THT vs BSS

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,883
2,763
Waswahili wanasema kuwa ngooma ikivuma sana hupasuka. Mashindano ya Bss japo yapo kitambo sasa yameonekana hayana tija kwa upande wa washiriki ila ni mtaji kwa waandaaji. Nasema hivi kutokana na ukweli kuwa tangu haya mashindano yaanze miaka takriban 5 iliyopita hakuna bidhaa (msanii) ya kweli ambayo imeweza kuingia sokoni na kudumu japo miezi 6! Wengi huishia pale hela zao walizopewa zinapoisha.

Wapi Jumanne Iddi, wapi Misoji, wapi Leah Moudy, wapi Kassim, wapi Iddi Ramadhani. Hao nazungumzia wale washindi wa kwanza. Top ten nzima hakuna ambaye ameweza kuchomoza tangu mashindano kuanza. Kizuri zaidi ni kuwa hata Benchmark wanakiri hilo.

Matokeo yake tunashuhudia walioshindwa Bss wakikimbilia Tusker Project Fame. Hao ni pamoja na Peter Msechu, pamoja na wengine wanaoshiriki mwaka huu. Historia inaonyesha kuwa hata Project Fame nayo haina tija kwani tangu kipindi kile inafanyika South Africa, Lindiwe (mwanadada mwenye sauti kumshinda Whitney) wa Zambia aliibuka mshindi. Yuko wapi? Kulikuwa na Dare wa Nigeria mwenye sauti kama Luther Vandross. Yuko wapi?

Tusker project fame imehamia Kenya lakini nayo imeshindwa kutoa wasanii waliotegemewa kufanya vyema zaidi ya kutengeneza majina kwa usiku mmoja. Bss imeshindwa kutimiza lengo ikaamua kubadili malengo ya mashindano kwa kusema kuwa wanawawezesha vijana kujitegemea kimaisha hata kama si kupitia muziki. Ingekuwa hivyo basi ungebuniwa mradi mwingine kama ilivyo kwa Big Brother au iliyokuwa yetu ya Maisha Plus.

Kwa kiasi kikubwa hili la kujenga wasanii limeweza kutekelezwa na Tanzania House of Talents (THT). Hawavumi ila wapo sana. THT inatoa wasanii wengi wa aina tofauti lakini wa muziki ndio zaidi, na kizuri zaidi wameweza kuwepo kwenye tasnia kwa kitambo huku wakiendelea kuimarika.

Msanii kama Amini, Barnaba na Mataruma kipindi hicho nawaona kwenye Jenerali on Monday sikujua kama ndio hawa wa sasa japo walikuwa na dalili za wazi za kuonyesha kuchomoza.

Kilichonifanya kuandika haya yote ni baada ya kuona mahojiano ya msanii Rachel (aka Ray c), pamoja na kuona wimbo wake mpya videoni. Ishu si video bali mpangilio wa sauti na ubora wa sauti yake. Nikasema ninawiwa kusema chochote juu ya THT.

THT imeweza Kutoa wasanii wengi na wazuri na wanaoonekana kudumu kwenye tasnia kwa muda mrefu, tangu kina Mwasiti, Barnaba, amini, Linah, Rachel na wengine wengi. Nina hakika hawa wangepitia BSS leo hii tusingewasikia katika ramani ya muziki wetu.

Kilicchobaki ni kuanza kutafuta ni nini hasa kinachofanya hawa wanaopitia BSS washindwe kabisa kufanya vyema kwani tangu kuingia kambini hadi siku ya fainali, ni kwamba wamepikwa hadi wakapikika. Wana walimu wazuri, vifaa, wanakula vizuri, wanalala pazuri... Kwa nini washindwe kutokelezea?
Sababu ni deni walilo nalo kwa watanzania au hofu ni ile publicity wanayopata? Au sababu ni media kuwabania? BSS nao wangekuwa na radio na tv yao inawezekana wasanii wanaotokana na Bss wangepata air time ya kutosha na kuwafanya kuwika? Haya ni mambo ya kuhoji.
 
