The Zitto saga: Vyombo vya habari vinaiua CHADEMA?

Status
Not open for further replies.
Mwaka jana December, Mwanahalisi (Kubenea) waliandika hii habari na leo hii tunaweza pia kuijadili kuangalia utafiti wa Mwanahalisi. Hili gazeti nimekuwa nalisoma na kuwaamini nusunusu maana wanachoandika huwa ni kweli ila lazima WAONGEZE CHUMVI . Tatizo ni kujua hii chumvi iko wapi. Tujikumbushe:

Kibaya zaidi ni kuwa, Kubenea ambaye ni member wa JF, na Mwakalinga akiwa member wa JF, alishindwa hata kumuandikia EMAIL kumuuliza kipi ni kweli katika haya. Walau kuna mengine yangelirekebishwa na kuacha makosa ya waziwazi kama ya NI MWANAFUNZI wakati ukweli jamaa alishamaliza siku nyingi sana.
From: Ubunge wa Mwakyembe shakani | Gazeti la MwanaHalisi

naona umejaza si kweli kibao,kwamba hamna la kweli hata moja wanaandika hawa watu au?
 
Assuming alichoandika mwanahalisi ni kweli.

CDM, kupitia Dr Slaa, wanaituhumu TISS wa kusaidia kuvuruga uchaguzi mkuu, uchaguzi ambao CDM kinaamini mgombea wake wa urais alishinda [Kwa kitendo hiki ni wazi CDM inaona TISS kama maadui. Zitto anaionaje TISS/Zoka? Hivi inawezekana Zoka hakuhusika katika huo mchakato?]

Mwanahalisi limegundua kuwa 'vigogo kadhaa wa TISS wanaingilia CDM'
[Kumbe ni kuna zaidi ya Zoka? Wanaingilia kupitia kwa Zitto tu au kuna milango mingine?]

Vigogo hao, hususani Zoka, wanamahusiano ya karibu na Mh Zitto
[kwa mawasiliano ya zaidi ya mara tatu kwa siku kudhani watu hao wana uhusiano wa karibu si vibaya, inawezekana ni marafiki! Lakini marafiki mara nyingi wanakuwa na interest moja au zaidi zinazofanana. I hope hiyo inerest sio ya kuipokonya ushindi CDM wala ya kuivuruga! Au pengine ni 'mtu na bosi' wake...alikuwa anapewa maelekezo ya kazi na kutoa feedback?]

Kuna ushahidi kuwa Zitto na Zoka wamekuwa wakiwasiliana kwa simu (SMS na Voice calls) zaidi ya mara tatu kwa siku
[WikiLeaks! uzuri na ubaya wa simu.....labda wiki ijayo baada ya Zoka na Zitto kukanusha tuhuma hizi Mwanahalisi linaweza kurelease 'cables' ili tuone hizo sms zinazoleta mashaka]

Mwanahalisi halikuweza kugundua mara moja undani wa mawasiliano ya Mh Zitto na Zoka
[Ni mtego huu. Pengine hapa ndipo Mh Zitto na Zoka ndipo waanatakiwa watuweke sawa na kwa umakini mkubwa maana bila shaka hawaju extent ya details ambazo Mwanahalisi inazo]

Shaka ya baadhi ya wachunguzi wa mambo inatokana na ukweli kuwa Zoka ni mmojawapo ya vongozi wa TISS (kigogo) na Mh Zitto ni mwanasiasa kutoka chama ambacho kinaituhumu TISS kusaidia kuvuruga uchaguzi mkuu
[ I believe any skeptical mind would think the same!]
 
kamakuna ukweri anatumiwa watakapomtumia atatupwa nahapondomwishowake kisiasa mf ukinunuwa soda yakopo ukimarizasoda kopo hutupwa nahauwezilikumbukatena namukumbu zito asijeakawa kopo wakimutumia atatupwa jararani muogopemungu kumbukaariye msaliti yesu aliishiya wapi?
 
When are we (GREAT THINKERS) going to discuss serious issues instead of discussing about people?. My suggestion is that if we real think about bringing change to our country, let us make this platform a true reflection of GREAT thinkers. Sehemu kubwa ya posting ni malalamiko, shutuma na kukashfianan my friends this is a true character of IRRESPONSIBLE people and I think most of JF aren't those kind of people. Let us create a platform ambayo hata watawala wakiwa na challenge they can seek constructive opinion. Right now anyone raising a different view of specific issue is labeled ametumwa na mafisadi!!.Let us just review a simple issue. Angalia kama kuna topic yoyote ambayo imekuwa na michango minyofu, whether for or against kwa utaratibu unaomfanya bystander aweze hata kutengeneza documentary ya kuisaidia jamii yetu.
Let us wake up great thinkers, let us not allow our minds to be poisoned by political landscape to the extent of seing every issue as politics.
 
