Tido Mhando atemwa TBC

this is what I call a tragedy ktk fani na tasnia nzima ya habari. TBC chini ya mhando ili transform completely into a new vibrant and prospectful institute
 
Hivi wananchi hatuna say katika hili? Can someone tell me what lipi tunaweza kufanya kuhakikisha tido stays?

Hakuna kitu kama hicho, Tido aondoke amekuwa akipendelea sana CCM unakumbuka alivyozima Kurusha Hotuba ya Slaa 2009 bungeni? Mnakumbuka alivyokata matangazo pale Jangwani? naomba tusiwe wepesi wa Kusahau. huyu atakuwa appointed Soon na JK kuwa RC.
 
Jina hilo lipo katika makabila mengi tu, kama wazigua, wabondei, wanguu, wakaguru, wavidunda n.k.
 
Nadhani habari za kina na uchambuzi zinatakiwa kumwagwa hapa kabla ya kuanza kukimbilia kuwa kaonewa hasa mleta taarifa unaposema kuwa "BAADA YA MKATABA WAKE (WA KAZI KUISHA)".

Mkataba wa ajira ukiisha kama mlivyokubaliana huwezi kulazimisha kwa ni lazima wewe uendelee (maana haikuwa sehemu ya makubaliano). Kwa maana nyingine ni suala la Mwajiri na wewe (Mwajiriwa) wote kukubali kuwa uendelea na hivyo mkataba mwingine mpya unatengezenwa.
Je kama Tido ndiye angeamua kutokutaka mkataba mpya tungekimbilia kuhitimishaje?

Mwajiri anaweza kuona kuwa kuna wengine wana sifa zaidi kuliko huyu. Halafu tuwe pia na utamaduni wa wakati mwingine kupokea mabadiliko bila kutafuta mchawi.
 
Nini maana ya mkataba?
Nyambala, mikataba yote huongozwa kwa vipengele vya mkataba ambavyo ni points za kisheria, hivyo kisheria, Tido amemaliza rasmi mkataba wake tangu tarehe 15/12/2010.

Lakini licha ya kuwepo kwa mkataba husika, TBC ni shirika la umma, hivyo mikataba yake yote hutekelezwa kwa kufuata kanuni za utumishi wa umma zinazosisitiza six months notice prior to exipire date ya mkataba wake.

Kwa vile Tido was not served with leter of intent toka serikalini, tena siku hiyo ametoka kuonana na Katibu Mkuu wake asimweleze chochote kuhusu barua ya kumtaka kukabidhi ofisi, huu ni uthibitisho wa "malice ".
Sheria zimefuatwa lakini taratibu hazikufuatwa na kanuni zimekiukwa.
Smooth transition ni zile zinazo zingatia sheria, taratibu na kanuni.
 
Mods naomba ile thread ya jana kuhusu kina Mhando kujazana TBC iwekwe hewani.

Nadhani mtoa mada alikuwa anajua masahibu yatakayomkumba Tido.

Mtoa mada lazima atakuwa fisadi tu.

Pole Tido.

Chadema wekeni notebook na kalamu zenu vizuri.
 
Kina Acid mnakosea mnaposema watu wamegeuka, hapa kuna watu wengi sana na maoni yetu pia ni mengi na tofauti sana, pamoja na kuwa yanaweza kugeuka pia. Ila wale wasiomkubali pia wapo, na waliokuwa wanamkubali pia wapo.

Pia kuna kina sie ambao hatuangalii jina, bali vitendo, mie nakubali baadhi ya vitendo vyake na baadhi sikuvikubali, nakubali amefanya kazi kubwa mpaka TBC imekubalika. Huyu ni mwana CCM, na alijitahidi sana kujivua ili aweze kuifanya kazi ya umma, kuna wakati alishindwa. Binafsi nilikuwa napenda vipindi vyao wakati bunge linaendelea, watu tulipata uchambuzi wa wiki nzima bungeni.

Documentaries za kitanzania zimekuja juu ukiacha za STAR tv ambazo kwangu ni za juu zaidi.

Ametupa thamani ya kodi yetu kwa TBC.

Ilinipa hofu wakati walipokuwa wanamtuma Shelembi mitaani huko na mambo ya ajabu ajabu yanafunuliwa na wananchi nilianza kuhisi hiki kitu hakitadumu, na kweli naona ndio basi tena. Ila moto uliouwasha hautazimika. pamoja na mapungufu yako, I hope watu uliowascout hawatatolewa kukufuata!!!!
 
Hivi wananchi hatuna say katika hili? Can someone tell me what lipi tunaweza kufanya kuhakikisha tido stays?

1. Kudai katiba mpya
2. Kudai tume HURU (siyo ya uhuru) ya uchaguzi
3. Kutopigia kura CCM ww na familia/"kabila" lako lote
4. Kulinda kura zenu kama Mwanza na Arusha na Ubungo
5.Chadema na CUF wasirumbane bali waungane
6. Waislamu kwa wakristo washirikiane na wala wasifarakiane
7.........?

Hii ni hatari kubwa inayofanywa na CCM, baada ya muda mfupi sidhani kama tutaiona TBC nje ya Nchi, bcz we expect Makamba to dominate the transmision system.
 