Kuna kitu Gospel Star Search kimeibuka, na soon tutasikia mashindano mengine yakiibuka, je mashindano haya yana manufaa gani kwa wasanii na jamii yetu kwa ujumla?
 
Tatizo hawa waandaji ya bss na tusker project fame hata american idol wanachofanya wanatengeneza bubble gum musician...we huwezi mchukua mtu kisa anajua kuimba akiwa bafuni ukampa mazoezi ya wiki 2 hadi miezi 4 ukategemea atakuja kuwa mwanamziki mkubwa...sidhan ka elimu ingekuwa inatolewa hivyo tungekuwa na madokta na maprofesa....historia inajionyesha wasanii walioweza kuhimili mikikimikiki ya mziki wamekuwa kwe tasnia mda mrefu kabla hata hawajajulikana na nadhan ndo kitu kinachofanya Tht waweze toa wasanii wazuri kwani hadi wagraduate pale kuna madogo waliojifunza mziki hadi miaka mitatu mle ndani...maoni yangu
 
mkuu ni kweli unachosema. Chukulia mtu kama Peter Msechu, huyu jamaa ana kipaji cha ukweli. Pia ninavyoamini ni kuwa sauti ndio humfanya mtu awe mwanamuziki ama la. Sasa pamoja na kuwa big g, huoni kuwa kuna kitu kingine kinakosekana hapo-management ya msanii baada ya BSS? Tatizo kubwa ninaloona ni kuwa haya mashindano si endelevu, kwa maana kuwa ilibidi pawe na project nyingine pale Bss inapoishia. Kwa kuwa hawa jamaa ni bubble gum, wanashindwa kuhimili vishindo pale Bss inapowaachia.
 
Pamoja na kuwa ni miradi yao, wangeiganya endelevu maana mwisho wa siku watachokwa. BSS iliyopita ni tofauti kabisa na zilizotangilia kwa mvuto.
 
1.BSS:Tatizo haya mashindano wanaangalia mtu anayeimba vizuri kwa kucopy nyimbo za wasanii wengine(wana-Timbulolize) kitu ambacho si sahihi,ilitakiwa tuone uwezo wao kwa kuimba tungo zao wenyewe.kucopy na kuedit ni kitu rahis sana.

2.Media Suport kwa THT: uwepo wa Clouds Fm ambayo inasadikika ni powerful radio in tz kwenye ishu za burudan unawaboost sana ukizingatia ndo wamilik wa tht.BSS,mtu kama Kala Jeremiah ni product pekee niliyokuwa naikubali na jamaa yuko vzuri kiukwel lakin media zinambania sana.

ADDITION: Mwanzon nilikuwa siwakubali kabisa THT,nilihisi hawana kitu zaid ya kubebwa.fact: wanabebwa ndio kwa promo ya kutosha ila mtu kama BARNABA anadeserve such promo jamaa amekamilika,wengine kama AMIN,LINA,MWASITI,DITO,RECHO ni wasanii wazuri pia.
 
Katika hili ndio nikasema kama nao BSS wangekuwa na media za kuwaendeleza hawa washindi na kuwapa airtime ya kutosha wasingekuwa wanaishia njiani. Benchmark wana huu uwezo ila tatizo lao ni malengo yao ya muda mfupi na kupata hela za wadhamini tu. Wafanye outsourcing ya kitengo cha media baada ya BSS-yaani life after BSS. Kwa njia hii wanaweza kuwabakisha wasanii kwenye chati.
 
wangekuwa wanania nzuri nao kweli mi nazan media isingekuwa tabu coz bibie Rita nasikia yupo Close sana na mengi,so ilikuwa ni swala la kumuomba tu muheshimiwa awaambie watangazaj wake kutoa sapot ya kutosha kwa hizo product kama wafanyavyo cloudz kwa tht Raia Fulani
 
Last edited by a moderator:

jaquline Ntuyabaliwe(kama sijakosea) akikataa je?????
 