Wewe kubenea hebu tuwekee contnt ya hizo sms kama ambavyo ulikwisha wahi kufanya nyuma ili tukuamini, inawezekana na wewe ni katika wale wanaomchukia zitto kwa imani ya dini yake kama anavyosema mwenyewe
Poor guy, Mbona Kubenea nae ni Muislam atamchukiaje Muislam mwenzake ? Zito ni Spies au nikupe cheki namba yake ya salary toka TISS.
 
Usalama wa Taifa wavamia Chadema

Vigogo kadhaa wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) wametajwa “Kuingilia” Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mwanahalisi limegundua.

Taarifa zilizopatikana kutoka ndani ya idara hiyo zinaeleza kuwa vigogo hao wana mahusiano ya karibu na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe.

Anayetajwa rasmi kuwa na mahusiano na Zitto ni Naibu Mkurugenzi wa TISS, Jack Zoka.

Kufichuka kwa taarifa za kuwapo “uswahiba” kati ya Zoka na Zitto kumekuja katika kipindi ambacho Chadema kimekuwa kikituhumu maofisa wa juu wa TISS kuvuruga uchaguzi mkuu uliopita.

Aidha, kuibuka kwa tuhuma hizi kumekuja wiki moja baada ya gazeti hili kuchapisha taarifa mbalimbami za mawasiliano kati ya Zitto na Rais jakaya Kikwete.

Baadhi ya mawasiliano hayo ambayo Zitto ameyapeleka kwa rais aliyapeleka pia kea baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi nchini.

Kwa mujibu wa mgombea urais wa Chadema, Dr Wilbrod Slaa ambaye alitangazwa kushika nafasi ya pili nyuma ya Rais Kikwete, viongozi wa TISS walihusika, kwa kiasi kikubwa, katika kile alichoita “Kuchakachua matokeo ya uchaguzi.”

MwamnaHALISI limefanikiwa kupata rekodi ya mshororo wa mawasiliano kati ya Zitto na Zoka.

Kuna mwingiliano wa simu za mdomo na maandishi (sms) kutoka kwa Zitto kwenda kwa baadhi ya vigogo wa ngazi za juu serikalini na TISS, hasa Zoka.

Nyaraka za mawasiliano zinaonyesha kuwa Zitto amekuwa akiwasiliana na naibu mtendaji mkuu wa TISS huyo zaidi ya mara tatu kwa siku.

Kwa mfano, Zitto na Zoka walifanya mawasiliano ya simu mara tisa hapo tarehe 8 Agosti. Simu iliyotumiwa katika mawasiliano hayo ni Na. +255756809535 ambayo hutumiwa na Zitto na +255754787550 ambayo hutumiwa na Zoka.

Wakati mawasiliano hayo yanafanyika, Zitto alikuwa katika maeneo tofauti.

Mawasiliano ya kwanza kati ya Zitto na Zoka yalipokuwa yanafanyika, simu ya Zitto ilisomeka kuwa alikuwa katika maeneo mbalimbali.

Mathalani, wakati mwingine simu ilikuwa ikisomeka kuwa yuko Mtambani, Kinondoni, dare s Salaam, Kigoma Urban (Mjini), Kigoma Rural (Vijijini), Mtwara, Uwanja wa ndege, Ilala, Oyster Bay, Ukonga, Upanga na pia katikati ya mji.

Gazeti hili halikuweza kugundua mara moja undani wa mawasiliano ya Zitto na Zoka.

Kinachofanya baadhi ya wachunguzi wa mambo kujenga shaka ni kwamba mmoja ni mwanasiasa, tena kutoka chama kilichopo nje ya utawala, na mwingine ni mtumishi wa idara ya usal;ama inayolalamikiwa kukandamiza upinzani nchini………………

………Habari zaidi katika MwanaHALISI ya leo.

My take: Haya mambo ya Mbunge huyu sasa yanaanza kuzidi kumtikisa yeye mwenyewe kuliko chama chake.

Mimi nauliza swali hili:

Kwa kuwa tumehakikishwa kwamba mawasiliano katika mitandao ya simu za mikononi (sauti na ujumbe mfupi) ni ya siri na salama, je, chanzo cha habari cha gazeti la MwanaHalisi kimetumia teknolojia ya aina gani kuweza "kuingilia" mawasiliano kati ya Zitto na Zoka, na kuweza kubaini kilichozungumzwa kwenye mawasiliano ya ujumbe mfupi, sembuse kutambua ni mara ngapi waliwasiliana?

