maishapopote
JF-Expert Member
- May 28, 2009
- 3,277
- 5,514
amevuna alichopanda
Jamani Tido ni kichwa kizuri sana kile kwenye ile fani yake,tunapoteza mtu potential,mi nafikiri kama kuna redio na TV zinazoweza kumlipa hapa bongo achukue kazi au kama vp afungue yake
wako wapi wale waliokua wanailaani TBC nao waseme yakwao?? maana hapa naona zimejaa sifa wakati very short while ago nilizoea kusoma mabaya kuhusu TBC na huyu baba??
Au ndio wale mbayuwayu sisi??
Hivi wananchi hatuna say katika hili? Can someone tell me what lipi tunaweza kufanya kuhakikisha tido stays?
Hivi wananchi hatuna say katika hili? Can someone tell me what lipi tunaweza kufanya kuhakikisha tido stays?
Tido hajaisaidia Chadema kama Tido bali kutokana na kusisitiza impartiality wakati wa uchaguzi mkuu the biggest benefactor ni upinzani na Chadema ndio the lead.<b><i>tido ameisaidia chadema? Alikuwa akitangaza bila upendeleo wakati wa uchaguzi mkuu? Hii mbona siielewi?</i></b>
Afadhali umeliona hilo. Ninashangaa watu humu wapokuwa general kwamba "watu wamegeuka"! Ni lini JF ilitoa msimamo kwamba haimpendi Tido? Ni vyema Acid na wenzako mkajua kwamba hapa kuna watu wengi sana, kwa hiyo kutoa judgement kuwa watu wana msimamo fulani inabidi uwe specific sana. Heri ungesema "Sinkala umegeuka" au "Invisible umegeuka" na ukaweka quotes za misimamo ya zamani. Kuna watu humu hawachangii mara kwa mara, kwa hiyo ukiwaita kuwa wamegeuka wakati hawakuchangia hiyo hoja unayosema wamegeuka, utakuwa haujawatendea haki!Kina Aci mnakosea mnaposema watu wamegeuka, hapa kuna watu wengi sana na maoni yetu pia ni mengi na tofauti sana, pamoja na kuwa yanaweza kugeuka pia. ...!
Solution is to get CCM out not just make Tido stay....that permanent solution!!!Hivi wananchi hatuna say katika hili? Can someone tell me what lipi tunaweza kufanya kuhakikisha tido stays?
Send to a friend Friday, 17 December 2010 06:34 0diggsdigg
Sadick Mtulya, Patricia Kimelemeta
BAADA ya kufanya kazi nzuri ya kuboresha matangazo na uendeshaji wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), serikali imeamua kuachana na mkurugenzi wa chombo hicho, Tido Mhando baada ya mkataba wake kuisha, lakini mtangazaji huyo maarufu ameielezea uamuzi huo kuwa kuwa ni wa utata.
Kuenguliwa kwake kumefanyika takriban miezi miwili baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu ambao TBC iliripoti kwa kina na bila kupendelea chama chochote na hivyo kujivunia sifa kemkem kutoka kwa watazamaji wa TBC1 na wasikilizaji wa redio hiyo ya umma.
Hatua hii imenishtua kidogo na hata hivi ninapoongea na wewe wafanyakazi wengi wamepata mshtuko na wengine wanalia," alisema Tido alipoongea na Mwananchi jana. "Ni juzi (Jumatatu) ndio niliandikiwa barua na serikali ya kutakiwa kuondoka.... ilikuwa kinyume kabisa na uratatibu wa serikali.
Barua ya kutakiwa kuondoka niliipata mara baada ya kukutana na kuzungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Michezo, Utamaduni na Vijana , Seti Kamwanda.
Tido, ambaye kabla ya kujiunga na TBC alikuwa mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Habari la Uingereza (BBC), alisema kwa mujibu wa taratibu mfanyakazi anayemaliza mkataba wake anatakiwa kujulishwa suala hilo miezi sita kabla.
"Kimsingi (barua) hukumbusha kwamba mkataba unamalizika na kama serikali inakusudia kuuendeleza au la. Sasa hilo halikufanyika kwangu," alisema.
Kwa mujibu wa Tido, hatua hiyo inaweza kutafsiriwa tofauti na wananchi hasa ikizingatiwa kwamba imefikiwa miezi miwili tu tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu.
Wafanyakazi walipata taarifa ya kuondolewa kwa Mhando jana baada ya mkurugenzi huyo kubandika tangazo la kuwataarifu kuwa anaondoka na kwamba ametakiwa akabidhi ofisi kwa Joe Rugabaramu.
Nyambala, mikataba yote huongozwa kwa vipengele vya mkataba ambavyo ni points za kisheria, hivyo kisheria, Tido amemaliza rasmi mkataba wake tangu tarehe 15/12/2010.
Lakini licha ya kuwepo kwa mkataba husika, TBC ni shirika la umma, hivyo mikataba yake yote hutekelezwa kwa kufuata kanuni za utumishi wa umma zinazosisitiza six months notice prior to exipire date ya mkataba wake.
Kwa vile Tido was not served with leter of intent toka serikalini, tena siku hiyo ametoka kuonana na Katibu Mkuu wake asimweleze chochote kuhusu barua ya kumtaka kukabidhi ofisi, huu ni uthibitisho wa "malice ".
Sheria zimefuatwa lakini taratibu hazikufuatwa na kanuni zimekiukwa.
Smooth transition ni zile zinazo zingatia sheria, taratibu na kanuni.