Last edited by a moderator:
Mjini Mipango wadau....hata hao vijana wa tht tunaowaona nang'aa ukiwafatilia unaweza kusikia hawanufaik na chochote kwenye kaz zao zaid ya kuvaa na kujulikana.....unadhan rughe atawapa promo kijingajinga???ameshawatumia wasanii wangapi???
 
wangekuwa wanania nzuri nao kweli mi nazan media isingekuwa tabu coz bibie Rita nasikia yupo Close sana na mengi,so ilikuwa ni swala la kumuomba tu muheshimiwa awaambie watangazaj wake kutoa sapot ya kutosha kwa hizo product kama wafanyavyo cloudz kwa tht Raia Fulani

Tatizo radio one na itv zimekaa kitaifa sana. Capital fm haivumi. Labda eatv. Clouds they mean business
 
Last edited by a moderator:
Mjini Mipango wadau....hata hao vijana wa tht tunaowaona nang'aa ukiwafatilia unaweza kusikia hawanufaik na chochote kwenye kaz zao zaid ya kuvaa na kujulikana.....unadhan rughe atawapa promo kijingajinga???ameshawatumia wasanii wangapi???

kutumiwa hilo ni suala lingine, lakini cha msingi wanasikika vya kutosha. Hapo sasa ni akili vichwani mwao, maadam wana majina
 
1.BSS:Tatizo haya mashindano wanaangalia mtu anayeimba vizuri kwa kucopy nyimbo za wasanii wengine(wana-Timbulolize) kitu ambacho si sahihi,ilitakiwa tuone uwezo wao kwa kuimba tungo zao wenyewe.kucopy na kuedit ni kitu rahis sana.

2.Media Suport kwa THT: uwepo wa Clouds Fm ambayo inasadikika ni powerful radio in tz kwenye ishu za burudan unawaboost sana ukizingatia ndo wamilik wa tht.BSS,mtu kama Kala Jeremiah ni product pekee niliyokuwa naikubali na jamaa yuko vzuri kiukwel lakin media zinambania sana.

ADDITION: Mwanzon nilikuwa siwakubali kabisa THT,nilihisi hawana kitu zaid ya kubebwa.fact: wanabebwa ndio kwa promo ya kutosha ila mtu kama BARNABA anadeserve such promo jamaa amekamilika,wengine kama AMIN,LINA,MWASITI,DITO,RECHO ni wasanii wazuri pia.

We kweli ni Mkare wetu!
Mkuu Mkare_wenu nimekubali sana comment yako...

Kwanza kabla ya kuchangia naomba nitangaze conflict...... Siwakubali kabisa clouds na miradi yao yote sababu nawaelewa vizuri sana hawa jamaa toka mwanzo!

Mkuu Raia Fulani katika kusawazisha mjadala inaweza isiwe sahihi sana kulinganisha kati ya hizi star/model search na "talent center"...
Hasa talent center yenyewe inapo milikiwa na chombo cha propaganda na fitna huku kikipumbaza watu kuwa eti yenyewe ndio redio namba moja.
Katika mfumo wetu dhaifu wa media inalazimu hawa jamaa kuonekana "namba wani" kweli sababu ni wajanja hasa...

Hao wasanii "wakali" wameenda wapi hasa nao? Zaidi ya nyimbo zao kupigwa sana kwenye redio tu na kupewa show za laki laki??
Mafanikio ya wasanii wa THT ni ya muda mfupi sana....
Clouds uwezo wao utashia kwenye miradi ya matamasha mepesi tu ya humuhumu ila hii miradi music haitakuja kuweza hata siku moja kama ilivyokufa mradi wa "Smooth Vibes Project"...

Na hao wasanii wa kwenye star search makini (toa bss) bado wana nafasi kubwa sana ya kufika mbali sana.