Je, ina maana, teknolojia hii SI SALAMA na SIRI kama tunavyoelezwa?
 
Je, ina maana, teknolojia hii SI SALAMA na SIRI kama tunavyoelezwa?
Hizi teknologia haziwezi kamwe kuwa na siri mpaka labda pale mwingiliano wa binaadamu utakapoondoka kabisa. Si umeyaona ya WikiLeaks? USA...of all the nations?
 
Sasa hivi tutaanza kuona post zake chini ya aliases mbali mbali za kutetea, kuliponda gazeti etc bila hata ya kuwa na hoja! nadhani watu wa TISS na wawakilishi wa mafisadi nao wana ID kibao humu ndani ya JF wataanza kazi yao! Ngoja tu!
hIVI UNAWEZA KUJITETEA KWA MAMBO YALIYOTUNGWA NA WENYE NJAA? HEBU MUULIZENI HUYO KUBENEA AKIWAONA USALAMA WA TAIFA ANAWEZA KUWAJUA???
 
hIVI UNAWEZA KUJITETEA KWA MAMBO YALIYOTUNGWA NA WENYE NJAA? HEBU MUULIZENI HUYO KUBENEA AKIWAONA USALAMA WA TAIFA ANAWEZA KUWAJUA???

Lakini Kafiribangi hajakosea sana. Wachangiaji wengi 'wanaomuunga' mkono Zitto wamejiunga JF ktk mwezi mmoja hivi uliyopita. Nina hakika wengi wa hawa ni either Zitto mwenyewe, watu wa TISS, au mawakala wa mafisadi! Zitto ni kwishney, kajivua nguo kabisa -- na sasa anakimbilia udini anaona ndiyo utamuokoa!
 
Assuming alichoandika mwanahalisi ni kweli.

CDM, kupitia Dr Slaa, wanaituhumu TISS wa kusaidia kuvuruga uchaguzi mkuu, uchaguzi ambao CDM kinaamini mgombea wake wa urais alishinda [Kwa kitendo hiki ni wazi CDM inaona TISS kama maadui. Zitto anaionaje TISS/Zoka? Hivi inawezekana Zoka hakuhusika katika huo mchakato?]

Mwanahalisi limegundua kuwa 'vigogo kadhaa wa TISS wanaingilia CDM'
[Kumbe ni kuna zaidi ya Zoka? Wanaingilia kupitia kwa Zitto tu au kuna milango mingine?]

Vigogo hao, hususani Zoka, wanamahusiano ya karibu na Mh Zitto
[kwa mawasiliano ya zaidi ya mara tatu kwa siku kudhani watu hao wana uhusiano wa karibu si vibaya, inawezekana ni marafiki! Lakini marafiki mara nyingi wanakuwa na interest moja au zaidi zinazofanana. I hope hiyo inerest sio ya kuipokonya ushindi CDM wala ya kuivuruga! Au pengine ni 'mtu na bosi' wake...alikuwa anapewa maelekezo ya kazi na kutoa feedback?]

Kuna ushahidi kuwa Zitto na Zoka wamekuwa wakiwasiliana kwa simu (SMS na Voice calls) zaidi ya mara tatu kwa siku
[WikiLeaks! uzuri na ubaya wa simu.....labda wiki ijayo baada ya Zoka na Zitto kukanusha tuhuma hizi Mwanahalisi linaweza kurelease 'cables' ili tuone hizo sms zinazoleta mashaka]

Mwanahalisi halikuweza kugundua mara moja undani wa mawasiliano ya Mh Zitto na Zoka
[Ni mtego huu. Pengine hapa ndipo Mh Zitto na Zoka ndipo waanatakiwa watuweke sawa na kwa umakini mkubwa maana bila shaka hawaju extent ya details ambazo Mwanahalisi inazo]

Shaka ya baadhi ya wachunguzi wa mambo inatokana na ukweli kuwa Zoka ni mmojawapo ya vongozi wa TISS (kigogo) na Mh Zitto ni mwanasiasa kutoka chama ambacho kinaituhumu TISS kusaidia kuvuruga uchaguzi mkuu
[ I believe any skeptical mind would think the same!]

Nauliza: Hivi lini Mwanahalisi ilishindwa kesi ya kuwachafua watu. Lilikuwa gazeti pekee humu nchini liliandika majina ya ile list of shame -- ya wale mafisadi 11 wakiongozwa na JK mwenyewe. Nani alishitaki gazeti kwa hilo?

sana sana gazeti hilo hufungiwa na waziri kwani hatua hiyo haihitaji ushahidi wa kimahakama, ni wa mtu mmoja tu.
 
