, 2023
463
645
Hoja yangu kama inavyojieleza, hivi haya matukio ya Fatuma Karume, na swala la Mwambukusi wajuvi au wasomi wetu wa Sheria imekaaje na ukimya wa TLS?

Je, haki ilitendeka au ndio ile funika kombe mwanaharamu apite?

Kiukwel inanitia shaka juu ya mstakabali wa wasomi wetu wenye uelewa wa kutokuwa na hofu pale kwenye suala linalohitaji roho ngumu.

Au ndio tuseme Katiba ndio inaruhusu haya mambo yakihuni au mimi ndio uelewa wangu ni mdogo kwenye hizo nyanja.

Pale Mahakama inapobariki uzandiki ilihali inajua ukweli au sio Mahakama bali Hakimu au Jaji mwenye kusikiliza kesi mtawaliwa.

Je, Majaji na Mahakimu wao sio wanachama wa TLS?

Naomba kujuzwa jamani ,maana daaaaaah nimechoka mimi.
 
Back
Top Bottom