BSS yetu ilipoteza umakini baada ya ile ya kwanza tu iliyowatoa wakina Leah Moudy, ila kushindwa kwa bss pia ni ukweli kuwa bongo uimbaji ni tatizo kidogo pia rejea Cocacola Popstar (ilibidi wachukue watu wa rap Langa na Witty tu na Sarah Kaisy au ile pop Idol amabpo ilibidi wawachukue wakina Banana)

Hizi star search zinakuwa na lengo maalum na baada ya mshindi kupatikana anatumikia mkataba wake baada ya hapo anamwagika kwenye soko na kuanza kupambana kama wengine na kukabiliana na changamoto za soko husika...

Rwanda bado wanajenga soko lao la music likikaa sawa wakina Alfa watakuwa mbali sana hata hivyo kwa uwezo huwezi kumlinganisha Alfa na Barnabaz wa THT haijalishi kiasi gani mtu anapewa promo za kijinga,
Kenya marketi ya music ni ngumu sana, pale watu wanapenda na kuujua mziki hivyo kuna wakali wengi tu wana heshima zao na wanafanya music kwenye level yao na wana watu wao mfano watu kama Harry Kimani na Didge...
Ndugu yangu kuhusu USA acha kabisa, sababu wasanii wengi wakali wanatoka kwenye hizo search kwa kukumbusha wachache wakina Ruben Stadard, Carry Clarkson, Destiny's child (Beyonce), Fantasia, Leona Lewis (UK) etc etc

Hivyo suala la mtu anafanya vipi baada ya makataba wake wa kwanza na kampuni ile iliyomtafuta inategemea sana na hali ya soko la Music la nchi husika.

Soko letu la music linaugua fitna na ghiriba za hichi kiredio kinachojifanya kina hatimiliki ya wasanii matokeo yake wamevuruga kila kitu kwenye music ya bongo na saiv wanaelekea kwenye gospel.....

Last edited by a moderator:
kutumiwa hilo ni suala lingine, lakini cha msingi wanasikika vya kutosha. Hapo sasa ni akili vichwani mwao, maadam wana majina

Akili vichwani mwao kivipi tena wakati kuna mtu anawatumia??

Mkuu music ni business ambapo party zote lazima zinufaike kwa uwiano unaoendana!

Hamna mwanamziki asiyetumika hapa duniani, ila huyo anayemtumia ni lazima awe anaratibiwa na taratibu za soko ambazo ni lazima zilazimishe maslahi kwa msanii husika...

Kama zilivyo biashara zingine, music inataka kuendeshwa na watu wanaoijua, hivyo hata kama wewe una hele zako sawa unaweza kuwekeza kwa kutumia wajuaji wa music...

Mfano kama wewe sio mhandisi na unataka kuingia kwenye biashara ya uandisi itakulazimu uwatumie wahandisi....
Kwa bahati mbaya sana wafanya biashara wa hapa kwetu hawajui music na wanatumia matapeli wasiojua kitu kuhusu music!

Katika mazingira hayo huyo mwanamziki unayemwambia "akili vichwani" ni kumtelekeza tu na ndio kinachotokea kwenye vipaji vingi vya nchi hii.
 
Tatizo radio one na itv zimekaa kitaifa sana. Capital fm haivumi. Labda eatv. Clouds they mean business

Mkuu Raia Fulani

Hao jamaa wanatumia vizuri mianya ya mapungufu yetu ya mfumo wa sanaa..

Kweli ni wajasiriamali wazuri sana, na kweli wanaijua biashara!

Kwa bahati mbaya sana Music haiendeshwi na wafanyabiashara pekee kama haop jamaa zako wanavyofanya....

Hii bongofleva yao imekosa tija kwenye sura za kimataifa hata kitaifa ndio maana wasanii wake bado ni masikini sana...

Pia mbaya sana wabongo wengi tunapenda kufungwa na kitu kimoja tu...
Tungefungua macho tungejua kuwa Music yetu (sio Bongofleva) ilikuwa mbali sana kabla ya ujio wa hii redio ya kichiriku..

Wamevuka mipaka ya utendaji wa redio za kawaida na wameingia kwenye shughuri wasioiweza wala kuijua...

Wataendelea kuvuruga tu!

Niliwahi kujadili kidogo kuhusu
"HIKI KITU BONGOFLEVA NA UTATA WAKE NA UDAU FEKI WA WADAU"
 
Last edited by a moderator:
mkuu JG salute! Bila shaka wewe ni mdau mzuri sana kwenye tasnia ya muziki hapa ndani na nje. Kwanza naomba nikutoe shaka kuwa mi si mdau wa clouds media ila ninasema kutoknana na mazingira yaliyopo. Undani wa mazingira yenyewe ni ishu nyingine. Nikiri kuwa sijaingia deep kabisa kujua operations za ndani za hawa jamaa tunaowazungumzia. Naandika kutokana na kile kinachoonekana machoni.

Ukweli ni kuwa mfumo wa soko la muziki wetu licha ya kutokuwa na faida kwa msanii, bado hauko rasmi kiasi cha kuaminiwa kumlinda mwanamuziki na mlaji.

Najua pia kuwa tht kupitia clouds media wamehodhi mambo mengi, kuanzia wasanii hadi miundombinu ya kimuziki. Ilikuwaje wakafika hapo? Hivi kuna watu walionyimwa kujipanga kama clouds media? Hawa jamaa wananyanyasa kwa kuwa ni kama wamehodhi soko la burudani hapa nchini na ndio maana inaonekana kama wanafanya wanachotaka.

Chema siku zote hujiuza wandugu no matter what! Hizi nyimbo za wasanii toka tht ni nzuri na zimeimbwa na wanamuziki waliopikwa na ndio maana hazipigwi clouds fm pekee. Ukija top ten radio one zipo, ukienda majic fm zinapigwa sana! Ukirudi eatv zinachezwa na kuombwa mbaya.

Management nalo ni suala jingine. Pamoja na exposure waliyopata wasanii wa bss. Pamoja na kuwa na sauti nzuri za kuimba kama Msechu, Leah, Misoji, Kassim... Kwa nini walishindwa kupenya kwenye soko kama tunajua kuwa chema chajiuza? Juzi nimemwona Leah Moudy kupitia star tv wakiwa kwenye mazoezi ya bendi yao inaitwa Q. Hakuna wanachoimba! Na nilikuwa namtazama Leah usoni wakati anaimba nikaona wala hata hayuko pale, wala mood hana. Lakini mwisho waliimba wimbo wa shakira-this time for Africa, aliimba vizuri sana na kwa uchangamfu. Hii inanipa picha kuwa hakuna ubunifu.

Katika mazingira kama haya wasanii watabaki kupiga kazi za wasanii maarufu wa nje. Hili kundi ni la kina kitime, kinasha, mzee Zoro, then vijana wenzetu ambao wameamua kuingia nao kwenye mkumbo wa bendi kwa kisingizio cd haziuzi na hawapati air time ya kutosha. TID ni mfano mzuri. Aliiba wimbo wa nje akaupa jina la 'nyota yako.' alivuma nao sana kumbe kaiba nje. Sasa wimbo ungekuwa wake si angekuwa na heshima sana?

Ninachoona hapa ni kuwa kuna watu wamewekeza katika muziki, na katika muziki huo wanapata faida, ila cha kuangalia ni vipi na hao wanamuziki wanafaidika. Hawa ni pamoja na clouds media. Kuna wengine wamewekeza katika hela za wadhamini. Wanapata watakacho kisha wanamuweka msanii pembeni. Hawa ni pamoja na kina Benchmark.

Kinazchotakiwa hapa na watanzania kuacha kulalamikia clouds media. Wamekatazwa kufannya kama wao? Sikubaliani na unyonyaji, ila, kama msanii anaona ananyonywa, kwa nini ang'ang'anie kuendelea kunyonywa?
 
Back
Top Bottom