Ili mashirika ya Umma yanayomilikiwa nchini Tanzania yaweze kupata na kuhifadhi wanataaluma wanaofanya kazi zao ndani ya mipaka ya taaluma zao bila upendeleo kwa wateja wake wala kuhofia HASIRA, HILA, CHUKI BINAFSI AU KULIPA KISASASI ZA MTU BINAFSI KWA JINA TU LA KUWA KIONGOZI wa nchi, ni vema wakuu wote wa mashirika yetu nafasi hizo zitangazwe na mashirika ya ajira kuwafanyia usaili kiushindani haswa kama kule TFF (wakapeleke majina yaliokwishachujwa tuseme kama watu 4 bora hivi kwa nafasi moja) na hatimaye yule mtu gani wa kuchukua nafasi husika ni lazima apatikane kuthibitishwa na bunge letu tukufu kwa kufuata vigezo bayana.

Moderator, hili nalo liingize kwenye orodha ya mapendekezo ambayo sisi wana-JF nasi tutazifikisha kwenye mkutano mkuu wa kitaifa wa KUANDIKA UPYA KATIBA. Hili la Todo Mhando ni kielelezo tosha KWA NINI TANZANIA MIAKA YOTE TUKO NYUMA KIMAENDELEO.
Utendaji wako kazi haujalishi bali ni kiwango chako cha KUJIBARAGUJA kwa viongozi.

Kama KATIBA MPYA haiotofanyia kazi mambo kama haya na kuthibiti mamlaka ya raisi kwa njia ya bunge basi bado tuna safari ndefu sana katika kumudu ushindani ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
 
Tido nenda Tido, huna haja ya kutafakari what next kwani umeacha legacy itakayokujemgea heshima.
Big up Tido.

Legacy ipi?? mjinga kabisa huyu alikuwa kibaraka wa ccm na aende zake akalime shamba lake la viazi
 
Binafsi kutoka a guy from his calibre..... I expected more from TBC..... Ujuzi wake na experience TBC ingeweza kuwa better.... apart from uchaguzi TBC ililack creativity.... TV ya Taifa imejaa matangazo vipindi kama cherekocheroko.... na a lot of gambling......

He Could have done better....... Na ningependa ajaye afanye kweli hii iwe TV ya Taifa..... TV ya taifa inabidi iwe na vipindi vyenye tija kwa Taifa sio iendeshwe kwa minajili ya kupata profit (profit oriented)........ PUNGUZA commercials..... Bring informative and educative products.... Commercials na mambo ya biashara waachie the likes of ITV and other private TVS narudia..... I EXPECTED MORE FROM HIM
 
Hukujua unaocheza nao? Sasa yakowapi kuwabana wapinzani na taarifa zako za upendeleo mtupu!!!! ukaozee mbali kabisa
 
Hakuna kitu kama hicho, Tido aondoke amekuwa akipendelea sana CCM unakumbuka alivyozima Kurusha Hotuba ya Slaa 2009 bungeni? Mnakumbuka alivyokata matangazo pale Jangwani? naomba tusiwe wepesi wa Kusahau. huyu atakuwa appointed Soon na JK kuwa RC.

Inawezekana Tido ali pewa amri azime kurushwa live ,kama vile kile kipindi cha FNL cha cahhnel 5 ambapo Sugu alitakiwa kuwepo alipigwa stop.

Kigogo gani ambaye alimleta TIDo, ni Lowassa nini? maana tunajua Suzan alikuja kwa mgongo wa Lowassa , je kibarua chake naye kikoje?
 
Ndiyo maana wengi wetu tunalilia katiba mpya ili kuondoa upuuzi wa aina hii. TBC ni shirika la umma. Ajira ya mtumishi wake mkuu lazima itolewe kwa kufuata mchakato wa wazi. Na kwa kuzingatia unyeti wa nafasi hiyo kuna umuhimu pia wa kuhusisha bunge.

Pole mzee Tiddo. Hiyo ndiyo 'sisi ni m'.
 
Hakuna kitu kama hicho, Tido aondoke amekuwa akipendelea sana CCM unakumbuka alivyozima Kurusha Hotuba ya Slaa 2009 bungeni? Mnakumbuka alivyokata matangazo pale Jangwani? naomba tusiwe wepesi wa Kusahau. huyu atakuwa appointed Soon na JK kuwa RC.

hahaa unakumbuka sana vitu mkuu..mi nikisikia jina lake nataka kutapika hata uji wangu wa ulezi niliokunywa this morning
 
Kina Aci mnakosea mnaposema watu wamegeuka, hapa kuna watu wengi sana na maoni yetu pia ni mengi na tofauti sana, pamoja na kuwa yanaweza kugeuka pia. Ila wale wasiomkubali pia wapo, na waliokuwa wanamkubali pia wapo.
Pia kuna kina sie ambao hatuangalii jina, bali vitendo, mie nakubali baadhi ya vitendo vyake na baadhi sikuvikubali, nakubali amefanya kazi kubwa mpaka TBC imekubalika. Huyu ni mwana CCM, na alijitahidi sana kujivua ili aweze kuifanya kazi ya umma, kuna wakati alishindwa. Binafsi nilikuwa napenda vipindi vyao wakati bunge linaendelea, watu tulipata uchambuzi wa wiki nzima bungeni.
Documentaries za kitanzania zimekuja juu ukiacha za STAR tv ambazo kwangu ni za juu zaidi.
Ametupa thamani ya kodi yetu kwa TBC.
Ilinipa hofu wakati walipokuwa wanamtuma Shelembi mitaani huko na mambo ya ajabu ajabu yanafunuliwa na wananchi nilianza kuhisi hiki kitu hakitadumu, na kweli naona ndio basi tena. Ila moto uliouwasha hautazimika. pamoja na mapungufu yako, I hope watu uliowascout hawatatolewa kukufuata!!!!

Acid & Co. ni wajuaji wa kila kitu.

Wanadhani wapo hapa kufikiria kwa niaba ya sisi wengine.

Hasira za Zito Kabwe.
 
Back
Top Bottom