Sorry Zitto, I must part company with you. When you were throiwn from Mjengoni, you were my great inspiration and I said you could even be fit to be Presida! But noy you are just a puppet -- bought by a few coins stolen by mafisadi from the wananchi. You have let me dowm, I'm striking you off!
Na bado! In 2 to 3 years time from now, you will have striken off few dozens of your hitherto political inspirers! Not only Zitto, start also watching Hamad Rashid, Sitta, Mwakyembe, Mengi, Mabere Marando, Anne Kilango, Mbatia and even Mbowe and Slaa! We can not let this country go to the dogs!
 
Reading through most of the comments I think there is an oversimplification on the part of many of us; especially those that have not bothered to carry out some investigations before commenting. A little bit of research will reveal that most of the allegations contained in the article arise from distorted facts; whether this is intentional and politically motivated or just a case of honest mistakes is something else, however; and I make no judgement on that.

As for Zitto,would you care enough to defend yourself against these allegations? Kumbuka watu wanakuamini bado....kama kuna uwongo,ukiachwa utageuka kuwa ukweli and it wont be good,na kama kuna uwongo ukauacha still utakuwa ume-betray comfidence uliyopewa! Cheers!
 
Na bado! In 2 to 3 years time from now, you will have striken off few dozens of your hitherto political inspirers! Not only Zitto, start also watching Hamad Rashid, Sitta, Mwakyembe, Mengi, Mabere Marando, Anne Kilango, Mbatia and even Mbowe and Slaa! We can not let this country go to the dogs!

Kitu gani kinakufanya ufikirie nitafanya hivyo? Hata hivyo nakuhakikishia kwamba Zitto ka-nipain sana sana sana! Nilimuamini kupita kiasi, kumbe bure!
 
Ukienda kuangalia OPERA, huwa kuna vikaratasi wanatoa ili uelewe nini wanacheza. Usiposoma hicho, utatoka mweupe.

Siku nyingine soma kwanza utangulizi na si kurukia habari katikati na kutoa hukumu.
naona umejaza si kweli kibao,kwamba hamna la kweli hata moja wanaandika hawa watu au?
 
Kitu gani kinakufanya ufikirie nitafanya hivyo? Hata hivyo nakuhakikishia kwamba Zitto ka-nipain sana sana sana! Nilimuamini kupita kiasi, kumbe bure!
Oh, pole sana! I am politically sorry for you! Hiyo ndiyo siasa! Usije ukaweka mayai yako yote kwenye kikapu cha siasa! Ukiwa mwanasiasa hata wewe mwenyewe usijiamini kwa asilimia mia. Hata Shibuda aliwahi kuapa kwamba kamwe hatoki CCM, atapambana humo humo CCM hadi kiama! Yuko wapi sasa?
 
It depend kama kwako wewe hizi political tabloids ambazo mmiliki wake ni Mweka Hazina wa CHADEMA ambaye kwa miaka zaidi ya mitatu hajawahi kupeleka mahesabu yake katika kamati kuu ya chama kama katiba inavyotaka, hajawahi kukusanya mrejesho wa matumizi ya RUZUKU tangia tangia sheria ya kumtaka hivyo kupitishwa miaka miwili sasa, hajaweza kukabidhi bajeti ya vyanzo vya mapato na matumizi ya uchaguzi, nafasi yake haina baraka ya kamati kuu kama ambavyo katiba ya chama chao inataka na sasa yupo katika mkao wa kula wa nyongeza ya RUZUKU kutoka shilingi milioni 73 hadi mamia ya mamilioni mwengine....

This is the most desperate fight I have aver seen adopted by fisadi of any caliber. Kwao wao wako tayari chama kuvunjika na kupoteza heshima yote waliyoijenga kutokana na uchaguzi mradi kuhakikisha kuwa wanalinda uozo na maslahi yao binafsi.....

Ni wazi kuwa mhusika huyu sio mwandishi wa makala hizi za fitina, chuki na uzandiki lakini ni wazi ameamua kutumia desperate measures to cover his and his boss.........................

Thanks GOD for giving me the strengths to fight the temptations to join this gang of thugs camouflaging in democratic card...

Nawashangaa mnaomsapoti Zitto, Nashangaa Zitto ni kwanini hajajiuzulu kama alivyofanya Shitambala, nashangaa CDM kukaa kimya kuhusu Zitto na Tbc1. Ule ukali wa Dr. Slaa upo wapi? Nashangaa Komu na tuhuma zake zinaibuka leo. Nashangaa ni kwanini naandika haya. Nashangaa Zitto ndo nani. Nashangaaa, nashangaaa.

Alhaj Awadhan S.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom